Bado sijaona faida ya Elimu ya Tanzania hasa Chuo Kikuu na kidato cha sita

Mpaka nifanye utafiti .....ila nilishasoma kitabu cha donald trump alikuwa anakisifia chuo alichosoma kuwa kilimuandaa kuja kujiajiri.
Mkuu hio kumuandaa ni kutokana na matario yake yeye sasa wewe angalia kwamba katika darasa la aliosoma nao wote wamejiari?
 
Jamaa umeandika mapupu tulioyazoea. Kunanyuzi zaidi ya elfu sabini mia nane humu, zote zinazungumzia ukurutu huu.
 
Umeanza vizuri ila mwisho unataka tupige goti kwa mabeberu wa ukoloni maomboleo watwambie nini hatima ya vijana wetu, aibu gani hii kama siyo fedheha! Rudisheni tawala za kichifu na abakama, muone kama vijana watakosa ajira. Rudisheni jando na unyago, muone kama kuna kijana atakosa elimu sahihi kwa mazingira yake. Unaposema kompyuta liwe somo la lazima, unasahau kwamba dunia ya sasa inaendeshwa na automation chini ya mfumo wa A.I(Artificial Intelligence). Nimalize kwa kusema mwanadamu haitaji elimu ya mfumo rasmi ili aishi, ila mfumo rasmi ndo unamwitaji mwanadamu ili uendelee kuwepo. Tukiua mfumo rasmi wa kielimu tutakuwa tumejikomboa katika nyanja zote kimaisha.
Sawia kongole!!!!!
 
Sjaona connection ya title na content..so watu wasiende vyuo sasa..kisa tu elimu inamuandaa mtu kuajiriwa....huhuhu
Wewe pia ni matokeo ya elimu ya kukariri anayozungumzia mle uzi. Yaani elimu ambayo haifanyi mwanafunzi kuelewa mambo.
 
Mambo ya msingi ni kujadili Bernard Morrison amefuga ndevu

Mambo ya msingi ni kujadili Manara ameachana na Mke wake

Mambo ya msingi ni kujadili Mo Dewji ndio kila kitu Simba


Mambo ya msingi ni kujadili Mbona Rais Samia amevaa Gwanda la JWTZ


Mambo ya msingi ni kujadili Rais Kikwete ana miwani nzuri


Kwa mawazo kama haya tutafika tu
Halafu baada ya hapo wanaenda kubeti daaah...
 
Mambo ya msingi ni kujadili Bernard Morrison amefuga ndevu

Mambo ya msingi ni kujadili Manara ameachana na Mke wake

Mambo ya msingi ni kujadili Mo Dewji ndio kila kitu Simba


Mambo ya msingi ni kujadili Mbona Rais Samia amevaa Gwanda la JWTZ


Mambo ya msingi ni kujadili Rais Kikwete ana miwani nzuri


Kwa mawazo kama haya tutafika tu
 
1.Mimi naomba nitofautiane mtazamo kitu wasichokijua watu wengi ni kwamba wanafikiri elimu unayofundishwa au ya huko ughaibuni inamfundisha mtu kujiajiri au kuvumbua kitu..

2. Swala la kujiajiri au kuvumbua kitu ni suala la mtu binafsi na udadisi wa mtu huyo husika shuleni ama darasani haufundishwi wala nini ni wewe mwenyewe binafsi kuona changamoto inayokuzunguka na kuitafutia suluhisho ndo maana anaekufundisha wewe kujiajiri yeye mwenyewe ameajiriwa
ni kweli lakini.
 
Fahamu tofauti ya aina za elimu ambazo ni academic, professional and life halafu uamue ni elimu ipi unaitaka.

Degree, master, = Academic

CPA, CPB na professional zingine na law school= Profession

Kujua kusonga ugali wenye njaa wakakupa pesa ili washibe = Life.

Ukiwa na life qualification hakuna tatizo, utafanikiwa tu.

Ukiwa na hizo nyingine bila life una hati hati ya kufanikiwa. Sana sana wahindi watakunyoosha.
 
Kusoma form 5 na 6 ni kama kubeti tu,namshukuru mzee wangu alioiona hilo mapema.
Kwetu hata waliofaulu division za juu O level walipelekwa kusoma diploma za ujuzi vyuoni.
Faida yake ni kwamba ukijilinganisha na yule ambaye mmemaliza mwaka mmoja yeye kaenda advanced wote mtakutana mtaani baada ya miaka miwili,wewe unatoka na cheti ambacho una uhakika wa ajira moja kwa moja kitu ambacho kwake ni kigumu.
Na kama kafeli,jambo ambalo ni rahisi advanced,bado ni form 4 leaver.
Ukija vyuoni,vinaandaa wataalam wa kwenye theory na ndo mana wasomi wengi wana GPA za kutisha lakini ukimpeleka kwenye utendaji ni sifuri kitu ambacho kinapelekea ofisi nyingi kujaa fitna,majungu,ushirikina kujipendekeza nk.
VERY SAD.
Acha kufananisha advance na vitu vya hovyo, khaaaah
 
Mwanafunzi anatoka Nyantole kijijini umbwindeni kabahatika kwenda Chuo UDSM akienda maskini anarudi mtaan kaharibikaaaa...
Viwanja vyote anavijua.
Move zote anazijua yeye.
Watu maarufu Duniani ni yeye
Kutwa kucheza na Simu na kula chips

Mpaka wazazi wake wanaanza kumshangaaa mtoto wetu vipii huyu Tena.

Maana hata kulima tena hataki
Kuchunga hataki tena...Anataka akaishi mjini

TUSIPO KUWA MAKINI VYUO NI MAJIPU...

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Nimecheka hadi kupaliwa hapa lol,
 
Ukimaliz chuo 3 years umetumia mil 06 tu y serikali... Wakt hela ya ada ipo Kam namba tu udsm hailipwi na bodi! Hii million sita kwend China kujifunza elim yao Ni ndoto ngum sbab kuanzia nauli na makazi ya miez 3 hela kwisha. Nan atakugharmia 3 years!? Ni heri tungeitoa watto wakawekeze kwenye kilimo huku warsha mbalimbali zikiwaboresha
Kiimo kimewesaidia wangapi? Kila mtanzania alime? Mwenzio anatoa mtazamo wa uchimi wa kisasa, hata kilimo kifanyike kwa mtindo wa kisasa kuanzia machine, masoko, tafiti nk. Teknolojua ndio msingi wa maendeleo.
China imeendelea kwa kupeleka watoto katika nchi zilizoendelea na bado wanapeleka watoto mpaka muda huu.kisha watoto wanarejea na kuanzisha tafiti za kisasa.
 
Back
Top Bottom