Bado sijaona faida ya Elimu ya Tanzania hasa Chuo Kikuu na kidato cha sita

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
6,203
2,000
Kujua umuhimu wa elimu ni mpaka uwe nayo. Kama wewe hauna, umeishia darasa la 7, utajuaje faida ya elimu ya chuo sasa?
Elimu ya Tanzania imetumika miaka mingi kumuandaa kijana kuajiriwa na Serikali au Sekta binafsi, Watu ambao wamepata bahati ya kuajiriwa na mfumo huu wa elimu wao wanaona mfumo huu upo sawa kabisa

Mambo yanayoshangaza na kusikitisha zaidi watu wale wale ambao wanaona mfumo upo sawa wa elimu yetu wanahangaika kuwatafutia kazi vijana na ndugu zao maofisini kwa udi na uvumba

Mfumo wa elimu yetu tumeurithi toka kwa mkoloni, Mkoloni alimpa mtu mweusi elimu kwa lengo la mtu mweusi kuja kumtumikia mkoloni, Elimu aliyoitoa mkoloni haikumuandaa mtu mweusi kufikiri nje ya anachofundishwa darasani


Tangu mwaka 2000 mpaka sasa mwaka 2021 maelfu ya vijana wamehitimu vyuo vikuu ndani ya nchi, Waliobahatika kuajiriwa ni chini ya asilimia moja ya wahitimu wote

Kijana anatumia miaka takribani kumi na saba kutafuta elimu toka shule ya msingi mpaka Chuo Kikuu, Elimu ambayo nje ya cheti kijana hawezi kusimama na kujitetea

Tufanye kitu gani tutoke hapa tulipo na tusonge mbele kwa matumaini

Mosi, Watoto wetu wakishafanikiwa kujua kusoma na kuandika lugha yetu kwa ufasaha na lugha baadhi za kigeni, Wazazi pamoja na shule wawapime watoto wanahitaji wafanye kitu gani na wanapendelea kitu gani, Tuwaendeleze watoto kwa vitu wanavyohitaji na baadhi kama masomo ya teknolojia yawe ya lazima

Masomo ya lugha za computer yaani Coding yawe ni lazima kwenye elimu ya msingi, Masomo ya kutengeneza App yawe ni lazima hapa kwenye elimu ya msingi. Watoto wafundishwe matatizo tulionayo na jinsi watavyoweza kuyatatua kwa teknolojia

Miaka mitano inatosha kwa elimu ya msingi kwa watoto wetu kuweza kuelewa Basics au msingi wa wapi tunalipeleka Taifa hili

Pili, Hakuna haja ya vijana kusoma masomo zaidi ya kumi Katika ngazi ya kati ya Sekondari yaani Kidato Cha kwanza mpaka nne, Kidato Cha kwanza mpaka nne kiwe ni kipindi cha vijana kufundishwa mahesabu na teknolojia, Masomo ya Kompyuta kwa vitendo na Matumizi ya mahesabu kwa vitendo ndio muda wake hapa

Nafahamu hatuna walimu wenye uwezo wa vitendo na wala hatuna maabara za kuwaandaa hawa vijana, Lakini ni muda muafaka kuanza na shule chache na kuingia gharama za kuazima walimu toka China na Marekani


Tatu, Watoto wakitoka Kidato Cha nne waelekee vyuo vya kati vya kisasa sio hizi Amazoni College au University of Iringa au University of Dodoma au Sua au Udsm( Hivi ni vyuo ambavyo watoto wanaandaliwa kukariri mambo ili wafaulu tu mitihani na kutafuta ajira)

Elimu za vyuo kama Udsm, Sua, Udom na rafiki zao kama IFM na CBE vilishafeli kitambo sana kwa kutoa elimu za kukariri

Vyuo vya kati ndio ambavyo ilipasa pesa za IMF za corona na baadhi ya mikopo kuelekeza kununua mitambo ya kisasa ya computer na Machine za high Tech kwa ajili ya vijana kujifunza

Nne, Urafiki wetu na Mabeberu ulenge kutujengea uwezo na tuwatumie mabeberu vizuri, Pesa za Loan Board zitumike kuwapeleka vijana Field huko Google, Amazon, NASA, Microsoft. Na baadhi wapelekwe kwenye mazoezi huko London School of Economics wakajifunze, Harvad School of Medicine.

Ni muda wa kukaa chini na Balozi wa Marekani na China kuongea nao kuhusu mpango wa vijana wetu kila mwaka zaidi ya Mia tano kwenda kujifunza mazoezi kwenye taasisi zao za teknolojia za kati na kubwa ili tuhamishie uwezo wa teknolojia Nyumbani

Tano, Kundi la vijana wapenda masomo ya historia na Sanaa lipewe kipaumbele kidogo tofauti na sasa, Vyuo vyetu wamejaa vijana wa masomo ya uchekeshaji na uigizaji, Uigizaji Katika sociology, Political science, Fine art na watoto wao wanaolingana

Sita, Walimu wetu wa vyuo vikuu hawana uwezo wa kumuandaa kijana tena kujitegemea, Walimu tulionao sasa ni zao la watu waliokariri mambo kwa muda mrefu sana

Ni muda tupate walimu wa vitendo, Hawa walimu wa nadharia wa kuandaa notes na kutunga Test hawatufai tena hapa Tanzania

Serikali iwaondoe walimu wasiokuwa na umuhimu vyuo vikuu hasa wale ambao hana uwezo wa vitendo, Waletwe wataalamu toka China na Marekani kupima uwezo wa hawa walimu wetu Katika kila sekta toka Engineering, Accounting mpaka kozi za usanii


Nje ya Cheti cha darasani, Vijana waliomaliza chuo kikuu kwa sasa hawawezi kusimama, Ukimpokonya cheti chake ukamuuliza Haya sasa simama songa mbele lazima atadondoka tu

Tujiulize maswali muhimu kwa lengo la kusaidia hawa vijana wetu

Je kijana anapomaliza chuo kikuu mfano udsm au udom, Sua. Tukichukua cheti chake atafanya kitu gani huku uraiani, Walimu wa vyuo vikuu hawana uwezo kuwaandaa vijana tena kwa sasa

Je kila kijana neno kujiajiri ni kuuza nguo, maandazi, Nyanya, Mikate, mitumba na kuanzisha duka kariakoo?

Hitimisho
Tuna watu ambao wamesoma na wamepata taaluma ya vitendo kwa juhudi zao na ujanja wao, Ni muda wa kuwatumia hawa watu, Kuna watu wanafanya kazi Serikalini na Sekta binafsi wana uwezo mkubwa kwa vitendo kuliko hawa walimu waliopo vyuo vikuu kwa sasa,

Ni kuboresha mazingira tu na kuwa ondoa walimu wote ambao hawana uwezo kufundisha kwa vitendo

Mazingira yakiboreshwa hata mimi Gussie Nipo tayari kwenda Front line kugawa mbinu za kupambana kwa wanafunzi wetu kisiasa na hata kukabiliana na Biashara za kimataifa na kuachana na hawa wabunge wa kujua kusoma na kuandika tu

Tusipowaza matumbo yetu na Mamlaka tunaweza jenga Taifa imara kwa watoto na Vizazi vijavyo
 

JABALI LA KARNE

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
2,608
2,000
Fahamu tofauti ya aina za elimu ambazo ni academic, professional and life halafu uamue ni elimu ipi unaitaka.

Degree, master, = Academic

CPA, CPB na professional zingine na law school= Profession

Kujua kusonga ugali wenye njaa wakakupa pesa ili washibe = Life.

Ukiwa na life qualification hakuna tatizo, utafanikiwa tu.

Ukiwa na hizo nyingine bila life una hati hati ya kufanikiwa. Sana sana wahindi watakunyoosha.
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
16,044
2,000
Ni kweli elimu ya bongo inashindwa kuwakomboa wengi walioipata kifikra na kiuchumi pia. Graduates wengi bongo ni watupu sana kichwani na mifukoni pia.
 

Cryptographer

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
315
1,000
Kusoma form 5 na 6 ni kama kubeti tu,namshukuru mzee wangu alioiona hilo mapema.
Kwetu hata waliofaulu division za juu O level walipelekwa kusoma diploma za ujuzi vyuoni.
Faida yake ni kwamba ukijilinganisha na yule ambaye mmemaliza mwaka mmoja yeye kaenda advanced wote mtakutana mtaani baada ya miaka miwili,wewe unatoka na cheti ambacho una uhakika wa ajira moja kwa moja kitu ambacho kwake ni kigumu.
Na kama kafeli,jambo ambalo ni rahisi advanced,bado ni form 4 leaver.
Ukija vyuoni,vinaandaa wataalam wa kwenye theory na ndo mana wasomi wengi wana GPA za kutisha lakini ukimpeleka kwenye utendaji ni sifuri kitu ambacho kinapelekea ofisi nyingi kujaa fitna,majungu,ushirikina kujipendekeza nk.
VERY SAD.
 

Mamserenger

JF-Expert Member
Oct 14, 2019
1,021
2,000
Mi binafsi huwa najiuliza sana maswali.
Bara bara zetu zina Jengwa na Mchina mpaka leo na kwa Gharama kubwa sanaa tena Gharama hizo zikihusishwa na ununua aji wa Vifaa ghali sana kutoka huko huko kwao.
Lakini pale UDSM kuna wanafunzi wanajifunza Engineering na kila mwaka wanamwagika mtaani.

Sasa inashindikana ninii sisi wenyewe tukanunua vifaa vyetu wenyewe kutoka huko kwao na walimu kutoka huko kwao wakawafundisha wanafunzi wetu wa Chuo jinsi ya kupima na kuchonga bara bara na kuzijenga wao wenyewee.
Maana nijambo la aibu mpaka sasa Mchina anapewa kandarasi za kujenga bara bara.

Pia hata Majengo juz juz nimeoma kuna Jengo la Science kule Dodoma kapewa mchina kwa mabilion ya pesa wajenge waoo na huku tuna wahitimu vyuoni wanchora kufanya Design mbali mbali.

Kweli tusipo Jitambua tunayumbaaaaaa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 

mbwewe

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
3,250
2,000
1.Mimi naomba nitofautiane mtazamo kitu wasichokijua watu wengi ni kwamba wanafikiri elimu unayofundishwa au ya huko ughaibuni inamfundisha mtu kujiajiri au kuvumbua kitu..

2. Swala la kujiajiri au kuvumbua kitu ni suala la mtu binafsi na udadisi wa mtu huyo husika shuleni ama darasani haufundishwi wala nini ni wewe mwenyewe binafsi kuona changamoto inayokuzunguka na kuitafutia suluhisho ndo maana anaekufundisha wewe kujiajiri yeye mwenyewe ameajiriwa
Nchi km marekani vipo vyuo ambavyo vimejikita kwenye elimu ya kujiajiri wenyewe wanaviita business school....trump na matajiri wengi wa marekani wamesoma kwenye ivo vyuo
 

mbwewe

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
3,250
2,000
Mi binafsi huwa najiuliza sana maswali.
Bara bara zetu zina Jengwa na Mchina mpaka leo na kwa Gharama kubwa sanaa tena Gharama hizo zikihusishwa na ununua aji wa Vifaa ghali sana kutoka huko huko kwao.
Lakini pale UDSM kuna wanafunzi wanajifunza Engineering na kila mwaka wanamwagika mtaani.

Sasa inashindikana ninii sisi wenyewe tukanunua vifaa vyetu wenyewe kutoka huko kwao na walimu kutoka huko kwao wakawafundisha wanafunzi wetu wa Chuo jinsi ya kupima na kuchonga bara bara na kuzijenga wao wenyewee.
Maana nijambo la aibu mpaka sasa Mchina anapewa kandarasi za kujenga bara bara.

Pia hata Majengo juz juz nimeoma kuna Jengo la Science kule Dodoma kapewa mchina kwa mabilion ya pesa wajenge waoo na huku tuna wahitimu vyuoni wanchora kufanya Design mbali mbali.

Kweli tusipo Jitambua tunayumbaaaaaa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Wanampa mchina sababu anawakopesha ni ivo si vinginevyo
 

Mamserenger

JF-Expert Member
Oct 14, 2019
1,021
2,000
Mwanafunzi anatoka Nyantole kijijini umbwindeni kabahatika kwenda Chuo UDSM akienda maskini anarudi mtaan kaharibikaaaa...
Viwanja vyote anavijua.
Move zote anazijua yeye.
Watu maarufu Duniani ni yeye
Kutwa kucheza na Simu na kula chips

Mpaka wazazi wake wanaanza kumshangaaa mtoto wetu vipii huyu Tena.

Maana hata kulima tena hataki
Kuchunga hataki tena...Anataka akaishi mjini

TUSIPO KUWA MAKINI VYUO NI MAJIPU...

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 

Mamserenger

JF-Expert Member
Oct 14, 2019
1,021
2,000
Wanampa mchina sababu anawakopesha ni ivo si vinginevyo
Sawaa anawakopesha lakini bado tuna uwitajio mkubwa sana wa bara bara na majengo...

Basi walimu wa vyuo na wanafunzi wa kozi flan wafanye Project ya kwao kwa kila kozi vyuoni kwa kupitia mashirika ambayo yanatoa mkopo kwa serikali katika zile changa moto.

Mfano ule Mkopo wa mabilion ya Corona basi yangejenga maabara kubwa ya kisasa ili siku zijazo tusije shindwa pambana na gonjwa la mlipuko unaotokea.


Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 

Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,713
2,000
Nchi km marekani vipo vyuo ambavyo vimejikita kwenye elimu ya kujiajiri wenyewe wanaviita business school....trump na matajiri wengi wa marekani wamesoma kwenye ivo vyuo
Mkuu wakikuambia business school wanamaanisha unapewa elimu tu ya biashara..embu vitaje tu walau vitatu au vitano..
 

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,742
2,000
If you believe education is ignorance try stupidity and you'll yearn stupidity altogether with ignorance².
 

mbwewe

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
3,250
2,000
Mkuu wakikuambia business school wanamaanisha unapewa elimu tu ya biashara..embu vitaje tu walau vitatu au vitano..
Mpaka nifanye utafiti .....ila nilishasoma kitabu cha donald trump alikuwa anakisifia chuo alichosoma kuwa kilimuandaa kuja kujiajiri.
 

Mamserenger

JF-Expert Member
Oct 14, 2019
1,021
2,000
If you believe education is ignorance try stupidity and you'll yearn stupidity altogether with ignorance².
Unachanganya elimu na Fani kakaaa.
Elimu ya Form four tuu inatosha kabisa kukuongoza mtaani...Maana inagusa vipengele vyote kuanzia kuamka kwako na magonjwa na kila kitu.

Ila Chuo ni fani na kazi ndo kitu kikubwa.
 

Jorojik

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
3,936
2,000
Mfano, Unaenda chuo kikuu miaka mitatu kusomea How Africa were colonilized by British Halafu wanaongezea kozi ndogo ndogo ishirini inaitwa BA in History and Political Science
Hilo tatizo la viongozi wa vyuo ku-frame mitaala bora Kwa vyuo vyao. Sasa kama Ndalichako ni Profesa unategemea nini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom