Bado sijaelewa walikusudia nini hawa wanawake

kindigiwa

Member
Apr 5, 2020
84
132
Waungwana habari za mihangaiko ya hapa na pale na harakati za kujikinga na ugonjwa wa nyumonia!

Mwaka 2000 nilianza kidato cha Kwanza shule moja ya Sekondari iliyo kuwa ina milikiwa na jumuiya ya wazazi wa ccm iliyo kuwa ikijulikana kwa aka Nandungutu ipo kule wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Darasani kwetu kulikuwa na msichana mmoja ambaye alikuwa hanivutii kimapenzi na alikuwa mkimyaa sana hali iliyo nifanya nimuweke karibu sana kwangu kwa kumtania mchumba mchumba,hadi darasa lote walikuwa Wana jua kuwa namtania mchumba wangu,baada ya muda mrefu kupita kuna siku moja ya jumapili huyu binti na wenzake walikuja home(nilikuwa na kaa home)wao Wana kaa bweni na pale home Mara nyingi nilikuwa peke yangu kwa kuwa wazazi na ndugu zangu wengine walikuwa Wana ishi mji mngine pale Namtumbo mzee alikuwa amejenga nyumba.

Walikuja mabinti wa tatu mmoja wao alikuwa yule niliye kuwa nikimuita mchumba,tulipiga story sebuleni kisha wakaenda zao kuwahi kuhesabiwa shuleni.

Baada ya kumaliza mwaka wa Kwanza mimi nilihama kuhamia kule walipo kuwa wazazi na ndugu zangu wengine hivyo kuanzia kidato cha pili siku somea tena pale Nandungutu,kule Namtumbo nilikuwa nakwenda likizo Mara nyingi,nakumbuka likizo moja nakuja pale nakutana na habari kwamba yule binti ni mja mzito na anelezea kuwa mimi ndiye mwenye ile kitu!!! Mwanzo ni sikutilia manani hasa nikijua kuwa ni habari na zo zipata kwa jamaa zangu niliamini ni masihaara hasa nikikumbuka kuwa Wanajua nlivo kuwa niki mwita mchumba yule binti,labda niseme kuwa pale mwanzo nili mwita mchumba sikuwa na lengo lolote na yule binti ila siku zivo zidi kusonga yule binti alikuwa kama vile kapata faraja moyoni mwake akaanza kuchangamka ule ukimya wake /uzubavu ukamtoka kabisa aka jihisi naye ni pisi kali pale class lakini kiukweli kabisa sikuwa na mtamani hata kidogo bali nilikuwa namtamani shangazi yake ambaye naye tulikuwa naye darasa moja shida ikaja kila niki tema voko yule anti yake anachomoa kwa kigezo kuwa akija jua anti yake haita kuwa poa licha ya kuwa alijua mi nilikuwa na mchombeza tuu yule anti yake.

Basi bhana nilikuwa nakula vijisenti vya yule mchumba fake wangu kwani familia ya o ilikuwa nauwezo kifedha kwani baba ya yule binti alikuwa mfanya biashara maarufu pale sokoni Namtumbo akiuza bidhaa yake yakutoka ziwa Victoria huko!

Siku zikapita ishu ya ujauzito ya yule binti ikatinga kwa mzee wangu yule baba wa mchumba fake wangu alimtuma mtu kwa mzee kuuliza mipango yangu juu ya binti ni ipi?

Basi mzee akampa jukumu mke wake yaani mama yangu anipe ujumbe wangu ili ni waeleze nilikuwa na fikiria kitu gani hata nitie mimba binti ya watu na sasa wenye binti yao wanataka kujua huko,hapo ndipo nlipo shikwa na mshtuko kumbe ile ishu nloiskia kwa jamaa zangu ni serious!!! Nika jiuliza maswali mengi siku hiyo sikupata majibu nika mwambia mama yule mwanamke hata kiuno chake kina fananaje sijui kwani sijawahi mshika hata titi lake!

Mama aliniuliza mara tatu ikiwa nacho kisema ndicho ninacho maanisha?nami nika mjibu haswaa hivyo ndivyo ilivyo kifupi marehemu mama yangu alikuwa kama rafiki yangu tulikuwa tuna ongea mengi sana hasa ya kuhusu mahusiano alikuwa akinisihi sana kujiepusha na papuchi nakumbuka kuna siku kaja home ana tuita watoto wake anatua mbia "haya kila siku nawaambia kuhusu ukimwi nendeni pale mkamuone mtu mwenye ukimwi alivyo konda ndiyo mjue ukimwi ni hatari"

Basi mjumbe hau awi mama akarudisha jibu kwa mzee kuwa mwanao kasema hajawahi hata kushika titi la huyo binti hata yeye anashangaa hizo habari!

Mzee aka mjibu yule mjumbe jibu nilo wajibu na mjumbe kwa mshangao mkubwa akalibeba jibu lake na kulipeleka kwa wahusika.

Nilipo pata likzo nilikwenda kule Namtumbo bahati nzuri nlikutana na mwanamke tena akiwa kisha choka maskini na tumbo lake aliishiwa pozi alipo niona nami nilimuuliza tuu mimba ya nani hiyooo kiukweli yule mwana mke hakuongea chochote natoka hapo sija kutana na ye hadi hii leo na bado sija elewa alikuwa na kusudio gani kutaka kunipa mimba isiyo nihusu ilihali anajua kabisa sikuwahi kufanya naye chochote ambacho kinge pelekea yeye kupata ile mimba!

Pia kuna binti mwengine huyu nlimega tunda ki masihara na bimkubwa alinifuma geto niki mla huyu binti lakini niligundua siku ile yule binti tayari alikuwa mjamzito na mimi ndiyo ilikuwa mara yangu ya mwanzo namla cha ajabu baada ya kujuikana ana ujauzito yule binti aka waeleza home kwao ule ujauzito ni wakwangu,hapo nilipata wakati mgumu kwa mama kuelezea kuwa ile kitu siyo yangu sababu alinikuta nayule binti licha ya kujitahidi kuji express my self bimkubwa akanichana kama ulichomoka yule hatukuwa na ushahidi huyu ushahidi tunao wacha tusubiri azaliwe tuangalie!

Naamini wao walijua yule binti nilikuwa na saga kitambo kumbe mwenzao sikuile ndiyo ilikuwa na test kwa mara ya mwanzo baada ya kusumbuliwa sanaa!

Basi bhana baada ya kujifungua yule binti bimkubwa alikwenda mtazama yule mtoto alipo rudi akatuambia kweli yule siyo wetu mwenyewe alisema eti amemtazama vidole hafanani na sisi kabisaa!

Bado najiuliza ilikuwaje hawa Wana wake waamue kunipa watoto wao kama zawadi wkijua kabisa mimi siyo baba ya watoto wao!!Tena afadhali hata huyu mwengine nilihusika hata kuchangia kidogo manake baada ya kupita miaka kama mitano nilkutana na mama mmoja aka ni simamisha kwa heshima zote na kunislimia kwa adabu na kujitambulisha kuwa yeye ni mama mdogo wa fulani akimtaja huyu mwanamke niliye fumwa naye na akisema kuwa eti nime fanana na yule mtoto!!!
 
Tulia Fanya chaguzi sahihi
Epuka kuwakimbilia wanawake ovyoovyo
Angalia Moyo wako
Siku zote tamaa ndiyo inayotuponza ndio maana unakuja hats kupewa/kusingiziwa mimba isiyokua yako
 
Tulia Fanya chaguzi sahihi
Epuka kuwakimbilia wanawake ovyoovyo
Angalia Moyo wako
Siku zote tamaa ndiyo inayotuponza ndio maana unakuja hats kupewa/kusingiziwa mimba isiyokua yako
Hiyo ilikuwa miaka mingi imepita leo nina mke na watoto pia,najaribu kujiuliza hawa Wana wake walikusudia nini hata wachukue maamuzi yale!!
 
Unavyoandika sasa duu! Mwl wako wa darasa la pili hakuwa.mkaguzi mzuri wa mwandiko?
 
Unavyoandika sasa duu! Mwl wako wa darasa la pili hakuwa.mkaguzi mzuri wa mwandiko?
Alipiga hadi aka choka basi ikabidi aniache na mwandiko wangu ndiyo hadi leo na hangaika nao huku duniani huu mwandiko!!
 
Back
Top Bottom