Bado natafakari kauli hizi za Rais Magufuli siku ya Mei Mosi

kaishebo

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
819
579
"....nimezoe kufuta futa Sherehe, na hii nilitaka kuifuta ili pesa ikafanye mambo mengine.......nikaona nikubali maana Wafanyakazi mna mambo mengi mnayadai".
Nisichoelewa; Hivi sherehe hizi ni za Rais au ni za Wafanyakazi?.
Kama Mkoba na wenzake wangeamua kumwalika Kingwendu awe Mgeni Rasmi, JPM angezuia?


"...........msiwaruhusu wageni kufanya kazi nchini kwa kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania".
Ninachoelewa; Katika Makubaliano ya Mtangamano wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAM) ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya, Burundi,Rwanda na Sudani Kusini ni kwamba kila raia wa nchi hizo ana uhuru wa kufanya kazi yoyote ndani ya nchi yoyote mwanachama ili mradi afuate taratibu za nchi husika ; mfano, kulipia vibali vya kuishi na kufanyakazi.

Rais alimaanisha nchi gani au hana habari juu ya hili?

Wajuzi wa mambo mtanielewesha kwa busara maana mimi ni mkulima.
 
Nina uhakika kuwa hizo nukuu ulizoweka hapo hazikuwa kwenye hotuba yake, kama ikivyoandikwa na wataalamu wake (manuscript). Kwa maneno mengine, kila anapochepuka toka kwenye manuscript lazima ataropoka kiaina. Yaani, ndipo anaposema yaujazayo moyo wake.

Hata hivyo nafikiri huwa hana maana mbaya kando ya kubana matumizi na kuweka maslahi ya watanzania mbele.
 
uenda haitambui jumuia ya afrika mashariki,mfano kwa sasa serikali hairuhusu mtanzania yeyote kusomeshwa na serikali nje ya nchi ikiwemo nchi za afrika mashariki(Rwanda,Uganda ,Kenya,Burundi).
 
Back
Top Bottom