KABIDI BODO
Senior Member
- Jan 19, 2017
- 184
- 252
Bado natafakari hii kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda..
1. Tunaambiwa serikali kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 imetoa 33.33% tu ya pesa mpaka wakati huu tukiwa tumebakiza miezi miwili ili kumaliza mwaka wa kiserikali..
2. Mauzo ya hisa kwenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE) yameshuka kutoka 33bn hadi 3.3bn
3. Mfumuko wa bei huku mtaani ndio usiseme, ni hapa kazi tu kwa kweli..
4. Biashara zimezorota kwa kasi ya hatari, sitaki kuamini hawa wote walikua wapiga dili kama anavosema mkuu.. hadi wauza nyanya nao niwapiga dili...
5. Sekta nyingi zimekuwa zikishindana kupunguza wafanyakazi kwa kasi isiyo kifani....
Bado sioni mazingira rafiki ya kuigeuza Tanzania kuwa ya nchi viwanda zaidi naiona Tanzania ikiwa nchi ya viwonder.. Mpaka sasa hakuna dalili ya kiwanda kipya zaidi ya vile viwanda vilivyojengwa au vilivyoanza kujengwa wakati wa serikali ya awamu ya nne..
Washauri wa Serikali hii wajitathmini na kuamua hatima ya taifa hili vizuri kwa kuwashauri watendaji wote vizuri, kama hawashauriki basi watendaji hawa wajitathmini ili kulinusuru taifa mapema..