Bado nampenda japokuwa nilimwambia aoe mwanamke mwingine

Passed

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
561
156
Nifanyeje huyu mwanaume bado nampenda, kuna siku nilichukua simu yake nikakutana na text badae nikapata hasira nikamwambia aoe mwanamke mwingine, sasa amenivungia maana niliwaambia hadi ndugu zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jirudi mkayaongee kama bado ana nia nawe mtaendelea..
Tahadhari kubwa ; epuka kushika simu ya mpenzi wako na kuanza kupekua yasiyokuhusu
Nifanyeje huyu mwanaume bado nampenda, kuna siku nilichukua simu yake nikakutana na text badae nikapata hasira nikamwambia aoe mwanamke mwingine, sasa amenivungia maana niliwaambia hadi ndugu zake

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
Pregabalin wewe ulipomtamkia hivyo ulikua unampenda bado au baada ya kumpa maneno na kuingia mtaani ukapata changamoto ndio umeona ulikosea na kuanza kumpenda tena upya?

Mwombe msamaha anaweza kusamehe kama ulipoamua kumwambia aoe hukumwambia maneno gani mengine magumu
 
Pole sana kama bado unampenda kweli jitahidi muonane mmalize tofauti zenu, nakutakia mafanikio mema.
 
Ongeeni myamalize.

Lakini mkirudiana utegemee mambo kuwa hivyohivyo au hata zaidi, kuna uwezekano mkubwa.

Safari hii atakuwa na uhakika kuwa bila yeye wewe si kitu si chochote. Cha msingi ongeeni muelewane.
 
kabisa nmehisi ivo pia mpaka hapo mshikaji ana point za kutosha yan dada amekurupuka sana kafanya maamuzi akiwa na hasira
 
Kwa mwanaume aliyekamilika kila kitu,ni kawaida kuwindwa na totoz...kwa hiyo kukuta meseji na kuchukua maamuzi uliyofanya...ulikosea;cha kufanya tafuta muda mkutane na myazungumze
 
Back
Top Bottom