Bado naendelea kutafuta kibarua, nisaidieni ndugu zangu wana JamiiForums

Tamati

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,085
1,956
Hali bado tete siku hadi siku huku janga la Corona likiendelea kumea kila kukicha.

Hatma ya kupata riziki ya halali na ya kueleweka angalau mlo mmoja kwa siku bado giza nene. Kupata kibarua cha halali imekuwa changamoto sana kwa upande wangu. Najitajidi kuzunguka kila siku na kuomba kwa watu ninaoona wanaweza kunipatia kibarua ila nagonga mwamba.

Katika kuzunguka kwangu kote kutafuta kibarua nimebaini kuwa bila kujuana na mtu ni vigumu kupata kibarua.

Ndugu zangu wana JF naombeni yeyote mwenye kibarua hasa katika maeneo ya kibaha, Pwani (ninaishi Kibaha) anipatie ili niweze kufanya kazi ya halali na nipate riziki ya halali hatimaye niweze kupeleka mkono kinywani.

Tuendelee kujikinga na Corona na Mungu atuepushe na janga hili.
 
Ungefafanua pia kiwango cha elimu yako na ujuzi wa ziada ilionao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu si haba nimeigusa kwa kiasi chake, nina degree 1. Ila jambo kubwa linalonisibu nisiweke kipaumbele cha elimu yangu kwenye kutafuta kazi ni kuwa nina ulemavu wa usikivu(tatizo la kutosikia vizuri). Tatizo hili ndio linanipa changamoto katika kuinteract na jamii.

Ndoto yangu kubwa ilikuwa ni kujiajiri na nilianza kutekeleza ndoto zangu mwaka jana ila mambo yalikuja kuharibika( zaidi soma Wezi ni watu wabaya sana, wameniibia masufuria yangu yote kwenye kamgahawa, nimerudishwa jalalani - JamiiForums ). Sikuweza kuinuka tena hadi nikawa katika hali hii ya kukosa hata hela ya kula.

Sasa ndio nimeamua nitafute kibarua cha aina yoyote ili niweze kupata hela japo ya kula tu.
 
daaa pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom