moodykabwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2015
- 625
- 602
M/MWENYEKITI SANGA
Mimi kama mwanachama wa Yanga, na kama mtazania wa kawaida ukimya wako na viongozi wenzako wa Yanga na hata Matawi ya Yanga na mashabiki wake kuhusu Mwenyenyekiti wetu Yusufu Manji. Yani hakuna hata anaelizungumzia wala kugusia wanaendelea na maisha yao kama kawaida tu, kana kwamba mateso anayopata Manji mahabusu sio Mweyekiti wetu. Tujuzeni Manji yuko wapi?
Tukumbuke Yanga tumeishi na kwenda chooni kwaajili ya Manji tumefanyiwa mengi na tukajipa jina wakimataifa kwaajili yake na raha zote tunazo kula, lakini naona hakuna fadhila au hata utu mnaomfanyia Manji juu ya haya yanaondelea kwake.
Tukumbuke Mahakama ndiyo inayohukumu kwamba fulani ndiyo anakosa na sio polisi. Hapo alipo Manji ni mtuhumiwa kwahiyo nilitegemea ofisi ya klabu ya Yanga ingekuwa inatujuza kila kitu na alipo Manji tukampe pole zetu au nyie mukampe pole zenu na kumtembelea mara kwa mara. Na nyie kukaripia sheria zinapokiukwa juu yake.
Alipotajwa Mbowe Chadema walicharuka, alipotajwa Gwajima waumini wake walicharuka, lakini kwa upande wa Manji imekuwa tofauti. Yaani ameachwa kama mtoto yatima wote mmempuuza huku tunataka hela zake.
Nakumbuka mienzi ya nyuma Manji alitishia kujitoa Yanga. Tukamuomba sana, akarizia siku chache tukamtuhumu. Mengi yanahusika kumsumbua Manji ajitoe yanga. Tukachoma hadi magazeti yake na matusi juu, lakini Makonda kumzalilisha Manji tumetulia tuli.
SANGA TUNAHITAJI TAARIFA KWANZIA LEO KUHUSU MWENYEKITI WETU
Unaona kama kiongozi wetu ukitupa taarifa juu ya Manji uma ukajua tutapata faida sana? Umeona bora Manji ateseke peke yake ili uwafurahishe watawala? Ili wasisemwe?
Viongozi wa Yanga onyesheni vitendo vya kumsaport mwenyekiti wetu na muache uoga maana hao mnaowaogopa hawalipi hata mshahara mmoja wa mchezaji wetu.
Sanga najua kuwa. Inasemekana kuwa hakuna anayelijua taifa hadi awe amewahi kuwa ndani ya jela. Manji kuendelea kuishi maisha anayo ishi ndiyo analijua Taifa lake. Kwako makamu Mwenyekiti Sanga Je, Manji yuko Jela? Au yuko wapi?
Na nyie wana Yanga:
Mtu mwenye akili si yule anayejisikia kuogopa, bali yule aushindaye woga. Wanayanga tumekuwa waoga sana. Kuwahoji viongozi wa Yanga kuhusu Mwenyekiti wetu wa Yanga Yusufu Manji.
Ninaomba nikulize Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Sanga. Wewe ndiyo mbadala wa Manji kama hayupo wewe una taarifa zote za Manji. Je sisi wanayanga wengine tutapata wapi majibu ya Manji. Sanga popote ulipo tunaomba taarifa sahihi za Manji. Au nawe umefurahishwa anacho fanyiwa kiongozi wako. Mambo ya subirini tumechoka.
Tunahitaji kuona uhuru wa Manji “Kwa sababu kuwa huru si tu kutupa minyororo, bali kuishi katika namna inayoheshimu na kukuza uhuru wa wengine.”
Haiwezekani wanayanga wanaishi kwa kuambiwa Manji yuko nje ya nchi kwa matibu, hivi kweli Sanga makamu mwenyekiti wangu wanayanga tuishi kwa maneno ya mtaani kulishana wakati upo wewe wakutupa taarifa sahihi kuhusu Mwenyekiti wetu?
Nyuso za wanayanga zimejaa huzuni kubwa sana, nyoyo zao zimejaaa maumivu makubwa sana, fuuraha imetoweka katika klabu yetu kuhusu Mwenyekiti wetu Manji. Tafakari Je haya ndiyo malipo mnayo mlipa mwenyekiti wetu. Najiuliza zile kauli za kutuambia mwenyekiti kasema tutulie kisha na sisi tukazipokea kwa furaha. Manji ni mtu mwenye haiba ya hekima na busara sana Wakati naongea hivyo basi Sanga ulipaswa kutujuza kila hatua anazondelea kufanyiwa mwenyekiti wetu. Kuna methali inasema "Kimya kingi kina mshindo mkuu" mimi nasema kimya hiki ndani ya Yanga ni kuzidi kumuongezea mateso Mwenyekiti wetu. Kwa maana hakina madhara yoyote.
Sanga na wewe siku ukiwa na matatizo uukupotezeee?
Ni Mimi kijana wenu Moody Kabwe Comredy