Bado naamini nyapara hawezi kuwa mkuu wa gereza

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,260
7,198
Well, Nimeweka hii thread kuwa kumbusha na ku waambia wanajukwaa bado naamini kwamba " nyapara hawezi kuwa mkuu wa gereza " . Nyapara hahitaji kuwa msikivu ili asijelegezwa na mfungwa mvivu, mwenye hila. Nyapara hahitaji fikiria au kubuni utaratatibu , ila kwenda tekeleza kwa kufuata utaratibu aliopewa.

Nyapara hahitaki busara, kwani utaratibu aliopewa umebeba busara za waliouweka.

Nyapara hahitaji kujua haki za binadamu kwani waliomtuma wanahitaji kuzibana hizo haki ktk utaratibu.

Nyapara haachi kutaka sifa tena kwa sana, kwani hayo ndio maslahi yake. ndio furaha yake. Ndio chakula ya fahari yake.

Nyapara huhitaji chuja maneno yatokayo mdomoni kwake , kwani hata awaendeshao hawana muda wa kuyanasikia na wakiyasiki wanasikia machungu wapatayo ni adhabu ya kuingia gerezani.Nyapara akipata akili kidogo tuu,atajitambua kuwa nae ni mfungwa tuu.Ujasiri wa wa sifa ndio humuondesha.

Nyapara km askari wa mlango huhitaji kuwa na akili timamu , ili asijitambue , au kujiuliza sana kwa anachofanya.kwani kufikiri kidogo kazi mbaya hatofanya.

Sio kitu kigumu kufahamu mapema tuu kwamba nyapara mzuri hawezi kuwa mkuu wa gereza.
 
Sijui watu wanaotumia kila rasilimali ya nchi kuweka nyapara ktk nafasi ya ukuu wa gereza baadae hujisikiaje? Hujifunza nini au huwa tayari kuchukua njia gani.
 
Back
Top Bottom