Bado mwamko (consiousness) ni mdogo miongoni mwa Tanzania juu ya nchi yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bado mwamko (consiousness) ni mdogo miongoni mwa Tanzania juu ya nchi yao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dangire, Apr 19, 2012.

 1. Dangire

  Dangire JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Miongoni mwa mambo yanayochelewesha kasi ya maendeleo ya nchi hii ni kile kinachojulikana kama 'mwamko mdogo wa watanzania juu ya nchi yao'. Ni zaidi ya miaka 50 sasa tangu nchi hii ipate uhuru, bado tungali tunaishi katika hali ya 'ukondoo' (wengi hawawezi kujenga hoja, kuuliza swali,nk...ni watu wa ndio mzee!!!!!!). Hii imetokana na sera ya kikoloni ya kuwafanya watawaliwa watawalike (pasification policy).walitujengea woga kwa watawala,;walitupa elimu ya kwao ili tusijitambue na kuwatukuza wao; walituambia tuwapende maadui zetu (wao), nk.

  Matokeo yake, ijapokuwa tunasema kwa miaka ya hivi karibuni watz wameamka, ni wazi kuwa bado mwamko huu si wa kutufanya tuendelee.......we have to be more than active to respond to different happenings in our country. hebu fikiria, ripoti ya CAG ya hivi karibuni imeonesha ufisadi mkubwa sana serikalini, ambapo mabilioni na matrilioni ya pesa za wavuja jasho wa nchi hii zimeteketezwa na walafi wachache tu! huku hali ngumu na umasikini wa watanzania ukizidi kushamiri. Lakini bado watanzania tunasikiliza na kisha kusahau.......maisha yanasonga mbele!! hivi taarifa hizi hazitugusi???

  nchi za wenzetu kama malawi, msumbiji, nigeria, zambia, nk. huandamana kwa kupanda bei mkate, mafuta, nk. kwa kiasi kidogo....sisi tunaridhika na hali hii iliyopo.......ama.........

  Mkisikia kesho ninaandama peke yangu naomba mniunge mkono.........am tired!
   
 2. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Still not understood you are title: ( consiousness ) or ( consciousness )
   
 3. Jehanamu Hii

  Jehanamu Hii Member

  #3
  Dec 19, 2016
  Joined: Dec 16, 2016
  Messages: 41
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Unajua nini huleta mwamko? Elimu. Watu wanapojua haki zao wanaanza kuzidai. Asilimia kubwa ya wananchi ambao ndiyo wenye mchango mkubwa sana wa kuwaweka viongozi madarakani hawana elimu. Hawajui hili wala lile. Wananachojua ni maisha yao ya kila siku tu, na wanafikiri maisha ndivyo yalivyoondokea kuwa na hakuna namna ya kuyabadilisha, Mungu pekee ndiyo awezaye kuyabadilisha! Wanasubiri muujiza wa Mungu. Elimu inahitajika. Mnaweza kuniona mjinga nikisema elimu ya kwanza inayotakiwa kuchangia kuleta kujitambua ni ile inayotolewa mashuleni, kuanzia ngazi ya shule za msingi, hadi ngazi ya sekondari na vyuo. Kwa bahati mbaya, elimu inayotolewa shule ya msingi haimjengi mtoto ku 'argue' kuhusiana na hoja yoyote inayotolewa. Ile ya sekondari vilevile. Mbaya zaidi ile ya sekondari inatolewa kwa lugha ya Kiingereza, lugha ambayo kwanza mwanafunzi haijui. Vipi unategemewa aelewe maudhui ya somo (elimu)? Eti mwanafunzi anafundishwa 'uraia' (civics) kwa kutumia lugha ya Kiingereza. Wakati bado hata ungetumia Kiswahili lugha anayoielewa bado bidii ingehitajika kumfanya mwanafunzi aelewe mantiki ya somo! Ukivuta lensi zaidi na kutazama yaloandikwa kwenye somo la 'Civics' au 'General studies' pia, bado hayasadifu hali halisi ya nchi. Hali mbaya ya 'ukoloni ndugu' (ukoloni unaosabaishwa na wananchi wenyewe ambayo ni serikali yetu) baada ya kupata uhuru kutoka katika ukoloni wa nje ya nchi. Inauma sana serikali yetu inatunyonya na ku 'take advantage' ya ujinga wa wananchi kwa kuwanyonya na kuwanyanyasa. Wale wachache wenye upeo na wanaojitambua nao washakata tamaa. Au wanaona hakuna maana yoyote kuhangaika na kutafuta au kudai haki au uhuru wa mawazo, na mambo mengine kama hayo. Ni wachache wanaoandika, wanaotoa hata maoni yao kwenye posti kama hizi. Itachukua karne nyingi kuja kukomboka tu kifikra kabla ya kukomboka kiuchumi, au katika nyanja zingine za kimaendeleo. Na hivi mtu kama Max anayejaribu kuwaweka watu pamoja kwa kutoa chombo hiki cha jamii forums kinachokutanisha mawazo ya wananchi pamoja anapewa mshikemshike na polisi? Nani mwingine atajaribu kusimama kuwaweka wananchi pamoja? Ni wale wenye hasira ya maendeleo tu ambao ni wachache sana katika nchi yetu.
   
Loading...