Bado Mizengo Pinda (PM) hajanusurika kuondoka madarakani. Hoja ya Zitto imeongezeka uthamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bado Mizengo Pinda (PM) hajanusurika kuondoka madarakani. Hoja ya Zitto imeongezeka uthamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Apr 28, 2012.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ndugu wanabodi,

  Suala la Kamati Kuu ya CCM {CC-CCM} kutangaza kwamba imemruhusu JK alisuke upya Baraza la Mawaziri linaweza kuwa limefanikiwa kubadili upepo wa uelewa wa wananchi. Nikiangalia hata thread mbalimbali humo ninaiona hivyo.


  Sijui ni wangapi wameshagundua kwamba kwamba maamuzi ya jana ya CC-CCM yameipaisha zaidi hoja ile ya "Kutokuwa na imani na Waziri Mkuu" badala ya kui-pre-empt.

  Ambao hawajanielewa, basi badala ya kukejeli thread hii ni bora wanisome between lines.

  Kwanza tuanze na kilichofikisha yote hapa. Kilicholeteleza yote haya ni mfululizo wa report ya Mkaguzi Mkuu (CAG) ambayo chronology yake ninaipanga kama ifuatavyo:

  01: CAG ku-submit report kwa Serikali
  02: Report kuifikia kama ya Bunge
  03: Report kusomwa mbele ya Bunge
  04: Report kujadiliwa na Bunge
  05: Mwitikio wa Serikali kwa hoja za Wabunge
  06: Zitto kutaarifu ukusanyaji wa sahihi 70
  07: Zitto kukusanya sahihi 70
  08: Zitto kuwasilisha hoja na sahihi zaidi ya 70
  09: JK kuitisha CC-CCM kuitishwa kwa ajenda ikiwa ni siri
  10: CC-CCM inamruhusu JK kufumua Cabinet yake

  Tuanze kuujadili mfululizo huu kifungu cha kwanza kwa kujiuliza, je, CAG ni muajiriwa wa nani? Anawajibika kwa nani? Kazi zake zinaripotiwa kwa nani?
  Ukweli ni kwamba Executive yaani Serikali ndiyo muajiri wa CAG. Ameajiriwa kwa kukagua matumizi ya Serikali.

  CAG si muajiriwa wa Bunge. Bunge haliwezi kumfukuza kazi kama report zake hazifiki bungeni. Kinachoweza kutokea ni Bunge kuishinikiza Serikali kumshughulikia CAG na si vinginevyo.

  Hivyo, report ya CAG, kituo chake cha kwanza ni Serikalini. Wakuu wa Serikali ni Rais, Makamu, Waziri Mkuu kisha Mawaziri yaani kwa kifupi Cabinet. Kumbe, watu wa kwanza kabisa kujua kilichomo kwenye report ya CAG ni Serikali.


  Sasa tujiulize, ni hatua gani zilichukuliwa na Serikali toka siku report ya CAG ilipofika mikononi mwao kabla ya mtu mwingine nchini kuiona. Mbona tume iliyopelekea Gavana Daud Balali ilipotoa report yake hatua zilichukuliwa ndani ya masaa 24 ya kutengua ugavana wa Balali. Kumbuka report ya Balali ilikwenda moja kwa moja kwa Rais mwenyewe wakati report ya CAG inasomwa kwa ushrikiano na President, Vice na PM. Tungetarajia ubovu uliokutwa kwenye report ya CAG ushughulikiwe kwa speed zaidi kwa sababu ya ushirika huu. Lakini hakuna uwajibikaji uliotokea.

  Tuje kipengele cha pili, taratibu zetu zimeruhusu report yaCAG ifike kwenye Kamati za Bunge. Ikishakuwa kwenye Kamati tayari kundi la wanaoujua madudu yaliyomo kwenye report linaongezeka. Mwanzo walijua timu ya Cabinet, sasa wanajua wanakamati, na tetesi zinaanza kuwafikia wabunge waio wanakamati. Hadi hapa siku zimeongezeka na bado hakuna kuwajibika mtu yeyote Serikalini.

  Tunaingia sasa kipengele cha 03 cha chronology, kwamba report ya CAG inasomwa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati. Hapa kundi la tatu kuelewa ubovu linaongezeka yaani wabunge wasio wanakamati. Ndipo sasa na sisi wananchi na tunaelewa upotevu uliomo kwenye report ya CAG.

  Inaposomwa Bungeni, Waziri Mkuu na Mawaziri wenzake, hapa si mara yao ya kwanza kujua kilichomo kama sisi na wabunge wasio wanakamati. Kwao hapa ni zaidi ya mara ya pili!
  Moyoni wanasema "upotevu waliouona kabla kabla ya wengine wote nchini, sasa unaanikwa hadharani". Hadi hapa, siku zimeongezeka na hakuna Waziri aliyewajibika.

  Hatua ya nne sasa ni report inajadiliwa vikali na wabuunge. Ukipitia hansard, utaona si CCM au upinzani ukishinikiza njia kadhaa za kuwajibika. Hivyo, muitikio wa kuwajibika kwa mara ya kwanza unaanza kujionyesha. Si kutoka kwa Waziri Mkuu au Waziri yoyote, ambao siku zinaongezeka za kuwa kuwa wamejua kilichomo ripotini, bali unatoka kwa Wabunge.

  Point ya tano, ni reaction ya mawaziri baada ya reaction ya wabunge. Kwanza wapo mawaziri ambao wakati wa mjadala ule mkali hawakuwemo. Kuna wakati wabunge walihoji kwa nini PM hakuwemo wakati wabunge wakihoji kwa ukali. Kuna wakati wakahoji kwa nini Waziri Mkulo hakuwemo wakati wa mjadala. Waziri Lukuvi ndiye alijaribu kuzima moto kwa kueleza grounds za absence ya PM na Mkulo.

  Reaction ya mwisho ya mawaziri ni kusema, sasa wamejifunza wanaenda kuwashughulikia watendaji wabovu. Hii inatamkwa na Aggrey Mwanri na wengine kadhaa. Zitto Kabwe anahoji kuna tofauti gani na pledge ileile ya mwaka jana kuwa watawashughulikia wakati walishindwa.

  Kwa kifupi ni kwamba hapa Serikali inakiri ubovu lakini action yake si kuwajibika bali kuwawajibisha wakosefu mle reportini.

  Kabla ya kujadili kipengele cha saba cha hoja ya kutokuwa na imani na PM, napenda tukubaliane kwamba hadi hapa, unajiuliza iweje Serikali nzima iliyomtangulia kila mtanzania kujua madudu yaliyomo mle ripotini ndipo sasa ionyeshe reactio tena ya ahadi.

  Tujiulize, kwa nini Serikali kuanzia Waziri Mkuu hawakujipanga mapema kwamba wawajibishwe watu Serikalini kabla hata Bunge halijakutana ili Bunge litakapoanza wawe walau wana cha kutueleza kuwa Waziri fulani ameshawajibika, au Waziri mkuu alishauri na ushauri wake Rais anaufanya kazi. Badala yake Bunge lilianza bila kuwa na response yoyote ya kiserikali kuhusu haya. Hivyo, ukitaka kuelewa mantiki ya kumuondoa Waziri Mkuu kwa kura ni vizuri kuuangalia mpangilio huu.

  OK, sasa Zitto katangaza adhma ya kukusanya sahihi 70 kama tunavyojua. Humu nimeweka hilo kwenye section 06. Haipiti siku tatu Zitto bila kutarajia anakusanya zaidi ya signature 70 na kisha ana-submit hoja kwa Spika. Hadi hapa hoja ya Zitto ya kumuondoa Waziri Mkuu haina tena kizuizi kikatiba, inasubiri siku 14 zifike na wakati wowote itinge Bungeni mapema iwezekanavyo. Narudia ni kwa mujibu wa katiba si kwa mujibu wa JK, Makinda, Zitto, CCM, CHADEMA au wewe na mimi. Ni kwa mujibu wa Katiba.

  Sasa, wakati tunasubiri siku14, ghafla juzi tunaambiwa CC-CCM wameitana na agenda tunambiwa ni siri. Tunaweza kuwa wataalam wa kubashiri watakachoongea CC-CCM lakini ukweli ni kwamba wamesema ni siri yao hadi watakapoifanya isiwe siri.

  Jana jioni tukatangaziwa siri hiyo, kwamba CC-CCM imekubali mawaziri wang'oke. Magazeti yanaripoti jinsi mwana-CCM aitwaye Mizengo Pinda akimweleza mwana-CCM, Jakaya Kikwete azimio la wabunge wa CCM kuitaka Serikali iwawajibishe mawaziri.

  Mwanzoni nilikuwa mmoja wa waliomtetea Pinda asiwajibike kwa hoja kwamba hatujui communication yake kama PM na bosi wake President yakoje hivyo sikuwa na haki kumhukumu kwa kutomshauri. Lakini hata hivyo, bado unajiuliza kama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, angekuwa amependekeza wateule wa Rais wawajibishwe, halafu Rais wa Tanzania akawa mbishi,
  Hiki ndicho kisa kilimfanya Julius Nyerere amsakame Waziri Mkuu, John Malecela kwamba kwa nini haku-resign kama Rais alikuwa anaelekea kumpuuza ushauri wake.

  Serikali iliposakamwa kwa tuhuma ra rushwa, yaani February 1990, Waziri Mkuu, Joseph Warioba aliamua ku-resign, na ikambidi Rais Ally Hassan Mwinyi aunde upya Serikali japo alimteua tena Warioba huyuhuyo kuwa PM na sasa wakazindua ufagio mrefu unaoitwa "fagio la chuma" la kufagia wala rushwa.

  Leo, Mizengo Pinda anashindwa kumshauri Rais kuwawajibisha wazembe serikalini, eti jana anaweza kumshauri kama mwana-CCM akifikisha azimio la wabunge wa CCM.

  Maana yake ni nini? Shinikizo na ushauri ule bado ni la wabunge na Pinda alifikisha taarifa kwa mwenyekiti wa CCM kuonyesha hali tete bungeni si kwa wabunge wa CCM tu.

  Kumbuka wakati huo, hoja ya Zitto inaendelea kukata mbuga kwa maana siku.

  HITIMISHO:

  Hivyo, hadi hapa huoni sababu ya kuendelea kuwa na Mizengo Pinda kama Waziri Mkuu wa Tanzania. Hoja ya Zitto ya kumuondoa Waziri Mkuu, inambana Waziri Mkuu aliyeshindwa kuwajibika tangu dakika alipopata report ya CAG, mapema kabla ya hata ya Kamati za Bunge.

  Kosa ninaloona kwa CCM ni kudhani kuwa azimio la jana la CC-CCM, litapunguza makali ya hoja hii kwa wananchi sasa wanaona "alichotaka Zitto ni kuwajibika, sasa mawaziri wanawajibishwa, Zitto anahitaji nini zaidi ya hilo?".

  Wanaodhani hivyo, ukweli ni kwamba hoja ya Zitto inazidi kupanda chat. Kitendo cha mwana-CCM, Mizengo Pinda, kuonekana kulizingumza na JK mbele ya wanakamati, kinathibitisha kwamba, mwana-Serikali, Mizengo Pinda, hakuitumia nafasi hiyo wiki zilizopita kutoa ushauri huohuo aliotakiwa kuutoa kabla suala halijatinga Bungeni.

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda angepona hoja ya Zitto, iwapo wangeenda Bungeni tayari mawaziri hao wameshakukuliwa hatua inayotaka kutekelezwa sasa.
  Hivyo, kushusha thamani hoja ya Zitto na wenzake 70, ni kulivunja Baraza zima la Mawaziri akiwemo Waziri Mkuu (disolve) kama alivyofanya Ali Hassan Mwinyi, Feb. 1990 na Dec. 1994.

  Vinginevyo, hata JK abadili Mawaziri wote (reshuffle), akaleta wengine wapya lakini Waziri Mkuu hakuguswa na mabadiliko hayo, basi hiyo tutaiita ni reshuffle na bado hoja ya Zitto itabaki na uzito uleule yaani Waziri Mkuu aliyeshindwa kuwajibika dakika ileile ya mwanzao alipohitajika kuwajibika.

  Samahani kwa urefu wa post, imenibidi nifanye hivyo
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Hivyo vimaandishi vyako usidhani ni wote tunatumia lens kusoma, hebu edit hiyo thread yako uongeza size ya maandishi otherwise naona unatuumiza macho tu.
   
 3. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  dah! Wabongo jamani. Kakuelewa nadhani.
   
 4. o

  oyaoya JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu, zipo tetesi WM aliwasilisha hoja ya kuwawajibisha mawaziri na watendaji husika kabla, (mbona hujaweka kwny hizo stages?) ikajibiwa "ni upepo tu, utapita"
  Wakuu, ikumbukwe si ishu zote za kiutendaji serikalini zinaanikwa hadharani, hivyo kinadharia (km ulivyowasilisha) hoja ya Zitto itatimizwa kwa kuwawajibisha wahusika kwa kuwa ndiyo lengo kuu la hoja na si kumwajibisha WM kwa kuwa yeye mwenyewe Zitto alikiri anampenda MP na anamheshimu isipokuwa wahusika wakiwajibishwa watakuwa wamemuokoa MP.
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu oyaoya usemayo ni kweli. Zitto hakumtaka waziri mkuu. Hoja ya Zitto ilikuwa mawaziri wanaotuhumiwa wajiuzulu na kama hawatajiuzulu basi wanamuweka rehani PM na wabunge watamchukulia hatua PM kwa kuwa wana uwezo naye. Hivyo kama mawaziri wataondoka Zitto atakuwa ametimiza lengo lake. Japo sioni Mtoto wa MKulima akibaki.
  Lakini pia mtoa hoja amesisitiza kuwa hoja ya kutokuwa na imani na PM inasubiri kujadiliwa na kwa mujibu wa katiba lazima ijadiliwe. Ukweli ni kwamba taarifa ikishapelekwa kwa spika basi spika ana uwezo wa kukubali ama kukataa hoja kuwasilishwa; kwa mujibu wa Katiba.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  asante kwa uchambuzi mwanana ndugu yetu
   
 7. G

  Greard Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nimejitahidi kusoma lkn siku nyingine jifunze kuandika thread fopi
   
 8. M

  MTK JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Good food for thought; kwa maono mengine ni kwamba PM pia alichukua attitude ya kusema kwamba ni upepo tu wa kisiasa utapita ili watanzania na wabunge wao washushe munkari hadi alipomsikia Mr. 2 akimwambia hiki ni kimbunga na destination ni yeye. unajua watu kama hawa kina PM ambao wamegeuza siasa kuwa taaluma ili waendelee kuganga njaa ni tatizo kubwa sana kwa nchi zinazoendelea na hasa ukizingatia na mifuma ya utawala na taasisi zetu.
  Itapendeza kama wabunge wetu wata push forward ili PM awajibike kivyake, hakuna sababu ya kumuonea huruma kama yeye hajionei huruma, falsafa ya "Funika kikombe mwanaharamu apite si faraja kwa taifa letu hata kidogo, PM purpots to be a devout and practicing Catholic lakini bado anacondone ubadhirifu kama huu!
   
 9. m

  mkurugenz JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  pm anaweza kuwa sasha kama reshafle itakuwa na tija vinginevyo budgetary parliament litamsumbua
   
 10. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kimbunga, hapo kwenye red. Hoja ikishakamilisha masharti ya kikatiba, hakuna kipengele chochte cha Katiba au Kanuni za Bunge kinachompa Spika uwezo mwingine wa kuikataa isifikishwe Bungeni.

  Kilichobaki ni mtoa hoja kuiondoa kama ameridhika na hatua zilizochukuliwa. Kumbuka sekeseke la G55 kudai Serikali ya Tanganyika ambapo licha ya Nyerere kupiga kelele Wabunge waliondoa hoja yao baada ya Zanzibar kujitoa kwenye OIC na wakaja na hoja nyingine mpya kabisa ya kura ya maoni.

  Spika akijipa uwezo usio ndani ya katiba, basi anajitakia matatizo yeye mwenyewe ya kukiuka katiba. Kumbuka aliyapata matatizo haya alipodanganya kuwa Tundu Lissu kashtakiwa kwa mauaji akasamehewa halafu ajitumbukize kwa jingine.

  Kosa la kuvunja katiba ni kosa la uhaini ambao hauna mjadala unatakiwa utoke kwenye kiti ulichokalia kwani kiapo chako ilikuwa ni kulinda katiba na si kuivunja.
   
 11. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu, wasilisho langu humu JF si kwa mtizamo wa kinadharia bali ni kwa mujibu wa Katiba. Zitto hakuwasilisha hoja yake kwa mujibu wa tetesi au nadharia yake. Ingekuwa ni nadharia basi hoja yake ingetupiliwa mbali dakika ileile ilipopokelewa.

  Kinachosubiriwa sasa ni siku 14 zitimie kwa mujibu wa katiba na si kwa mujibu wa matakwa ya binadamu anayeitwa Anne Makinda, Jakaya Kikwete au wewe au mimi au hata Zitto mwenyewe.

  Kila kitu hadi hatua tuliyopo na na tunayoelekea ni kwa mujibu wa katiba.

  Kinachoweza kuiondoa hoja ile wakati wowote sasa au baadaye ni kitendo cha Zitto mwenyewe kwenda kuichoma isiendelee na utaratibu unaoelezwa ndani ya katiba.

  Ukilijua hilo, ukaijua katiba basi taona ni wapi tunaelekea kwa mujibu wa katiba na si kwa mujibu wa tetesi au mtizamo wa Zitto, mimi, wewe au yule.
   
 12. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hatusingiziwi tunapoambiwa watanzania tu wavivu wa kusoma vitabu.
   
 13. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  niko kwa mobile otherwise ningekutwangia LIKE ya nguvu mkuu.
   
 14. S

  Saas JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimefurahi kwa uchambuzi wako makini pia naona itakuwa haina maana kama Kikwete ata dissolve Baraza la Mawaziri halafu akamuacha Pinda kwenye post ya Uwaziri Mkuu huyu naye anapaswa kuondolewa
   
Loading...