Bado miaka michache Uchaguzi Mkuu; Upinzani tunalolitaka ni madai ya Tume Huru ya Uchaguzi

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,942
3,819
Kama hamtaanza sasa hadi mnahakikisha Tume Huru Ya Uchaguzi imepatikana, msije mkahamasisha watu kuingi kwenye uchaguzi, fanyeni juhudi za wazi zionekane ziwaridhishe wapiga kura, sasa hata kama imebadilishwa au haikubadilishwa wananchi watawaelewa kuwa mlipigania kiume kudai Tume hio.

Haya mambo yao kwa sasa msiyape kipau mbele, hizi ni silaha za kampeni, yaani hayo mambo ya Mkaguzi na madudu anayoyaonyesha, msiyape kiki kabisa, kila yakiwa hivyo ndio kheri kwa upinzani kupata gudi target, wanarahisisha kazi na kila CCM wakiiba sana ndipo Serikali inapokosa hela ya kujiendesha, nasema hayo ni yao.

Huku tunahitaji mbinde za kudai Tume Huru Ya Uchaguzi mpaka Rais aliepo madarakani imfikie yakini ,kuwa ni kweli hili ni dai lisilo na shaka ndani yake.

Sio mnasubiri kesho uchaguzi ndio mnaaza lakini Tume sio huru voo, kazi ya kuhamamsisha Tume huru ni sasa ,msitoe nafasi kwa CCM kujikusanya mnawavuruga na wasielewane kabisa.

mambo ya Ndege meli hayo ni yao na weshavuruga sasa mkiwazindua watatafuta pakutokea. CCM ni wakukurupushwa mpaka wajutie kuwa viongozi, halfu wote inasemekana wana vimelea vya korona japo vipo dhaifu kwa sababu ya nyungu lakini nyungu weshaanza kuzitupa hawana muda.
 
Kuna yule mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mkurugenzi wake waliokuwa kichekesho na kejeli kwa taifa, huu ni wakati muafaka wa kuletwa mbele ya umma wajadiliwe na kuwajibishwa.
 
Acha uongo Mama Samia anahitajika sana kanda ya ziwa kuliko jana, nyie mnajaribu kupenyeza fitna ili aonekane anapigwa vita kanda ya ziwa Mama Samia kwa kanda ya ziwa ni dada yetu na shangazi yetu, amefanya kazi na Mjomba wetu na kaka yetu.

Mama Samia bado tuna jambo letu kwake, kwa miradi kibao ambayo inahitaji ufadhili wa serikali ya awamu ya sita.Chadema mna kesi kanda ya ziwa kwa kutubatiza SUKUMA GANG, kesi ile itahukumiwa 2025, mnatuona tumekaa kimya mkidhani tumefurahi na huo ubaguzi wenu.

2025 Mama Samia anazoa kura 95% bila jasho.Jana Mwenyekiti wenu kaongoe kwa upole huku akijua kabisa chama chake kimeingiza ubaguzi kwa kuwaita kanda ya ziwa SUKUMA GANG.Tusubiri muda utaongea
 
Acha uongo Mama Samia anahitajika sana kanda ya ziwa kuliko jana, nyie mnajaribu kupenyeza fitna ili aonekane anapigwa vita kanda ya ziwa Mama Samia kwa kanda ya ziwa ni dada yetu na shangazi yetu, amefanya kazi na Mjomba wetu na kaka yetu...
Kigogo ni kiongozi ndani ya CHADEMA?
 
Back
Top Bottom