Bado Kuna tatizo la "ulevi" wa madaraka/vyeo

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,113
7,688
Kuna kila dalili kuna baadhi ya viongozi/watendaji wa Serikali wanalewa madaraka mara baada ya kuteuliwa na wanasahau kabisa kuwa nafasi hiyo kateuliwa tu na wakati wowote anaweza kutenguliwa.

Baadhi yao wamekuwa wakidhani kuwa wao ni bora zaidi kuliko wengine walio achwa na hivyo kuanza kuinua mabega juu, Kumbe ubora wao unatokana na Utendaji wao.
Rais wetu leo kaongea maneno machache lkn yamejaa hekima na Busara ni vyema kwa watendaji wakayasikilizabkwa makini maelekezo aliyo yatoa.
chonde chonde kwa watendaji wote chapeni kazi, kazi yako, bidii na ubunifu wako ndio vitakavyo kutetea mbele ya jamii.
kazi iendelee asiye weza atupishe.
 
Mkuu kunywa beer za hela yote niliyokupa ukitaka kuongeza nishtue maana umegusa target, kibongo bongo watu wanajifanya Miungu kabisa
 
Bado kuna fikra kwamba ukipata nafasi ya uteuzi na vyombo vya habari vikakutangaza basi wewe ndo bora kuliko wote na dunia yote inakutambua. Hili swala limeharibu vijana na wanatumia nguvu nyingi kuvizia nafasi za uteuzi badala ya kufikiria kuanzisha miradi yao binafsi. Wanaofanikiwa kuteuliwa wanashtuka wakitenguliwa bila kupewa kazi mbadala.
 
Pongezi kwa wateule wote,
mara baada ya kiapo wanapaswa wachape kazi kwa speed na weledi.
Watanzania wengi tunapenda kuona Watendaji wanafuatilia miradi ya serikali kwa karibu.
hatupendi kuona viongozi wanakaa ofisini tu.
Mfano, Prof: Mbarawa ni mfuatiliaji mzuri ila sio mkali hivyo ili afanikiwe ni lazima awe mkali pale inapo bidi.
Makamba ni mfuatiliaji mzuri ila apunguze ushikaji kazini apige kazi, nishati ni nguzo ya uchumi wa Taifa.
Kijaji ni mpambanaji mzuri sana pia ni mkali hapendi masihara awapo kazini.
Mama Tax ni mweledi tunategemea maboresho mazuri zaidi.
 
Back
Top Bottom