Bado kuna mwenye Swali juu ya Unafiki mkubwa wa Watangazaji wa Vipindi vya Michezo Redio za Tanzania?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Juma Khatib ( Antonio Nugaz ) alipokuwa Yanga SC...

"Haji Manara hana uwezo na bado kabisa hajaweza kumfikia Antonio Nugaz kwa Kuhamasisha, Kushawishi na kupiga Madongo ya maana na huyu ndiyo kiboko yake"

Juma Khatib ( Antonio Nugaz ) baada ya kuondoka Yanga SC Jana...

"Haji Manara hana Mshindani hapa Tanzania kwani ana Karama ya Kipekee na hata Antonio Nugaz kuachwa Yanga SC hakuna pengo kwani alikuwa hata bado hajamfikia Manara na pia Nugaz hana Mvuto wa Kiushawishi"

Sasa naanza kuyaamini maneno aliyoyasema Rais Mstaafu Hayati Mkapa Kipindi chake kuwa Waandishi wa Habari ( Watangazaji wamo ) kuwa ni Wapumbavu na wanatakiwa Kujitathmini na Kubadilika upesi.
 
hakuna sehemu iliyojaa makanjanja kama kwenye vituo vya redio hasa habari za michezo na tv. Yaani wanataka tuamini upuuzi wao kama vile tuko madongo kuinama hatujui nini kinaendelea.
 
Nilishangaa baada ya Senzo kuteuliwa kuwa ceo wa muda wakaifanya habari kubwa utafikiri Senzo ndio mara ya kwanza kuja Tanzania kila redio watangazaji wanahangaika kusoma wasifu wake.
 
Juma Khatib ( Antonio Nugaz ) alipokuwa Yanga SC...

"Haji Manara hana uwezo na bado kabisa hajaweza kumfikia Antonio Nugaz kwa Kuhamasisha, Kushawishi na kupiga Madongo ya maana na huyu ndiyo kiboko yake"

Juma Khatib ( Antonio Nugaz ) baada ya kuondoka Yanga SC Jana...

"Haji Manara hana Mshindani hapa Tanzania kwani ana Karama ya Kipekee na hata Antonio Nugaz kuachwa Yanga SC hakuna pengo kwani alikuwa hata bado hajamfikia Manara na pia Nugaz hana Mvuto wa Kiushawishi"

Sasa naanza kuyaamini maneno aliyoyasema Rais Mstaafu Hayati Mkapa Kipindi chake kuwa Waandishi wa Habari ( Watangazaji wamo ) kuwa ni Wapumbavu na wanatakiwa Kujitathmini na Kubadilika upesi.
Michezo hawajui uchambuzi wala kutafuta habari, 98% ya habari ni football, timu ya wanawak ya taifa inacheza hata kutuambia hawasemi, hawatupi jibu wala hawahamasishi.
 
Back
Top Bottom