Bado kidogo kupata chenji ya noti ya elfu kumi ni hadi benki au super market.

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
19,146
2,000
Yaani leo nimepanda gari free kabisa baada ya kutoa noti ya 10,000 kulipa nauli konda akanirudishia hela yangu kwa kukosa chenji,yaani kwa sasa ukiwa na noti ya 10,000 kupata chenji ni kimbembe sana mzunguko uliopo ni kuanzia 5000 kushuka chini ,na ukiwa na laki moja kwenda juu my friend jitahidi usizihesabie mbele ya watu mazingira sio rafiki tena,ni hayo tuu nadhani mmenielewa.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
20,385
2,000
ndio ile thamani ya pesa mliyokuwa mnaililia inarudi kwa kasi ya ajabu.

sasa hivi mtu haogopi kukupa machenji chenji meengi hata ya elfu nane eti atakosa mengine waala.

hamsini nayo imerudi kwenye mzunguko ingawa bado inawekwa kama kishungi,haijamudu kusimama yenyewe bado.
 
Tuttyfruity

JF-Expert Member
Dec 3, 2017
2,419
2,000
True! Kua na elfu kumj ni mzigo kwa sasa yani. Konda atakutukana, utaenda dukani utakosa huduma kisa hawana chenji. Tafrani tupu kwa kweli
 
tempid

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
1,023
2,000
Yaani leo nimepanda gari free kabisa baada ya kutoa noti ya 10,000 kulipa nauli konda akanirudishia hela yangu kwa kukosa chenji,yaani kwa sasa ukiwa na noti ya 10,000 kupata chenji ni kimbembe sana mzunguko uliopo ni kuanzia 5000 kushuka chini ,na ukiwa na laki moja kwenda juu my friend jitahidi usizihesabie mbele ya watu mazingira sio rafiki tena,ni hayo tuu nadhani mmenielewa.
Uko wapi mkuu? Huku kwetu uswazi chenji hukosi kwasababu tunaziuza vituoni
 
google helper

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
8,434
2,000
Yaani leo nimepanda gari free kabisa baada ya kutoa noti ya 10,000 kulipa nauli konda akanirudishia hela yangu kwa kukosa chenji,yaani kwa sasa ukiwa na noti ya 10,000 kupata chenji ni kimbembe sana mzunguko uliopo ni kuanzia 5000 kushuka chini ,na ukiwa na laki moja kwenda juu my friend jitahidi usizihesabie mbele ya watu mazingira sio rafiki tena,ni hayo tuu nadhani mmenielewa.
Au petrol station
 
Michibo

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
1,818
2,000
Yamenikuta...!!
Hapa nimeshuka kwenye daladala na kurudishiwa msimbazi wangu, ila ni kama nimezingua kwa vile nimetoa noti nikiwa tayari nipo kituoni.... konda kauliza kama niko na japo mia mbili SINA kaamua isiwe tabu kasepa.
 
Lengutee

Member
Feb 16, 2011
29
95
Yaani leo nimepanda gari free kabisa baada ya kutoa noti ya 10,000 kulipa nauli konda akanirudishia hela yangu kwa kukosa chenji,yaani kwa sasa ukiwa na noti ya 10,000 kupata chenji ni kimbembe sana mzunguko uliopo ni kuanzia 5000 kushuka chini ,na ukiwa na laki moja kwenda juu my friend jitahidi usizihesabie mbele ya watu mazingira sio rafiki tena,ni hayo tuu nadhani mmenielewa.
Nchi gani mkuu hiyo
 
kiben10

JF-Expert Member
Apr 28, 2018
594
1,000
Daaah me niko Moro kwa week sasa na hii ndio imenipa kysafiri bure kwa 4times yaani navizia gari inataka kung'oa nanga tu najifanya nimestukia kituoni kuwa nimefika then natoa Msimbazi aisee Konda analalamika na kuuliza ndani kuna mwenye chinji ya buku 10 na hapo hapo anasonya then ananirudishia raha sanaaa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom