Bado Haijapoa: Ripori ya ajali meli MV Skagit yatolewa.. isome hapa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


na Mohammed Mhina, zanzibar


Tume ya Rais wa Wanzibar ya kuchunguza chanzo cha ajali ya meli ya skagit, leo imetoa ripoti yake kwa waandishi wa habari na kubainisha baadhi ya karoro na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua kwa wale wote waliohusikakatika ajali hiyo.


Akitoa taarifa ya tume kwa waandishi wa habari mjini zanzibar, katibu mkuu kiongozi wa smz bw. Abdullahamid yahaya mzee, amesema tume imebaini kuwa taarifa za idadi ya abiria waliopanda meli siku ya tukio ilikuwa ni potofu.


Amesema tume hiyo imebaini pamoja na mambo mengine, kuwa meli hiyo ilikua na idadi ya abiria 447 wakiwemo watanzania 429 na raia wa kigeni 18 tofauti na idadi iliyotolewa awali na uongozi wa meli hiyo kuwa ilikuwa na abiria 295 wakiwemo wafanyakazi kumi wa meli hiyo.


Aidha tume hiyo pia imebaini kuwa meli hiyo ilisajiliwa kinyume cha sheria na hivyo kupendekeza msajili wa meli hiyo bw. Seif juma, kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu.


Hata hivyo taarifa ya tume hiyo imetoautia na taarifa zilizokuwa zikitolewa na jeshi la polisi kuhusiana na idadi ya maiti zilizokuwa zikipatikana siku hadi siku.


Katika ripoti ya tume hiyo, imesema kuwa watu 81 walipoteza maisha tofauti na taarifa zilizokuwa zikitolewa na jeshi la polisi kuwa hadi kufikia tarehe 11/8/2011, idadi ya watu waliopoteza maisha ilikuwa ni 143.


Maiti za watu 222 zilipatikana katika maeneo mbalimbali ya mwambao mwa bahari kwa upande wa zanzibar na nyingine 21 zikapatikana mkoani tanga.


Tume hiyo iliyokuwa ikiongozwa na jaji wa mahakama kuu mh. Abdruhakim ameir issa, pia imetoa mapendekezo kuwa watu watano akiwemo mmiliki wa meli hiyo bw.said abdahamani juma na nahodha bw. Mussa makame mussa pamoja na meneja mkuu wa kampuni ya sea gall inayomiliki meli ya skagit bw. Omari mnkonje washitakiwe mahakamani.


Wengine wanaotakiwa kushitakiwa ni nahodha wa meli hiyo bw. Makame mussa na mhandisi wa zamu wa meli hiyo.


Meli ya mv skagit ilizama tarehe 17/7/2012 katika baharini karibu na kisiwa kidogo cha chumbe na kusababisha vifo na manusura wa abiria waliopanda katika meli hiyo.
 
UFISADI na ULAFi utawamaliza WANANCHI WANYONGE... MATAJIRI wanatajirika hata kama Wananunua Vyombo Vilivyoisha Kazi kwa kufanya kazi kwa MUDA MREFU Kabla ya kununuliwa...

Haki na Usawa - Haipo Tena... WENGI Wanaikumbuka Mv. MAPINDUZI kilifanya kazi MIAKA nenda rudi HAIKUWAHI kusababisha MAAFA...
 
Ninaamini tume imefanya kazi vizuri na ni wakati wa mamlaka husika nazo kutekeleza mapendekezo ya tume, angalau adhabu kali zikichuliwa kwa wazembe waliosababisha vifo vya WATANZANIA wenzetu itakuwa fundisho kwa wazembe wengine.
 
Asante kwa kujuza! Hii tume imekopi na kupesti (copy & paste) almost taarifa yote hii, kabla ya tume kuundwa taarifa hizi zishawekwa wazi na vyombo vya habari hapa nchi na nje ya nchi, sioni kipya kwenye taarifa hii ya tume.
 
Asante kwa kujuza! Hii tume imekopi na kupesti (copy & paste) almost taarifa yote hii, kabla ya tume kuundwa taarifa hizi zishawekwa wazi na vyombo vya habari hapa nchi na nje ya nchi, sioni kipya kwenye taarifa hii ya tume.
Kwani ulitaka vp?nyie ndio wale wakifundishwa na mwalimu asiyeeleweka mnasema ' ticha kiboko test yake ukipata 30% we kichwa'
 
Back
Top Bottom