Bado Dunia ina watu wema sana

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Bado dunia ina watu wema hata kama ni wachache. Jana nilielezea kisa cha Jaji mmoja ambaye alidai mwenye bahati kushikana mkono na mimi. Ni kauli kubwa sana kuambiwa toka nizaliwe. Hadi nikatamani nijipitishe pale "Central" wanikamate kwa uchochezi halafu kesi apelekewe yule Jaji 🤣

Siku moja nilipewa taarifa za mtoto Pili aliyezaliwa kichwa kikubwa, mgongo wazi na sehemu ya utumbo wake ikiwa nje. Ikanigusa sana hasa baada ya kuambiwa baba yake ni marehemu, mama ni mgonjwa na bibi anayewalea ni mlemavu. Nikalazimika kusafiri hadi Arusha kuwaona.

Nikakaa Arusha siku 5. Asubuhi moja nikiwa kwenye hoteli niliyofikia akaja meneja akaniuliza kama ni Malisa. Nikamjibu ndio. Akafurahi sana. Akaniuliza gharama za kusafiri hadi huku nani anakulipia? Nikamwambia nalipa mwenyewe. Akastaajabu kidogo kisha akaniambia "kaka una moyo wa ajabu sana. Naomba nilipie gharama zako hapa hotelini." Akapewa bill akalipa.

December nikiwa natoka Mwanza, ndugu yangu akanipigia akasema "nina rafiki yangu anamiliki hoteli Morogoro ni mfuasi wako mitandaoni. Ameomba kama utaweza kufika Moro ulale kwenye hoteli yake angalau akusalimie." Nikiwa na rafiki zangu watatu tukafika na kulala kwa gharama za mmiliki.

Siku moja nikiwa Dodoma nilijaza mafuta kwenye kituo fulani, meneja wa hicho kituo akaniruhusu niende bila kulipa chochote. "Kaka nenda tu, nitaclear. Unafanya kazi kubwa sana kwenye jamii"

Siku moja nikiwa ofisini nikapigiwa simu na rafiki yangu mmoja. "Kaka unaweza kupata nafasi ukaja ofisini kwangu leo?" Nikamwambia "nipo tight kidogo kaka naomba nije saa 11 nikitoka ofisini" akajibu "sawa kaka hamna shida, nitakuwepo hadi saa 2 usiku"

Tulipokutana akasema "Unafanya kazi kubwa sana ya jamii. Najua unatumia muda wako na wakati mwingine fedha zako kuwafikia wahitaji. Wengi hatujali sana unapoteza mangapi, tunachojali ni kuona wahitaji wanasaidika. Mimi na Mkurugenzi mwenzangu tumeona tuchangie angalau mafuta lita mbili unapokua katika safari zako za kusaidia wahitaji" Akanipa hundi ya $1,000.

Hakika watu wema bado wapo. Nawashukuru wote mlioniunga mkono kurudisha tabasamu kwa watanzania wenzetu mwaka 2020. Tuzidi kushirikiana mwaka 2021. Mungu awabariki sana.

Baba Nicole AKA Malisa GJ
 
Mmmh haya bhana
 
Kila wema anaotenda Mungu anamlipa kwa njia nyingine na anamkutanisha na watu wema
 
Hapana Mkuu mimi si Malisa ila huyu jamaa ananigusa sana moyoni kwa juhudi zake kubwa sana za kuwasaidia Watanzania mbali mbali wenye matatizo ya kila aina ili kuwarudishia tabasamu zao na bahati nzuri Watanzania wamemkubali sana katika juhudi zake hizo na hivyo wanajitoa sana na wengi ni Watanzania wa kipato cha kawaida tu.
Mkuu BAK,ww ndio malisa au umepost ujumbe wa malisa??,by the way malisa nimesoma nae chuo kikuu yupo peace sana.
 
Mbona umeguna Mkuu?
Huyo malisa sijui ndi wewe, anapewa pewa offer ambazo anatakiwa afikirie mara mbili zaidi maana yaweza kua lengo si zuri la hao watoao offer hizo au yawezakua anatumika kwa namna moja ama ingine.
 
Wakati mwingine inabidi tu tuwaamini binadamu wenzetu wanapotenda wema wa aina yoyote ile. Hatumiki na yeyote yule zaidi ya kuwa na roho nzuri sana ya kuwasaidia wenye matatizo ambao hawajui bali tu ni kwa kuwa ni Watanzania wenzie.
Huyo malisa sijui ndi wewe, anapewa pewa offer ambazo anatakiwa afikirie mara mbili zaidi maana yaweza kua lengo si zuri la hao watoao offer hizo au yawezakua anatumika kwa namna moja ama ingine.
 
Huyo malisa sijui ndi wewe, anapewa pewa offer ambazo anatakiwa afikirie mara mbili zaidi maana yaweza kua lengo si zuri la hao watoao offer hizo au yawezakua anatumika kwa namna moja ama ingine.
Malizia andishi lako.
 
Wapo tu wema japo wachache na hawafahamiki. Nilimrudishaga jamaa flani wallet yake kwa kumkimbiza nyuma aliisahau kwenye kiti cha treni na alikuwa anatembea kwa haraka na mimi namkimbiza na kwenye wallet kulikuwa na hela nyingi pamoja na kadi na vitambulisho. Alishtuka na kushangaa nilipompa. Akanishukuru nami nikaondoka zangu faster kwasababu nilikatiza safari yangu ya kwenda 'kubeba boksi'.

Sasa cha ajabu baada ya tukio miezi kadhaa nami nimeshakimbizwa mara tatu kurudishiwa simu na wallet nilizosahau kitini kwenye bus na treni
 
Kama ni Copenhagen sawa, ila Jon Stephano nina mashaka
 
Kwa hiyo anajitangaza ili watu waendelee kumpa vya bure siyo?
Hajakulazimisha usome alichopost..Wala hajakuomba chochote.
Tatu rejea kusoma heading ya bandiko na alichopost ndani yake,alitaka tu kuonyesha kwamba kuna watu huwajui lkn huko waliko wanathamini kile unachokifanya ktk jamii.Jaribu kufikiri ktk mtazamo chanya utapata amani ya moyo.hutateseka.
 
Back
Top Bottom