Badilisha matumizi ya nyumba yako kubwa, kuwa ya kibiashara; hasa kwa wale walioajiriwa

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,270
40,080
Kumekuwa na mahitaji au matamanio ya kila mtu anayepata kipato kutamani kumiliki na kuishi kwenye nyumba kubwa.

Wapo wanaodunduliza au kupata mikopo, na hatimaye kufanikisha lengo hilo.

Na kuishi kwenye nyumba kubwa, huku umeajiriwa, kiuchumi sio ufahari ; kwa sababu inakuwa haikuingizii kipato, zaidi ya kukupa gharama.

Na inapotokea pale umeachishwa kazi, ndipo majengo hayo yanaanza kuchoka; bustani inakufa, vibarua vya ulinzi na usafi vinakufa n.k

Ushauri wa kibiashara na kuongeza kipato: Kwa nini usiigeuze hiyo nyumba yako kubwa, kuwa 'lodge' na kuanza kuingiza kipato? Ili ata pale utakapoachishwa kazi, uwe tayari una-uwezo wa kujisimamia?

NB: Kuajiriwa ni utumwa, na huna hatimiliki na hiyo ajira.
 
Aisee hii kauli ya kuajiriwa ni utumwa mbona haina ukwwli....ebu muulize lionel messi kama kuajiriwa ni utumwa
 
Haijaishi utalipwa kiasi gani; lazima unyenyekee au uwe mnafiki ili uendelee kuwa na ajira
 
Unafiki wapi wewe ujue nondo zako hazijakaa sawa...ona watu kam wakina ancelotti wanafurahia kazi zao mpaka anamchukua mtoto wake kama asistant na maboss wanakubali.
Kaa nyumbani wiki nzima usiende kazini, uone matokeo yake.
 
Hata ukijiajiri lazima unyeyekee wateja wakoo..

Huoni wakandarasi wanavyotukanwa hadharani na watu wa serikali sababu ni wateja wao.

Mteja ni ananyenyekewa popote
Usipo-onekana JF, watapata hasara?
 
Kaa nyumbani wiki nzima usiende kazini, uone matokeo yake.
Sasa wee mbona ata mfanya biashara asipoenda kwenye biashara zake naye atavuna mabua.

Kama kazi yako waipenda na unalipwa vizuri mbona u aenjoy tuu. Sema ili kufika kwenye hiyo stage ya kulipwa vizuri mpaka ufurahie kazi yako....utasoma vitabu mpaka hanjam mbichi inatoka.
 
Katika dunia hii, wapo waliozaliwa kwa ajili ya kuajiriwa tu na si kutengeneza ajira kwa wengine.
 
Sasa mumbe walitambua hilo. So tuache ujinga wakusema kuwa ajira ni utumwa. Tunahitaji wote waajiriwa na wale wamiliki business ndio mambo yanaenda
 
Kumekuwa na mahitaji au matamanio ya kila mtu anayepata kipato kutamani kumiliki na kuishi kwenye nyumba kubwa.

Wapo wanaodunduliza au kupata mikopo, na hatimaye kufanikisha lengo hilo.

Na kuishi kwenye nyumba kubwa, huku umeajiriwa, kiuchumi sio ufahari ; kwa sababu inakuwa haikuingizii kipato, zaidi ya kukupa gharama.

Na inapotokea pale umeachishwa kazi, ndipo majengo hayo yanaanza kuchoka; bustani inakufa, vibarua vya ulinzi na usafi vinakufa n.k

Ushauri wa kibiashara na kuongeza kipato: Kwa nini usiigeuze hiyo nyumba yako kubwa, kuwa 'lodge' na kuanza kuingiza kipato? Ili ata pale utakapoachishwa kazi, uwe tayari una-uwezo wa kujisimamia?

NB: Kuajiriwa ni utumwa, na huna hatimiliki na hiyo ajira.
Kugeuza nyumba yako kuwa lodge kinadharia ni rahisi, ila kiuhalisia sio rahisi hasa kutokana na design za nyumba zetu zilivyo na masharti ya lodge yalivyo
 
Back
Top Bottom