Badili maisha yako leo: Yajue Mawe Saba na Madini saba tu yanayoweza kukubadilishia au kukuletea unachotaka

Hii moonstone nasikia ina nguvu sana hasa kwenye kutoa au kufuta laana. Sijui kama kweli
 
Wewe umebadilisha maisha yako kiasi gani? Hupendi kuwa rais wa nchi hii?hupend kuwa billionea?kwa nini hukupenda kumpata mo haraka kipindi kile?

The devil is very tricky. Unaona ukitaja jiwe la yesu utawapata na wakristu?yesu hana jiwe lake smewhre.huo ni ushirikina na kutaka kuwateka watu kwenye giza.jiwe la muhamad linapatikana wapi?hapo unawapata waislamu.

Rakims unachofanya ni 1. Utapeli 2. Ushirikina.

Si mbaya ukiendelea utapata chochote kitu.maana humu mbumbumbu hawakosekan.wapige maana wajinga ndio waliwao.

Anasahau kwamba Copper ni Shaba kwa kiswahili etc
 
*Ulishawahi kujiuliza ni lini na wewe utakuwa mtu mbele ya watu?

*Rafiki mbele ya marafiki?

*Mwenye pesa mbele ya wenye pesa?

*Msemaji mbele ya wasemaji?

*Mfano mbele ya mifano?

*Tajiri mbele ya matajiri?

*Mwenye kutoa huduma mbele ya wahudumiaji?

* Mwenye kuoa mbele ya wenye ndoa?

*Mwenye kuibuka mbele ya walioibuka?

*Mwenye kutamanika mbele ya wenye kutamanika?

*Mwenye kazi mbele ya wenye kazi?

*Mwenye kukubalika mbele ya wenye kukubalika?

*Mwenye Miujiza mbele ya wenye Miujiza?

Just stop asking yourself and act today,

Ninachoenda kufundisha hapa kwenye hii thread basi itamnufaisha kila mmoja na kila mtu kwa level zote za maisha na akapata anachotamani bila kufanya dhulma ya nafsi au roho yake mwenye na kujikita katika ushetani,au mambo yasiyopendeza mbele ya Mwenyezi mungu na jamii nzima,


Kwa kuanza wakuu nitawakumbusha au kuwarudisha nyuma kwamba kabla ya kuumbwa mwanadamu na vyote vilivyopo ilianza kauli ya Mwenyezi mungu ambayo waislamu tunaitambua kama "Kun faya kun" kuwa na jambo likawa kauli yake Allah (S.W)

Lakini pia kwa jamaa zetu wa karibu ambao tunaishi nao kwa wema wakristo nao pia wanaamini kuwa hapo mwanzo kulikuwa (Neno) neno kwa maana ya kawaida ni kauli inayotamkwa,

Dunia hii inaaminika kuwa iliubwa kwa Mawe au kauli za Mwenyezi mungu au kwa wasioamini uwepo wa roho pia wao husema kuwa Dunia ni mkusanyingi wa elements mbalimbali ambazo zilijichanganya na kufanya Creation ya viumbe,

Nachochukua kutoa hapo sehemu zote 3 mean kwamba (Islam/Christian & pagan)
Ni elements

Elements zipo katika sehemu 4 ambazo ni:

*moto
*upepo
* Maji
*udongo

Sisi tunaoamini katika dini na Mwenyezi mungu tunaongeza moja Ambayo ni

*roho

Hivyo inakuwa

*moto
*upepo
*Maji
*Udongo
*roho

Hivyo kwa mpangilio huo tu tunaonakwamba

Huwezi kupata udongo bila roho? Sawa sawa?
Huwezi kupata Maji bila udongo!

Huwezi kupata upepo bila maji!

Na huwezi kupata chochote kile bila Chanzo!

Hata kazi huwezi kupata bila elimu,

Naimani tupo pamoja hadi hapo,

Sasa sisi teyari ni roho za Muumba wetu na pia ili tuweze kufika popote pale tunapotaka kwenda lazima tufuate vema safari tunayoenda bila kukosea hatua moja, ili mwisho wa siku tuweze kurudi kuwa roho bila kukosea na kutokukwamia kwenye moto(maybe hell will help you to understand)

Ur source is Spirit and your end is Spirit if your end is in fire that's your choice,

Kwamba:
"Chanzo chako ni roho na mwisho wako ni roho kama utaishia Motoni hayo ni machaguo yako"

Hivyo sote tunakubali kwamba mwenyezi mungu ni wa mwanzo na wa mwisho,

Islam "Allahu Al Awwal wa Al Akhir"

Christian "Alpha na Omega"

Mimi huwa naamini jambo moja kwamba Mwenyezi mungu vyovyote vile unavyomjua wewe hakuleta mtu duniani kuja kuteseka bali kuishi na kumuabudu na kisha kwenda zake kurudi alipotoka..

Nikiendelea kuzungumzia kwa upana thread itachosha wacha nifupishe kwa kuwasaidia wanyonge wa kusoma

Katika hii dunia kuna mawe saba tu na madini saba tu ambayo mtu anatakiwa ayatumie pale ambapo anakuwa na tatizo linalomshinda kutatua ikiwa atataka roho yake itulie bila kuwa na bugudha ya kukosa utulivu au bila kufanya jambo kwa mafanikio, sio kila anayeishi anajua vitu vyote na kazi yake hivyo kuongozana na kukumbusha au kuhabarisha ni heri kwa kila mtu,

Aina saba za madini ni:

1: Lead/Risasi

2: tin/Bati

3: iron/ chuma

4: Gold/dhahabu

5: Copper/ kopa

6: brass/ shaba

7: silver / Fedha

Aina saba za mawe ni:

1: Jet
2: Amethyst
3: Bloodstone (jiwe la Yesu)
4: Amber ya njano
5: Jade
6: Carnelian(Aqiq) jiwe la mtume
7: Moonstone

Wakuu hayo ndio madini na mawe makuu yenye maana pana na kubwa sana na historia iliyo nzuri na kipekee na panapomajaliwa taanza kuelezea moja moja kwa mapana na marefu

Wadogo na wakubwa zangu mnaolimbukia kuvaa stones na metals ambazo hamjui maana zake na utumikaji wake nawapa pole mwisho wake ni kuangamia na kujikuta kwenye wakati mgumu usioweza kusaidika, pia unakuta mtu anavaa pete mkono usiofaa na madini yasiyofaa na jinsi isiyofaa ndugu yangu hatutashangaa tukiskia umejiua au umefanya jambo la kutikisa dunia, unakuta mtu anavaa pete

*kidole cha gumba bila kujua maana yake, hivyo ni kuwish kufa kwa kujiua au udhalili

*pia kuvaa pete kidole cha shahada ni kukaribisha tabia za Sodom & Gomorrah katika roho yako na utafanya kwa sababu wao walikuwa wakifanya hivyo baada ya kuingiliwa,

*pia unakuta mtu anavaa pete kidole cha kati bila kujua maana yake

*mwingine huvaa kidogo bila kujua maana yake,

Jiepusheni na mambo msiyoyajua


Pia pole kwa wavaa dhahabu na fedha bila kujua mwisho wake ni hovyo tu, heri kuachana navyo tu,

Itaendelea,!!

Hadi hapo kwanza mwenye swali Aulize

Rakims
Mkuu huwa nakubali sana news (nyuzi) zako pamoja sana kwa madini haya adim

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Somo zuri sana, endelea kushusha nondo Mkuu. Sikuizi wa vaa mapete wamekua wengi kweli unakuta mtu anapete nne za rangi tofauti na wengi hawajui maana yake ikiwemo mie. Nazani kwa elim hii tutakua tumejifunza kitu
Mkuu hizo unazozani ni pete ni kweli unaziona ni pete ila umebebea majini na hayo ndiyo yanakufanikioshia mambo yako.Unachotakiwa kujua hata shetani anauwezo wa kuwafanya watu wawe maarufu na wawe na pesa na nguvu katika jamii.Mtegemee Mungu wa Isarel na utakuwa salama.Huyu jamaa hajaanza leo kuwafundisha watu ushirikina akijificha kwenye vitabu vya dini na majina ya mitume na manabii,hapa mnaelekezwa uchawi wazi wazi,si kwamba hamtafanikiwa mtafanikiwa ila mtajuta baadaye.
Mpokee Yesu akae moyoni mwako ili ufanikiwe katika mpango wa Mungu hauhitaji pete ila katika mpango wa shetani pete unazihitaji.Be Watchful.
 
Back
Top Bottom