Mdanganywa
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 620
- 342
Najua suala la pension limetaimiwa vizuri na watu. Si kwamba lina hoja ya kutisha hadi nchi nzima ikatetemeka, bali waliolikuza walicheza na uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya Social Security.
Inaeleweka kwamba watanzania wengi ni wagumu kusoma vitabu. Ni wengi kiasi cha kutisha.
Hivyo, unapoleta hoja ambayo wana uelewa kiduchu basi hicho kiduchu kitapigiwa kelele kupita kiasi. Na kama mleta hoja hukupima matokeo ya unacholeta basi kelele hizo zitakufundisha adabu na ukicheza unaweza kubwaga manyanga.
Ndicho kilichotokea kwenye suala hili la SSRA ambalo thread humu zimepungua.
Hoja ya wengi humu ilikuwa je, iweje mtu afukuzwe kazi akiwa na miaka 35 halafu asubiri miaka 20 ndipo apate hela yake ya Pension.
Anayeuliza swali hili ukweli ni swali ambalo ni rahisi kujibu katika mazingira fulani lakini yapo mazingira utatumia nguvu nyingi kueleweka.
Hivi kweli kwenye conference ya wasomi wa Social Security, hili swali lina ugumu gani? Pale IFM kuna watu wanachukua degree ya Social Security. Swali hili ni rahisi kabisa kujibu pale.
Lakini tabu ni kuliuliza swali hili kwenye public. Hakika utakuwa unaleta fujo maana hapo humjibu profesa anayeshisha Social Security exam bali unawajibu watanzania ambao wamekariri kwamba ukifukuzwa kazi unachukua pension yako. Hakika hapo ukumbuke kwamba ukilijibu kama unavyomjibu yule profesa basi kuna hatari hata ya chama chako kuondoka madarakani kwenye uchaguzi ujao iwe CHADEMA au CCM.
Tuje sasa kwenye topic ya leo. Pamoja na yote hayo, kilichoonekana ni kwamba kumbe pressure ya watu inaweza kufanya serikali ikabadili jambo liwe watu wanavyotaka. Sina matatizo na hili.
Lakini jambo kubwa kwangu ni kwamba kwa nini tusiutumie mwanya huu ili Tanzania iwe na UNEMPLOYMENT BENEFIT. Maana ile hoja kwamba mtu akifukuzwa akiwa na miaka 35 isingekuwa na nguvu kama kuna UNEMPLOYMENT BENEFIT scheme. UNEMPLOYMENT BENEFIT ni kiasi unacholipwa kukidhi maisha yako kama hukuajiriwa.
UNEMPLOYMENT BENEFIT ikiwepo basi hapo ndipo kweli tunakuwa tunaingia kwenye Social Security haswa. Kwa hiyo najua thread hii inaweza kuleta majibu ya kila aina lakini tutakuwa tumefaidika na wale watakaotufafanulia kuhusu uwezekano wa kufikia hatua ya kupata UNEMPLOYMENT BENEFITS.
Hela inayoibiwa na kufichwa huko nje ingefaa kabisa kuboresha schemes kama hizi na kusingekuwa na kelele kama tulizoona baada ya SSRA kutangaza utaratibu wao kwa mujibu wa sheria.