Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,349
- 6,476
Tabia mbaya ya wengi wa madereva Bongo, hasa Dar es Salaam ni kutokuruhusu madereva wengine kuingia barabara kuu ingawaje sheria inawapa wao maamuzi hayo. Lakini, kuna wakati mwingine nao utaka kuingia njia kuu.
Yawezekana hawa ndio wanaolazimisha. Na inawezekana wanabania wengine kulipiza kisasi, lakini je, unayembania ndiye aliyekubania mwanzo?
Sasa nikikuruhusu, kama ambavyo mara nyingi ufanya, badala ya kuhaha na mi-hazard lights yako kushukuru, tafadhari kamfanyie na mwingine.
Wengi wakiwa mbele yangu baada ya kuwaachia njia, hawaruhusu wengine. Halafu, mkiruhusiwa, basi muingie walau watano kama mpo zaidi ya watano, badala ya kutaka kuingia wote.
Jamani, tuwe wastaarabu!