Badala ya kuanzisha somo la Historia ya Tanzania, tuwekeze nguvu kwenye haya ili vijana wajikwamue kiuchumi

PAND PIERI

Senior Member
Jul 30, 2020
183
270
Kwa hali ilivyo sasa hivi hilo somo litamsaidiaje mwanafunzi kujikwamua kiuchumi baada ya kumalizia masomo yake? Kuna historia gani mpaka ifundishwe kwa miaka kumi na tatu tena kwa Kiswahili? Kwani masomo ya uraia na historia ya sasa hivi hayasaidii mwanafunzi kuijua Tanzania ipasavyo?

Ni muda mwafaka badala ya kuwekeza nguvu kwenye Somo la Historia ya Tanzania kwa Kiswahili tuwekeze nguvu kwenye masomo yanayohusu

1. Teknologia
2. Ujasiriamali
3. Kilimo na mifugo
4. Computer
5. Ufundi
6. Kuendeleza vipaji

Ili tuondoe changamoto ya ukosefu wa ajira na vijana wajikuamuwe kiuchumi.
 
Nafikiri wangeboresha somo la stadi za kazi lisomwe kwa wote, liwe na DIY za kuandaa vitu tofauti.....na kila mwanafunzi wa for 1 anapewa task akimaliza form 4 anatakiwa alipresent mbele ya wasimamizo wa necta apewe na marks same to form 5 and form 6 students hii ingesaidia sana.

Au hata hiyo physics baadhi ya vitu ibadilishwe watoto wasome vitu realistic zaidi utengenezaji wa simu, computer, kurepair na the likes
 
nafikiri wangeboresha somo la stadi za kazi lisomwe kwa wote, liwe na DIY za kuandaa vitu tofauti.....na kila mwanafunzi wa for 1 anapewa task akimaliza form 4 anatakiwa alipresent mbele ya wasimamizo wa necta apewe na marks same to form 5 and form 6 students hii ingesaidia sana.......

au hata hiyo physics baadhi ya vitu ibadilishwe watoto wasome vitu realistic zaidi utengenezaji wa simu, computer, kurepair na the likes
Sijui hiyo historia ya Tanzania kuanzia darasa la kwanza hadi kidato Cha sita kwa Kiswahili ndio utamweka mwanafunzi kuwa Mzalendo wa kutii chochote hata Kama ananyimwa haki yake ?
 
Uamuzi huu wa Kiswahili ni mujarabu. Kongole & hongera kwa Team JPM kwa kazi nzuri ya kizalendo. Kamwe msisikilize kelele zao
 
Wajapani na wakorea wanakazia somo la hesabu.
Mtu akijua hesabu utapata
Engineer
Msanifu
Daktari
Mwalimu
Mtehama na kadhalikaa
Hebu niambie mtu akijua uraia
Atatawalika kirahisi!
Historia yenyewe haitotambua mchango wa familia za kina Marealle, Mbowe, Sykes, Okello, Rupia, Kahama, katika uhuru wa nchi!

Everyday is Saturday...............................:cool:
 
Eti vijana wawe wazalendo. Nawaambia hivi mtu mwenye njaa ni ngumu sana kuwa mzalendo. Boresha uchumi wa watu na uzalendo utajijenga.
Aiseee! Tangu hii njaa muiimbie nyimbo za mapambio from many years back, ingekuwa imewalamba raia wote milioni ngapi huko, if maneno yenu yangekuwa kweli kwamba raia wana njaa. Lakini, kinyume chake, tunawaona Watanzania wakizidi kuzaliana tuuu. Nguvu wameipata wapi kama siyo kwenye chakula!??? Na chakula kimetoka wapi kama nchi ina njaa!??? Simply, ^njaa^ hapa ni hoja zuku tu (invented argument), baada ya msisimko bandia wa Korona kukosa ladha waliyokuwa wakiisaka.
 
yaani watu wa mataifa mengine wako keen na mauvumbuzi,nyie mnakalia historia??!!!..tena ingekua hiari bora eti lazima!, akili zenu zimeshndwa kuwa creative kuja na mbinu za kuboresha elimu yetu?
 
Aiseee! Tangu hii njaa muiimbie nyimbo za mapambio from many years back, ingekuwa imewalamba raia wote milioni ngapi huko, if maneno yenu yangekuwa kweli kwamba raia wana njaa. Lakini, kinyume chake, tunawaona Watanzania wakizidi kuzaliana tuuu. Nguvu wameipata wapi kama siyo kwenye chakula!??? Na chakula kimetoka wapi kama nchi ina njaa!??? Simply, ^njaa^ hapa ni hoja zuku tu (invented argument), baada ya msisimko bandia wa Korona kukosa ladha waliyokuwa wakiisaka.
Huyu paraumu nae yupo yupo,endelea kushabikia undwecha wako .
 
Aiseee! Tangu hii njaa muiimbie nyimbo za mapambio from many years back, ingekuwa imewalamba raia wote milioni ngapi huko, if maneno yenu yangekuwa kweli kwamba raia wana njaa. Lakini, kinyume chake, tunawaona Watanzania wakizidi kuzaliana tuuu. Nguvu wameipata wapi kama siyo kwenye chakula!??? Na chakula kimetoka wapi kama nchi ina njaa!??? Simply, ^njaa^ hapa ni hoja zuku tu (invented argument), baada ya msisimko bandia wa Korona kukosa ladha waliyokuwa wakiisaka.
Hoja yangu imekuzidi uwezo wako wa uelewa. Mtu anae ishi nyumba ya tope hata kama anakula ana njaa huyo. Mtu ambae hana ajira na anakula kwa wazazi au ndugu ana njaa huyo. Malazi bora , makazi bora na chakula bora kimojawapo kikikosekana maana yake una njaa. Panua fikra, kuishinda njaa ni zaidi ya kula ugali.
 
Eti vijana wawe wazalendo. Nawaambia hivi mtu mwenye njaa ni ngumu sana kuwa mzalendo. Boresha uchumi wa watu na uzalendo utajijenga.
Hapa ndipo hoja ya msingi ilipo. Haya mambo ya kulazimishana uzalendo, huku wewe mwenyewe ukiwa si mzalendo! Ni kuchoshana tu.

Serikali iboreshe maisha ya watu kupitia mipango na mikakati mbalimbali inayo tekelezeka. Baada ya hapo kila Mtanzania atakuwa Mzalendo kwa Nchi yake. Kinyume na hapo, natarajia tu kuona Rais mwingine akiingia madarakani akija na yeye na la kwake.

Tuirudishe kwenye Mchakato Katiba ya Wananchi, ili haya mambo yote yakawekwe huko! Badala ya kuwa kila anachotamka Rais kugeuzwa kuwa Sheria. Tanzania kwa sasa inahitaji uwepo wa mifumo imara na siyo mtu imara.

Bado namkumbuka sana namna tamko lake la kuhusu Simba na Yanga lilivyo vuruga mchakato wa uitwaji wa wachezaji walioshiriki CHAN mwaka huu wa 2021 kule Cameroun.
 
Hoja yangu imekuzidi uwezo wako wa uelewa. Mtu anae ishi nyumba ya tope hata kama anakula ana njaa huyo. Mtu ambae hana ajira na anakula kwa wazazi au ndugu ana njaa huyo. Malazi bora , makazi bora na chakula bora kimojawapo kikikosekana maana yake una njaa. Panua fikra, kuishinda njaa ni zaidi ya kula ugali.
^Kuishinda njaa ni zaidi ya kula ugali^ --- kuna familia zinakula viazi, makande, wali and the like; ugali wako hawagusi. Hao tuwaweke kwenye kundi gani, wewe tandabelua wa Indian Ocean!???
 
Back
Top Bottom