BAD NEWS: Coastal V Yanga kugeuka mechi ya kirafiki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAD NEWS: Coastal V Yanga kugeuka mechi ya kirafiki?

Discussion in 'Sports' started by Mlitika, Apr 1, 2012.

 1. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mabingwa watetezi wa kabumbu nchini Dar Y.A. leo/jana (samahani, sina hakika na saa yangu) walikuwa wageni wa Coastal Union huko ugosini ambapo muda wa mchezo uliisha kwa mabingwa hao watetezi kuwa mbele kwa bao moja. Katika mechi hiyo mabingwa hao watetezi walimchezesha Stephano Mwasika ambaye kwa kadiri ya sheria za kabumbu alikuwa bado anatumikia kifungo halali cha Kadi nyekundu kwa kosa la kumchapa makonde mwamuzi. Baada ya rapsha za mechi hiyo Kamati ya Mashindano ya TFF ilitembeza kibano kwa wachezaji watano wa Yanga ambapo bondia Mwasika pamoja na kifungo cha kawaida cha kadi nyekundu cha kuwa benchi kwa mechi zisizopungua tatu alilimwa ban ya kuwa nje ya ligi kwa MWAKA MMOJA.

  Katika hali inayo-apply tu katika busara za soka la
  Kibongo Kamati ya Nidhamu ya TFF chini ya njagu mstaafu Tiba iliamua kuondoa vibano vya wanasoka hao. Yanga kwa ulevi wa ushindi wa kesi wakaamua kumchezesha Mwasika leo (jana) wakijisahaulisha kuwa ishu yake ilikuwa na adhabu mbili toka Mamlaka mbili tofauti

  1. Kadi nyekundu which is indubitable kwa maana kwamba ktk sheria za kabumbu hakuna awezaye kutangua maamuzi ya refa halafu matokeo ya mechi yabaki halali. Mamlaka yoyote itakayotangua maamuzi ya refa hata katika tukio moja la mchezo basi maamuzi yoye ya refa kisheria yanapashwa kuwa batili na kwa sababu hiyo mechi inapashwa kurudiwa.
  2. Kamati ya Mashindano ya TFF ilimpa Mwasika mezani hiyo ban ya mwaka 1 kama adabu ya pili (ambayo haifuti ile ya kwanza).

  Ili iwe halali kwa adhabu ya kwanza hapo juu kufutwa na kamati ya Tiba ni lazima sentenso zifuatazo ziwe mantiki sahihi:
  · Maamuzi ya refa siyo ya mwisho / maamuzi mbadala yanaweza kutolewa na mtu kama Tiba ambaye siyo lazima awe uwanjani wakati mechi inachezwa.
  · Mwasika alikuwa sahihi kumpiga refa/ Mwasika kumpiga refa ilikuwa halali ndiyo maana kadi nyekundu aliyopewa siyo halali.

  Kama tukifuata tu sheri za FIFA ili kujenga heshima yetu na kukuza nidhamu ya wachezaji wetu ambayo ni mbovu na ndiyo inayodidimiza soka letu, Yanga wana sababu ipi ya kutonyang'wanywa pointi tatu za mechi hii?


  SOSI NI MIMI NA SHERIA ZA SOKA!
   
 2. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kibongo bongo kila kitu Kulindana! Walijisahau kama walivyojisahau Tipimazembe kumchezeza yule mchezaji na simba wakanyang'anywa ushindi!
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  Soka la bongo ni sawa na biashara ya ndumu, haina regyulesheni
   
 4. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo siasa tu imeingia kila mahali katika taifa letu .Tusali tu tuombe MUNGU nchi iwe kama za wenzetu kwani adhabu hiyo angepewa mchezaji wa timu zingine kama Ruvu JKT isingefutwa milele.
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  marafiki wa simba mna taabu sana,tatizo wengi mmeingia kwenye soka kwa kukurupuka bila kujifunza kwanza sheria za mchezo mnaoupenda(soka). Ngoja nitoe darasa kidogo kwa faida yako na mbumbumbu wengine wa sheria mpya za soka.

  Iko hivi,mchezaji akipewa straight red card ni kweli anakosa mechi tatu,ila immediately anaanza kutumikia adhabu hiyo ya mechi tatu katika mchezo ambao ndio siku hiyo amepewa kadi nyekundu,it means mchezo huo aliopelewa kadi unahesabika kama ndio mchezo wa kwanza kwa mchezaji husika kutumikia adhabu ya kukaa nje michezo mitatu,hivyo mchezo husika unapomalizika anakua amebakiza michezo miwili ya kukaa nje ya dimba kati ya mitatu.

  Hivyo canavaro sijui mwasika na pamoja na salum aboubakar wa azam,mchezo wao wa kwanza kutumikia adhabu ya michezo mitatu ulikuwa ni ule wa azam na yanga!
   
 6. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Tibaigana ameongozwa na hisia ambazo zinatoka kwenye moyo wake na akasahau kutumia ubongo ambao ndiyo unajua na umejicunza sheria.
   
 7. Asango

  Asango JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kadanganye wanawake wenzio!
   
 8. +255

  +255 JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,909
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Aliyepewa red card ni Cannavaro na sio Mwasika.
   
 9. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 1,746
  Trophy Points: 280
  USIMBA na UYANGA
   
 10. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ... tatizo mlegezo.
   
 11. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kama kumbukumbu ni sahihi, Mwasika hakupata adhabu yoyote ya uwanjani. Hivyo hana red card.
   
 12. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Wewe ni Muongo mkubwa....

  Katika mechi ya jana Stephano Mwasyika hakuwepo hata kwenye benchi la wachezaji wa akiba na hata katika mechi na Azam Stephano hakupewa kadi nyekundu licha ya kwamba yeye ndiye aliyempiga ngumi muamuzi Israel Nkongo....Aliyepewa kadi nyekundu ni Nadir Haroub na ilikuwa ni kadi nyekundu kavu(bila kupewa kadi ya njano) yaani straight red card....

  Kinachoangaliwa hapa ni kanuni za TFF za kudhibiti wachezaji wanapofanya makosa uwanjani na kanuni ya 25 inasema hivi:

  a). Mchezaji atakayetolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi mbili za njano,hataruhusiwa kucheza mchezo
  mmoja.

  b). Mchezaji atakayetolewa kwa kadi nyekundu bila kupewa kadi ya njano(straight red card) hataruhusiwa kucheza
  michezo miwili.

  c). Mchezaji atakayetolewa kwa kadi nyekundu kavu(straight red card) kwa kosa la kupiga au kupigana hataruhusiwa
  kucheza michezo mitatu inayofuata ya klabu yake na atalipa faini ya Tshs. 500,000/

  d). Wachezaji watano wa klabu moja wakipata kadi katika mchezo mmoja(nyekundu au njano) klabu itaadhibiwa kulipa
  faini ya Tshs. 500,000/

  e). Mchezaji akipata jumla ya kadi tatu za njano hataruhusiwa kucheza mchezo mmoja.

  Kwa suala la Nadir yeye anaangukia katika kipengele 'c' ambapo alipewa kadi nyekundu kwa kutuhumiwa kumpiga refa,na baada ya kupata adhabu hiyo tayari alikosa mechi 2,hata hivyo adhabu yake hii ni mojawapo ya zile adhabu zilizositishwa na kamati ya Nidhamu na Usuluhisi ya TFF so Nadir aliingia uwanjani akiwa huru baada ya adhabu za wachezaji wote kusitishwa mpaka kamati hiyo itakapokutana jumanne ijayo na kutoa maamuzi upya....

  Tatizo sio Yanga....Tatizo ni TFF na umbumbumbu wao katika kusimamia kanuni na taratibu walizoziweka...Wanazo kamati nyingi mpaka wanashindwa hata kuzidhibiti kamati hizo......
   
 13. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,861
  Likes Received: 4,243
  Trophy Points: 280
  Ndo tatizo letu wa-tz tutaishia kutetea upuuzi kwa kujali hisia zetu km alivofanya Tiba, matokeo soka letu linabaki km cha ndimu tu na tunaendelea kujinasibu kwa timu za nje oh, mi Man u, mi Arsenal, mi Brazil mi Ghana...
   
 14. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  swala ni kwamba watoa maamuzi tanzania hii ni zaidi ya mmoja kwaiyo kila m2 anafanya awezavyo
   
 15. papason

  papason JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Kwa vile leo ni siku ya wajinga nakusamehe, vinginevyo leo ningekuharibia siku asubuhi asubuhi....
   
 16. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Inamaana watu mmesahau kama leo ni FOOL'S DAY??
   
 17. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Kakak mimi pia ni YANGA TENA MWANACHAMA HAI!
  ILA KWA HILI UNAPOTOSHA!
  KASOME TENA SHERIA!
   
 18. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​haya mdigo tumekuelewa ila leo ni fools day
   
 19. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuuu umetoa elimu ya bure kwa wajinga.
   
 20. n

  nyandaojiloleli JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  soka la bongo halifai kabisa
  ni soka uchwala halina maana ndo maana tuko nyuma vibaya mno.
   
Loading...