Cathode Rays
JF-Expert Member
- Nov 3, 2011
- 1,738
- 1,492
Wapendwa wana MMU,
Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifanikisha na kunivusha katika hatua ya muhimu kwenye maisha yangu mnamo siku ya tarehe 24/11 ambapo nilijipatia mwenza wa maisha huko mkoani Tanga. Kama ndoto lakini imekuwa kweli na sasa siko peke yangu tena bali tu "wawili tulio mwili mmoja"
Tumekuwa na wakati mzuri pia kwa honeymoon tukifurahia ndani ya Tanga, kisha tukakatiza mpaka Bwagamoyo hapo angalau kupitia historia inayopatikana eeneo hilo tukajirukia zetu na FastJet kutoka Dar mpaka KIA na kutumbukia hapo Arusha angalau kuendelea kushangaa maajabu ya Mungu na kisha kurudi tena Dsm na leo rasmi nimerudi kazini Morogoro....
Mpwa Elli, snowhite, Pdidy, Mamndenyi, Mbimbinho na wengine wote, ahsanteni kwa shule nzuri mliyonipatia na changamoto za hapa na pale....
Karibuni sana Morogoro na ahsanteni kwa yote

Last edited by a moderator: