'Baby walker' yangu inataka kunipasua kichwa!

Babywoka yangu (IST/Passo)

Tatizo la kwanza limeanza juzi:
Nimerudi jioni home, nikapaki nikaingia ndani. Usiku nikawasha gari nilisogeze getini nikashangaa 'Parking' gear haioneshi kwenye dashboard.

Yaani 'Parking' haionekani kwenye dashboard ingawa gear ipo kwenye Parking. Gear zingine zote zinaonekana. Nikizungusha funguo niwashe (ignition) haiwaki, mpaka nipeleke kwenye 'Neutral' ndio inawaka.

Tatizo la Pili (Limeanza Leo):
Nalo linahusiana na Mambo ya gear, sema ni wakati naendesha (nipo kwenye mwendo).

Kuna muda nikiwa naendesha (nipo kwenye D) nikakanyaga mafuta kuongeza mwendo zaidi gari inapiga kelele za Race gyyyyyyym.
Ni ile sauti ya ukikanyaga mafuta gari ikiwa kwenye parking. Sasa mimi naisikia nikiwa kwenye mwendo.

Hii imenitokea mara mbili, na inapotokea inabidi niachie mafuta kisha nikanyage tena mdogo mdogo ndio inarudi kwenye hali ya kawaida.

Wakuu, haya matatizo mawili yatakua na uhusiano? Yanaweza kuwa chanzo ni kitu gani? Spark plugs, Coil, nozzle, transmission fluid ama yaweza kuwa Nini wakuu.

Yaani kuwasha gari mpaka niweke Neutral (Kama kuna mteremko gari inaanza kuserereka duh)

Na hiyo ya kupiga resi (kupoteza gear ghafla) napokua nakanyaga mafuta kuongeza mwendo.
Mlolongo, mbona unaona aibu kutaja aina ya gari yako? Hivi ungekuwa na BMW au Mercedes Benz, ungeona aibu hii uinayo sasa?
 
Aiseeh hii kali!! Ist/passo si zipo nyingi sana mjini sasa atajuaje
Anafaham eneo naloishi. Lakin exact mtaa haujui. Na anajua nina gari ndogo.
Kwa msala ule aliniachiaga mpaka kunitumia 'ma-baunsa' aisee niko chonjo.
 
Kwani mkuu kwenye mteremko ukiweka neutral na kukanyaga break gari litaserereka?
Mkuu... Heshima yako kwanza.

Story iko hivi.
Gari za siku hizi (zinazotumia umeme) ili iwake (ignition) lazima gear iwe kwenye Parking au Neutral.
Sasa tatizo ni kuwa Parking haioneshi, maana yake the only option ni kuwasha gari ikiwa kwenye Neutral.

Haya, unasema kukanyaga brake, brake za gari ya umeme haifanyi kazi kama gari haijawaka.
Na ndio maana ukijaribu kukanyaga brake wakat gari imezima utaona kabisa brake pedal haishuki chini. Mpaka engine iwake.

Kwahiyo nawashaje gari:
Naingia, nachomeka funguo, naweka Neutral (Foot Brake Haina kazi hapa, maana gari imezima), kisha nazungusha funguo. Kama gari ilikua kwenye mteremko lazima isereke kidogo kisha inasimama kwa msaada wa 'Hand Brake'.

Kuserereka nakomaanisha ni pale gari haijawaka, ndio umeweka Neutral unataka uiwashe sasa. Kumbuka hapo foot brake haifanyi kazi maana engine haijawaka bado.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom