sangujoseph
Senior Member
- Nov 30, 2015
- 164
- 183
Kurudi katika matumizi ya dawa za kulevya kwa msanii Chidbenz licha ya mara ya kwanza kutangaza kuacha watu wa kwanza ninaowaelekeza lawama hizi ni BABUTALE na KALAPINA maana hawa ndo watu wa mwanzo kujitokeza kumsaidia Chidbenz alipoonekana na tatizo hilo kwa mara ya kwanza.
Kwanini nawalaumu hawa BABUTALE na KALAPINA nakumbuka hawa ndo walipropose [HASHTAG]#CHIDBENZ[/HASHTAG] aende Sober house Bagamoyo kwa ajili ya tiba na utaratibu wa pale mgonjwa lazima akae miezi 3 kama awamu ya kwanza ya Matibabu akionekana hali yake haijatengemaa anaongezewa miezi 3 mingine.
Ajabu kwa Chidbenz alikaa mwezi mmoja tu Sober house kabla hajamaliza Dozi BABUTALE, KALAPINA waliamua kumuondoa kituoni hapo wakiamini kwamba ameshapona na mlezi wa kituo alipowashauri walisema watahakikisha Chid Harudi kwenye Madawa manake walikubali kubeba mzigo lawama Endapo chid angerudi katika madawa kama tunavyomuona sasa TALE na Kalapina hamna budi kubeba lawama za chidi kwa kuwa mliridhia aondoke bila kumaliza tiba.
Kwanini CHIDBENZ alipokuwa katika matibabu chid alitaka kuishi kama mtu maarufu ambapo alikuwa akiwadharau Wauguzi wake na wagonjwa wenzake pia alikuwa na rafiki yake mkubwa ambae nae kwa mujibu taarifa nilizopewa aliruka ukuta wa Sober house siku chache baada ya chidbenz kuchukuliwa na kina TALE na KALAPINA.
Kuna haja kubwa ya wasanii wetu kujifunza kwa hili sio kulalamika kama Madee unasema ni kumdhalilisha kumpiga picha wakati yeye mwenyewe alishamuimba katika nyimbo zake kumweka kwenye mitandao naamini itakuwa ni second chance kwa yeye katika vita ya kuachana matumizi ya dawa kwa kuwa wadau wengi wataguswa kumsaidia.
[HASHTAG]#kijanamzalendo[/HASHTAG] [HASHTAG]#ilovetz[/HASHTAG] [HASHTAG]#maoniyangu[/HASHTAG] [HASHTAG]#Sangujoseph[/HASHTAG]