Babu yangu mdogo ni mkoma (Magusu) na ndio maana niliamua kusoma maalum ili kulinda utu wa kila mtu

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
ukoma.jpg


Ndugu Watanzania mimi DEOGRATIUS KISANDU ni Baba wa watoto na pia ni Baba kijana mzalendo kwa Taifa letu. Leo nimeonelea kuweka jambo hili wazi ambalo ni vigumu kwa mwingine kufanya kama nilivyofanya mimi.

Mdogo wake na Babu yangu mzaa Mama, Mzee BELLO wa Ubirimbi, wilayani Kahama, yeye ni mwenye Ukoma, na Ukoma huo sio wa kujitakia yeye bali ni mapenzi ya Mungu. Tambua kuwa yaweza kuwa wewe unanitenga mimi na kuharibu mipango yangu kwasababu ya babu yangu, wakati wewe mama yako au baba yako ni Kilema, au mwenye UKIMWI au mlemavu wa mwili mzima.

Mzee Bello Maziku pia ni FAMASIA wa MADAWA wa muda mrefu na ameweza kuimudu kazi yake ya Ufamasia kwa muda mrefu sana tangu niko mdogo nimekuwa namuona akifanya kazi yake ya kuuza Madawa ya binadamu na Mungu amekuwa akimbariki, mimi siwezi kumtenga kwa kuwa ni babu yangu tuu hata iweje. Na hii iwe mfano kwa Mafamasia wote.

Nilikuwa nawashangaa watu wakinitusi na wengine hata kunifanyia unyama au kuninyanyapaa kwasababu ya Babu yangu mdogo kuwa MKOMA, lakini sio wote wenye hali hiyo, kuwepo kwa mtu mmoja sio hoja na pia ukoma sio dhambi wala laana bali ni hali ya mazingira yalivyotokea, huoni wewe baba yako au mama yako amepata ulemavu kwasababu ya ajari na hufikirii kuchukia watu ni jambo baya au ndugu zako ni majambazi nao ni ulemavu.

Nimekuwa na shangaa eti kwakuwa una ndugu mlemavu basi uwe na rafiki walemavu tu, huu ni ujinga namba moja, urafiki hauchagui maumbile.

Nje ya kupenda sana siasa za maendeleo niliamua kwenda kusoma Shahada ya ELIMU MAALUM Chuo Kikuu cha SEKUCo kwasasa SEKOMU mwaka 2009 -2012(Lushoto,Tanga) kwa malengo mawili tu, moja ikiwa ni Kupata hati ya elimu katika siasa maana tayari siasa naijua, na mbili kujua jinsi ya kuishi na kusaidia watu wenye mahitaji maalum, kumbuka kila mtu anaweza kupata ulemavu wa aina yoyote bila kutarajia, yawezekana hapo ulipo unamatege au macho yenye malyenge, au Malaya au changudoa au albino lakini hujui kama pia ni hitaji maalum(ulemavu).

Babu yangu Mzee Bello aliwahi kuniambia “hii hali unayoniona nayo hata wengine wanaweza kuipata, hivyo penda watu wote hata wakikunyanyasa”. Wapo watu huwa wanafikia hata kuvunja urafiki kwa kuwa wanamjua babu yangu mdogo kuwa ni mkoma, lakini leo hii SERIKALI inatumia BUSARA yangu kuongoza NCHI, Viongozi wa dini wanatumia BUSARA yangu kwenye Madhehebu, Waimbaji wanaiga mastaili yangu, Dunia inanifuata na kunielewa japo nimetengwa(nimefungiwa ndani).

Nampenda babu yangu sana, nakumbuka iliwahi kufikia hatua ndugu wote wa baba yangu Mzazi walinitenga kabisa kutokana na baba yangu kuzaa familia ya wenye Ukoma, lakini Ukoma huo ndio umeokoa Dunia.

Niliwahi kuwashauri chama cha CHADEMA kumteua ubunge Viti maalum babu yangu Mzee Bello ili awakilishe walemavu wenye Ukoma. Ukimcheka babu yangu au kumtenga ni sawa na kujidanganya mwenyewe, ukinitenga mimi kwasababu ya Mzee bello(Dominick) ni sawa na kumchukia Bwana Yesu aliye watakasa wakoma. Kimsingi nimeweza hata kudhalilishwa kwa kuvujishiwa siri zangu za ndani za mapenzi kwa video kisa eti laana ya Ukoma, kufanya tu huo unyama ni tosha kuwa Taifa limelaaniwa.

SHIRIKA LA WAFRANSISKANI.

Nilijiunga na Shirika la Wafransiskani kama VIRAFRA vijana Rafiki wa Yesu wa Mtakatifu Fransisko jimbo la Kahama mwaka 1995 kwa kuwa Mtakatifu Fransisko aliwasaidia wakoma na wengine aliwaponya na ndio maana nimelelewa na WAKAPUCHINI, OFM na Ndugu wadogo wa Afrika wote Tanzania na Franscan Brothers wa Kenya (kupita mawasiliano).

Tanzania yote tu wakoma, na Ukoma wetu mkubwa ni Umaskini, maradhi na Ujinga na ndio maana hatujitambui. Mimi kama mzazi natambua kuwa kila mtoto ana mapungufu yake.

Nawatakia siku njema.

DEOGRATIUS NALIMI KISANDU

23 SEPTEMBER 2017.





I DECIDED TO STUDY SPECIAL EDUCATION DEGREE BECAUSE MY YOUNG GRAND FATHER HAS LEPROSY.

It was not my intention to study this Bachelor Degree(2009-2012) for employment but I studied in order to know how I can help people with Disabilities because my young Grandfather has Leprosy, through my experience of living with him for long time I learned many things, he is Pharmacist in deed since I was a kid, My name Deogratius Kisandu from Tanzania, I love all people who have and who have not disabilities because all we are before God. Remember Jesus was Loving Leprosy people and was healing them according to a bible. Do not segregate any people because your Leprosy now is HIV/AIDS, TIB,POVERTY, IGNORANCE, PROSTITUTION, HANDCAPPED, ACCIDENTS n.k, I Remember my father Clan segregated me because of Leprosy of my young father to my momy, but now after I tried to educate one by another they become aware with Leprosy person.

DEOGRATIUS NALIMI KISANDU

23 SEPTEMBER 2017.
 
Kwa mara ya kwanza umeandijka habari ya kutia huruma..

Ila ukweli siasa huji unajua kuonewaa..
 
huyu jamaa ananifurahishaga sana yaani
Leo hakuna mvua/mawingu wala upepo antena iko vizuri haijacheza

Namfananishaga na jamaa mmoja alikua anaitwa Ganesh enzi hizo JF. Halafu alikuja kuwa verified kuwa ni mtoto wa mwalimu na rubani mstaafu wa jeshi. Ila dishi lilikua lina vipindi vya kushika chanel. Siku nyingine chenga tu
Nadhani siku hizi wamempora simu

JF burudanii sana
 
Tanzania tuna uhitaji mkubwa wa wanajamii wenye mtizamo chanya kwa watu wenye ulemavu
hongera mkuu kwa uzi mzuri weny ujumbe
kula like
 
Kisanduuu......Muda mwingine huwa najiwaziaga tu...''SIJUI ALBADIR ?''....eti ''inawezekana hapo ulipo una matege au macho ya malyenge''
 
Mimi huwaga sikuekewi Deo. Mniwie radhi lkn kwa mada zako huwa sijui nikuweke kundi Gani.

Bandiko lako la mwisho kabla ya hili uliongeleaga kushtaki taasis zaidi ya moja kwa kukosa jina lako na kukunyima fursa.

Leo umekuja kivingine kbs kwamba unanyanyapaliwa kwasabb ya babu mkoma. Lkn ukisoma kwa umakin utagundua ni njia ya kutaka kupata mke wakati tayar unawatt.

Mm nikushauri tuu weka bandiko jf kwamba unawafurahusha mke ambaye atakuwa mama wa watt wako. Inatosha sana hizo nyuzi za hivi havieleweki
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ndo ubaya wa albadir huu...Yaani ni sawa na kurusha jiwe sokoni matokeo yake unampiga yule aliye wako.
What goes around must...
 
wala sio mke bali ni jinsi jamii zetu zilivyo.

Mimi huwaga sikuekewi Deo. Mniwie radhi lkn kwa mada zako huwa sijui nikuweke kundi Gani.

Bandiko lako la mwisho kabla ya hili uliongeleaga kushtaki taasis zaidi ya moja kwa kukosa jina lako na kukunyima fursa.

Leo umekuja kivingine kbs kwamba unanyanyapaliwa kwasabb ya babu mkoma. Lkn ukisoma kwa umakin utagundua ni njia ya kutaka kupata mke wakati tayar unawatt.

Mm nikushauri tuu weka bandiko jf kwamba unawafurahusha mke ambaye atakuwa mama wa watt wako. Inatosha sana hizo nyuzi za hivi havieleweki
.
 
Back
Top Bottom