Babu wa Loliondo ni kisa cha kupungua watu kliniki za vvu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa Loliondo ni kisa cha kupungua watu kliniki za vvu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 14, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,330
  Trophy Points: 280
  Babu wa Loliondo kisa cha kupungua watu kliniki

  Imeandikwa na Stella Nyemenohi; Tarehe: 13th December 2011 @ 14:10 Imesomwa na watu: 301; Jumla ya maoni: 0

  [​IMG]
  [TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Marquee"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  WATAALAMU wa masuala ya afya wamefanya utafiti kuhusu tiba ya asili maarufu kama Kikombe cha Babu kinachotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Loliondo na kusema imechangia wagonjwa wengi wa Ukimwi kutohudhuria kliniki za tiba na ushauri.

  Utafiti huo ulioibuka na ushauri kwa Serikali kuelimisha umma juu ya magonjwa sugu, unatarajiwa kuwasilishwa keshokutwa katika Mkutano wa Nne wa Kisayansi wa Mtandao wa Afrika wa Ufuatiliaji na Utoaji Elimu ya Magonjwa ya Milipuko (AFENET).

  Mpango wa Mafunzo ya Ufuatiliaji na Elimu ya Magonjwa ya Mlipuko Tanzania (TFELTP) ulio chini ya Afenet ndiyo uliofanya utafiti huo Julai mwaka huu.

  Mkurugenzi wa Programu ya FELTP Tanzania, Dk. Peter Mmbuji ni mmoja wa walioandika matokeo ya utafiti huo.

  Wengine ambao hata hivyo hawakufafanuliwa taasisi wanazotoka, ni Christina Kahembe, Sasita Ramadhani, Boniface Panga, Thomas Ruta, Janneth Mghamba, Innocent Semali, Zubeda Ngware, Mohamed Mohamed, Azma Simba na Senga Sembuche.

  Wataalamu hao wanasema utafiti wao umebaini baada ya kutangazwa Kikombe cha Babu, kumekuwepo upungufu wa matumizi ya mfumo rasmi wa utoaji huduma ya afya miongoni mwa watu wenye magonjwa sugu.

  Utafiti huo wa TFELTP uliofanyika mkoani Arusha, ulilenga kupata matokeo ya dawa hiyo iliyoanza kutolewa na Mchungaji Mwaisapile Agosti mwaka jana ikitajwa kuwa inatibu maradhi yote sugu.

  Katika utafiti wao, walijaribu kupitia rekodi za wagonjwa wa Ukimwi, shinikizo la damu, kisukari na kifafa kutoka kwenye kliniki za kutolea huduma na matibabu ya (CTC) kando ya barabara iendayo katika Kijiji cha Samunge na pia kwenye kituo kinachotoa huduma kijijini
  hapo.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya kitaalamu, vituo viwili kati ya vitatu, vimebainika kuwepo kushuka kwa mahudhurio kwenye CTC kwa watu wenye Virusi vya Ukimwi.

  Vituo hivyo ni Seha ambacho mahudhurio yalishuka kutoka asilimia 48 hadi asilimia 38.

  Kituo cha Mount Meru, mahudhurio yalitoka asilimia 57 hadi 45. Wanasema asilimia 10
  zilipungua kati ya Januari na Aprili mwaka huu.

  Hata hivyo, taarifa hiyo inasema kwa upande wa shikinizo la moyo, kisukari na kifafa hapakuwa na mabadiliko yoyote katika mahudhurio.

  Taarifa hiyo inawakariri watumishi katika Kituo cha Mount Meru wakikiri kuwepo kushuka kwa idadi ya wagonjwa wa Ukimwi waliokuwa wakihudhuria katika vituo hivyo vya kutoa huduma na tiba.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,330
  Trophy Points: 280
  lakini waganga wa kienyeji wako wengi humu nchini wanendelea kuvuna kwa utapeli mtupu........
   
Loading...