Babu wa loliondo ni kama nabii musa na nyoka wa shaba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa loliondo ni kama nabii musa na nyoka wa shaba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MTENDAHAKI, Apr 19, 2011.

 1. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Baada ya Mungu kuteremsha nyoka wenye sumu kali wa aina mbalimbali(Ukimwi,kansa,vidonda vya tumbo,BP nk) ili kuwaadabisha wana wa Israeli wana wa Israeli walimlilia Musa (Babu wa loliondo) awaombee kwa Mungu ili awaondolee janga hilo,baada ya musa kumsihi Mungu mungu alimwambia Musa(Babu wa loliondo) amsimamishe nyoka wa shaba (kikombe cha shaba) ili kila atazame asidhurike na nyoka. Ni wale waliotii na kuamini bila mashaka na bila kuteremsha macho kuwatazama tena nyoka ndio waliopona!
  Kama haitoshi Musa(Babu wa loliondo) alipokuwa akitoa ishara kwa farao kuwa ametumwa na Bwana aliagizwa aitupe fimbo yake chini nayo itageuka kuwa nyoka tazama baada ya musa kuitupa fimbo yake wachawi na werevu (vikombe vya tabora, mbeya, ruvu moro nk) nao walifanya vivyo hivyo tazama nao fimbo zao zilgeuka kuwa nyoka lakini nyoka wa musa(Babu wa loliondo) aliwameza wale wengine! Babu katumwa na Mungu!
   
 2. n

  ng'wandu JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sio kweli, samahani sana lakini tafsiri yako ya maandiko iko nje kabisa. Nabii kwa mfano wa Musa ni Yesu Kristo peke yake. Yeye alitumwa na Mungu awaokoe wanadamu kutoka kwenye utumwa wa dhambi kama vile Musa alivyotumwa awaokoe Israeli kutoka utumwa wa Misri. Nyoka wa shaba aliyetundikwa juu ya mti na Musa alikuwa ni mfano wa Yesu ambaye angelikuja kutundikwa msalabani ili awaokoe wote wanaomtazama. Na ndyvyo anavyofanya hata leo, mtu akimwamini Yesu kuwa anaweza kumwokoa ataokoka. Babu wa Loliondo hajatumwa na Mungu, ni mganga wa kienyeji yule!
   
 3. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  hyo ni imani yako, tuache tusioamini miziziology tuangamie.... una ushahidi gani mungu amemtuma hyo babu yako wa loliondo?
   
 4. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  nani kakwambia kuwa nyoka wa shaba ni yesu!Yeye mwenyewe hakuna kifungu chochote alichojitambulisha hivyo,hizi ndo tafsiri mbaya za kibiblia Ng'wandu!Soma maandiki kama yalivyo na tafsiri kwa usahihi acha kufananisha vitu!Kama yesu ni mungu basi ijulikane kuwa Amri ya pili ya Mungu inakataza kuweka mfano wa kitu chochote (akiwamo nyoka wa shaba) kama mfano wa mungu!
   
 5. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nimeingia leo kutoka Loliondo. It was really fantastic voyage. Nimefurahi kuuona live na kupiga piche mbele ya Mlima wa Mungu, Oldonyo Lengai. Daima nilikuwa na shauku kubwa ya kuuona mlima huu lakini Babu wa Loliondo kanifanya nione kwa macho hatimaye kupiga picha mbele yake.
  Jamani kapigeni vikombe, kama unapenda adventure uta enjoy sana.
   
 6. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Aminia Kiranja Mkuu,wasaidie kuelimisha na wengine waende hat kama ni utalii tu
   
 7. n

  ng'wandu JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yohana 3: 14 -15 inasomeka hivi "Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; - 15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye."
   
 8. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  nilijua ndio kifungu utakachokitumia,kiangalie vizuri na kwa makini,hakimhushi yesu na nyoka wa shaba!
   
 9. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Huo ni uzima wa milele mimi naongelea afya za watu duniani,kama ilvyokuwa kwa musa!Yesu hakuinulia kwa sababu watu walikuwa wanamlilia au walikuwa na shida ndio maana walimuua kwani hawakumthamini yesu alikuja ni kwa sababu mungu aliona uovu umezidi ulimwenguni ndipo akamtuma ili aje afe masalabani na kuuokoa ulimwengu!usichanganye maada!
   
 10. s

  sha Senior Member

  #10
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  NDG YANGU MTENDAHAKI POLE SANA,MAANA HUYAJUI UYAONGEAYO NA KAMA UNAYAJUA BASI WEWE NI MTENDA KAZI PAMOJA NA BABU WA UPANDE ULIO KINYUME NA MUNGU, YAWEZEKANA mungu UNAYEMWONGELEA NI TOFAUTI NA MUNGU WETU SISI TULIO WA KRISTO YESU NA NDIO MAANA MAPEMA WATU WA JINSI YAKO WAKAANDIKIWA" 2 WAKORINTO 4:3-4 =LAKINI IKIWA INJILI YETU IMESITIRIKA IMESITIRIKA KWA HAO WANANAOPOTEA AMBAO NDANI YAO mungu WA DUNIA HII AMEPOFUSHA FIKIRA ZAO WASIAMINI, ISIWAZUKIE NURU YA INJILI YA UTUKUFU WAKE KRISTO ALIYE SURA YAKE MUNGU"
  1. ZABURI 107:18-20 HULITUMA NENO LAKE KUWAPONYA.
  2.LUKA 7:1-10 LAKINI SEMA NENO TU NA MTUMWA WANGU ATAPONA - HUNA HAJA YA KUINGIA CHINI YA DARI YANGU.
  IWAPASAPO KUWA WAALIMU KWA WENGINE MMEBAKI KUWA WATOTO WACHANGA KIROHO SABABU YA UVIVU WENU KATIKA KUJIFUNZA.
  3.WAKOLOSAI 2:17-18 =" MAMBO HAYO NI KIVULI CHA MAMBO YAJAYO,BALI MWILI NI KRISTO,MTU ASIWANYANG'ANYE THAWABU YENU KWA KUNYENYEKEA KWA MAPENZI YAKE MWENYEWE TU NA KUABUDU MALAIKA, AKIJIITIA KTK MAONO YAKE NA KUJIVUNA BURE KWA AKILI ZAKE ZA KIMWILI.
   
 11. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  nawashangaa mnagombana nini hapa wote mko sahihi kadiri Roho Mtakatifu alvokuangazia kuyaelewa maandiko.Ngwandu uko sawa,Mtendahaki uko sawa na ww Sha kulingana na mitizamo yenu.Kuna wale wanaouhubiriwa na wainjilisti wa vichochoroni wao hukazia neno kuwa kama wanavotaka wao na kuna wale wanaouhubiriwa na wainjilist na mapadri waliosoma zaidi theolojia na falsafa ya kanisa wao wanachambua maandiko na kuyalinganisha na hali halisi.Mfano nlimsikia nabii na mtume mmoja akitoa ule mfano wa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano akiwa ameshika sindano halisi kumbe hakujua anadanganya waumini kuwa Yesu hakumaanisha sindano tunayoshonea bali alimaanisa matundu yale madogo ktk ukuta kule uyahudini yanayopitisha kondoo na mbuzi tu ambapo ngamia kama mnyama mkubwa hawezi kupita.Hakuna anajejua maandiko wala usijifanye unayajua maandiko kwani hata mitume wenyewe hawakumwelewa yesu ingawa walikuwa nae siku zote hadi alipowaahidi Roho Mt kuja kuwaangazia.Hakuna mwenye ushahidi kuwa babu hakutumwa au katumwa na Mungu na pia sii wote waliomwamini Yule Nyoka wa Musa wengi walisita kuamini na walioamini Yule nyoka baada ya kupona waliiabudu ile sanamu ya Nyoka kuwa ndio Mungu wao wakasahu Mungu ndio kaagiza atengenezwe kama ishara ya watakaomini waponywe.ndugu zangu biblia ni kitabu kitakatifu kinachohitaji imani na maongozi ya Roho Mt kukielewa si kwa akili yako wala elimu yako pekee.Baba Yangu mzazi kaumwa siku nyingi katibiwa hospitali nyingi sana lakini alikwenda kwa babu na imani yake na ampeona kabisa magonjwa yake hatumii tena dawa yoyote na anafanya kazi zote bila tatizo lolote na daktari kathibitsha hilo.:A S 465:
   
 12. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  hapo kwenye blue ni imani yako
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Apr 19, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Vipi umepona?
   
Loading...