Babu wa loliondo na tiba ya magonjwa sugu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa loliondo na tiba ya magonjwa sugu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by babayah67, Mar 15, 2011.

 1. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF, Toka nianze kusikia habari juu ya tiba ya Babu wa Loliondo, nimesoma na kusikia mengi ndani ya magazeti na news media mbalimbali. Nimesikia taarifa za namna watu mbalimbali walivyoenda kwa babu na kupatiwa tiba hiyo. Wengi wa niliowasikia au kuwasoma maelezo yao wamekuwa wakielezea kupata nafuu ya haraka toka wapate hiyo dawa ya babu, na karibu 60 -70 % ya hao wagonjwa ni wale waliokuwa wakisumbuliwa na maradhi ya kisukari (Diabetic), ni leo hii ndio nimesoma taarifa ya mgonjwa wa HIV ilowekwa hapa JF, lakini before this sikuwahi kusoma sehemu yoyote kitu kama hicho zaidi ya kusikia tu mitaani story ambazo kiasi fulani ngumu kuziamini. Katika maradhi yote haya, SIJAPATA TAARIFA YA UHAKIKA ZAIDI JUU YA WAGONJWA WA KANSA, kama toka wapate dawa ya babu kama wamepona kabisa au kupata nafuu ya kiasi fulani. Nasema sijasoma sehemu yoyote. Ombi langu hapa JF ni kuwa kama kuna mgonjwa yeyote wa kansa aliepata bahati ya kufika kwa babu na kupata kikombe naomba atueleze maendeleo yake yakoje toka apate kikombe hicho??? Au kama kuna ndugu au Rafiki anayejua mgonjwa yeyote wa Kansa alopata dawa ya babu naomba anieleze/atueleze juu ya hii tiba kama imewaponya au kuwasaidia wagonjwa hao. Kutokana na kuwa sijapata soma au kuelezwa habari za wagonjwa wa kansa nashawishika kuamini kuwa huenda dawa ya babu inatibu Kisukari zaidi na maradhi yanayoambatana na kisukari kuliko maradhi ya kansa. Namalizia kwa kuomba huo ushuhuda hapa JF!!!
   
Loading...