Babu wa Loliondo kutoa kikombe leo 1-4-2011 Jangwani Dar

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
836
49
Leo saa 6 mchana babu atakuwa viwanja vya Jangwani Dar es salaam akitoa kikombe kwa wenye shida wote. Babu ameamua hivyo kusherehekea siku ya leo na kurahisisha huduma kwa wananchi. Kikombe atakitoa hadi saa 12 jioni na kurudi tena Loliondo ambako ndio makazi yake yalipo.

Nyote mnakaribishwa katika sherehe ya siku ya leo ambayo inasherehekewa pote duniani.
 
Leo saa 6 mchana babu atakuwa viwanja vya Jangwani Dar es salaam akitoa kikombe kwa wenye shida wote. Babu ameamua hivyo kusherehekea siku ya leo na kurahisisha huduma kwa wananchi. Kikombe atakitoa hadi saa 12 jioni na kurudi tena Loliondo ambako ndio makazi yake yalipo.

Nyote mnakaribishwa katika sherehe ya siku ya leo ambayo inasherehekewa pote duniani.

Leo ni sikukuu ya wajinga - msikimbilie Jangwani kwenda kupata kikombe
 
Babu wa Loliondo kutoa vikombe Jangwani
Imeandikwa na Waandishi Wetu, Dar na Loliondo; Tarehe: 31st March 2011 @ 23:30 Imesomwa na watu: 721; Jumla ya maoni: 2


Mchungaji Ambilikile Mwasapile "BABU" ametua Dar es Salaam kutoa huduma yake ya tiba ya kikombe kwa muda akisubiri eneo lingine kubwa zaidi aliloahidiwa na Serikali.
Babu aliwasili Alhamisi asubuhi kwa helikopta akitoka Loliondo ambako utoaji tiba umesimama kwa muda na Ijumaa atakuwa akitoa kikombe katika viwanja vya Jangwani ambako alisema nafasi ni pana zaidi.

Tofauti na Loliondo, Jangwani Babu ameweka vituo vipatavyo 10 ambako hadi usiku wa kuamkia leo, askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakishirikiana na watumishi wa Chama cha Msalaba Mwekundu walikuwa wakiendelea kusimika mahema.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili jana alasiri, Babu alisema, amefarijika kwamba ataweza kusaidia hata ambao walikuwa hawana uwezo wa kufika Loliondo.

“Nadhani nitawasaidia wengi ambao hawakuwa na uwezo wa kufika Loliondo, lakini bado nasema wagonjwa mahututi waendelee kubaki hospitalini na wenye Ukimwi waendelee na dawa walizopewa hasa ARVs,” aliasa Babu.

Kwa muda mrefu Babu amekuwa akitoa huduma zake katika kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro, Arusha ambako umati wa watu na misururu ya magari yanayokwenda huko, uliharibu mazingira hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika.

Kuharibika huko kwa mazingira kulisababisha baadhi ya magari kukwama na mengine kupata ajali jambo lililochangia ongezeko la vifo vya wagonjwa wanaokwenda kupata dozi na kutishia uwezekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko na kuongezeka kwa vifo.

Akizungumza jana na gazeti hili kuhusu masuala ya ulinzi na usalama wa eneo hilo leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema utakuwa imara na askari 200 wanatarajiwa kutumika kwa kazi hiyo na kuwataka wananchi wasiwe na wasiwasi.

“Barabara zinazokwenda Loliondo kutoka Arusha kupitia Mto wa Mbu, Monduli na kwenye hifadhi ya Ngorongoro wakati wa mvua hazipitiki. Hata barabara zinazotoka kwenye maeneo ya Bunda na Mugumu kwenda katika mji huo pia hazipikiki wakati mvua,” alisema Msaidizi wa Babu ambaye alikataa kutajwa jina.

Jana Babu na alisafirishwa kwa helikopta ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na leo atatoa huduma yake katika viwanja hivyo ili kutoa fursa kwa wagonjwa wengi kupata tiba hiyo bila kuharibu mazingira na miundombinu.

Pia Serikali imezuia magari yote yanayokwenda katika kijiji hicho na sasa wametakiwa kwenda Dar es Salaam kupata huduma hizo na ili kupunguza idadi ya vifo, tayari Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeanza kujenga zahanati ya muda kusaidia wagonjwa watakaozidiwa.

Hata hivyo uamuzi huo wa Babu umeshutumiwa na watu waliokuwa katika foleni kusubiri kikombe na wametishia kuandamana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kupinga uamuzi wa Serikali kumsaidia Babu kutoa huduma Jangwani.

Lakini mmoja wa wasaidizi wa Babu ambaye alizungumza na gazeti hili alithibitisha kuwa uamuzi wa Mchungaji huyo kuhamishia huduma zake Dar es Salaam kwa muda ni kutokana na kuongezeka kwa maombi ya watu na Serikali.

Msaidizi huyo alisema watu wengi hawana uwezo wa kwenda Loliondo kutokana na wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kujitajirisha kwa kutoza nauli kubwa inayofikia Sh 200,000 kutoka Arusha jambo ambalo watu wengi hawana uwezo nalo.

“Kama sasa hivi tu nauli iko aghali ina maana wakati wa masika itaongezeka zaidi, ndiyo maana tumeshauriwa kuhamishia huduma hii kwa muda Dar es Salaam,” alisema Msaidizi huyo.

Habari za kuaminika kutoka serikalini, zilieleza kuwa mti ambao unatumika kama dawa utaendelea kuchimbwa eneo hilo la Samunge na kusafirishwa kwa helikopta za JWTZ hadi Dar es Salaam.

“Serikali itatuma helikopta ambayo itatua Waso ambako kuna uwanja wa ndege ambao umekuwa ukitumiwa na viongozi wa kiserikali ambao wanaenda kutibiwa Samunge,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Mmoja wa wagonjwa ambao wanajiandaa kuonana na Babu leo alipotaka kujua zaidi kwa nini Mchungaji huyo amehamia Dar es Salaam ghafla, Msaidizi huyo wa Babu alimjibu : “Leo ni siku ya wajinga duniani”.
 
Back
Top Bottom