Suala la Babu wa Loliondo limeibuka tena Bungeni ambapo Mh. Dk. Dalali Peter Kafumu (Igunga) ametaka kujua status ya tiba ya Babu na kauli ya Serikali.
Naibu Waziri wa Afya akajibu kuwa dawa ya Babu imethibitishwa haina madhara kwa mtumiaji ila suala la kupona ni imani kati ya mtoaji wa dawa na mpokeaji wa dawa! Pia suala la matangazo ya dawa za jadi za kuongeza nguvu za kiume na urefu wa maumbile ya kiume likajitokeza kujua kama Serikali imeruhusu matangazo hayo.
Naibu Waziri akasema matangazo ya namna hiyo hayaruhusiwi kwa mujibu wa Sheria namba 23 ya mwaka 2002 inayosimamiwa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala pamoja na Sheria ya Vyombo vya Habari na Utangazaji. Ametoa agizo kwa wakurugenzi, waganga wakuu wa mikoa na wilaya kulitekeleza agizo hilo!