Babu wa Loliondo, Dawa za kuongeza Nguvu za Kiume vyaibua mjadala Bungeni


K

K-Boko

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Messages
700
Likes
7
Points
35
K

K-Boko

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2013
700 7 35
Suala la Babu wa Loliondo limeibuka tena Bungeni ambapo Mh. Dk. Dalali Peter Kafumu (Igunga) ametaka kujua status ya tiba ya Babu na kauli ya Serikali.

Naibu Waziri wa Afya akajibu kuwa dawa ya Babu imethibitishwa haina madhara kwa mtumiaji ila suala la kupona ni imani kati ya mtoaji wa dawa na mpokeaji wa dawa! Pia suala la matangazo ya dawa za jadi za kuongeza nguvu za kiume na urefu wa maumbile ya kiume likajitokeza kujua kama Serikali imeruhusu matangazo hayo.

Naibu Waziri akasema matangazo ya namna hiyo hayaruhusiwi kwa mujibu wa Sheria namba 23 ya mwaka 2002 inayosimamiwa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala pamoja na Sheria ya Vyombo vya Habari na Utangazaji. Ametoa agizo kwa wakurugenzi, waganga wakuu wa mikoa na wilaya kulitekeleza agizo hilo!
 
H

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2007
Messages
4,701
Likes
569
Points
280
H

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2007
4,701 569 280
Anasubiri kuoteshwa. Ndoto nyingine....
 
E

edward snowdern

Senior Member
Joined
Nov 30, 2013
Messages
139
Likes
0
Points
0
E

edward snowdern

Senior Member
Joined Nov 30, 2013
139 0 0
serkal haitaki watu warefushe mpini yaani wabaki na vibamia tehteh naambiwa waheshimiwa ndio wateja no 1.
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,724
Likes
3,407
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,724 3,407 280
Naibu Waziri wa Afya akajibu kuwa dawa ya Babu imethibitishwa haina madhara kwa mtumiaji ila suala la kupona ni imani kati ya mtoaji wa dawa na mpokeaji wa dawa!
Serikali yetu ina viongozi wajinga sana, ukisoma kwa makini hili jibu ndio utagundua kuwa tunaongozwa na misukule.

Unawezaje kuiita kemikali fulani ni dawa kama haujaithibitisha kama inatoa tiba???

Kwenye sekta ya utabibu na ufamasia huwa hakuna kitu kinachoitwa tiba ya imani, bali madawa na tiba nyinginezo zozote huwa ni matokeo ya tafiti za muda mrefu.

Sasa inakuwaje Waziri anachomekea suala la imani kwenye suala linalohitaji uchunguzi na utafiti wa kisayansi???

Hii nchi hii, eenh Mungu tusaidie waja wako
 

Forum statistics

Threads 1,251,958
Members 481,948
Posts 29,791,579