Babu wa Loliondo atangaza kukifufua kikombe

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
Mchungaji Ambilikile Mwasapile


Ngorongoro. Unamkumbuka yule Babu wa Samunge au Loliondo? Jina lake halisi anaitwa Ambilikile Mwasapile. Babu huyo pia ni mchungaji.

Mchungaji Mwasapile bado yupo na shughuli zake za kutoa kikombe cha dawa anayodai inatibu magonjwa yote yanayomkabili binadamu.

Hata hivyo, baada ya ukimya wa muda mrefu babu ameibuka na kuitaka kwa mara nyingine Serikali kuboresha miundombinu ya Loliondo kwa kuwa kuna mambo makubwa yanakuja kutokana na maono anayoonyeshwa. Akizungumza nyumbani kwake katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale jana, Mchungaji Mwasapile alisema watu waliokuwa wanakwenda kwa wingi miaka iliyopita wamepungua sana na sababu ni kuwa idadi kubwa ya walipokea uponyaji wakati huo.

Mchungaji huyo mstaafu alisema wito anaoutoa kwa Serikali kuboresha miundombinu unatokana na mambo makubwa anayoonyeshwa yatakayokuja wakati ambao Mungu ameupanga.
 
Mmmmmm yote sawa maana kama hospitali hazina dawa tunywe vikimbe,vijiko,na hata viloba lakini safari hii tutamtaka alipe kodi baaasi
 
huyu babu namkubali sn..miundombinu itaboreshwa ktk utawala huu maana hata mheshimiwa ni mmoja kati ya walipona
 
d61f7ecde9ef90153e064ff09c078142.jpg
 
Nilipita pale mwezi uliopita... Hakuna barabara nzuri.. No umeme... In short, Ngorongoro sehemu yenye umeme ni Loliondo Kwenye Gereza na pale WASSO Halmashauri...
 
Hii taarifa mbona ya muda mrefu Sana, anarudi Tena anarudi Tena wapi.
 
Back
Top Bottom