Babu Wa Loliondo Alikuwa Mgonjwa Wa Akili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu Wa Loliondo Alikuwa Mgonjwa Wa Akili

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by KIM KARDASH, Jan 6, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [h=3]Mobhare Matinyi: " Huenda Babu Wa Loliondo Alikuwa Mgonjwa Wa Akili"[/h]Submitted by Mjengwa on 1.1.12
  [​IMG]

  [​IMG]
  Maggid,

  Uko sahihi kabisa.

  Huyu Babu alikuwa janga kwa taifa letu na anapaswa kulaaniwa vikali na watu wote wenye akili timamu. Uwezekano mkubwa ni kwa Babu wa Loliondo kuwa na tatizo la akili ambalo halikujitokeza kwa namna tuliyozoea - ile kupiga kelele na kuvua nguo. Huyu babu labda ni mgonjwa akili aliyejikita katika imani za kimiungu.

  Watanzania, kutokana na ujinga wetu, umaskini wetu, na maradhi yetu, tulimpa fursa ambayo hakustahili. Taifa lenye watu zaidi ya 60% wanaoamini ushirikina, asilimia 40% wasiojua kusoma na kuandika, 35% wanaoishi katika umaskini uliokithiri, na viongozi wengi wanaoshinda kwa waganga, watu wanaofikiri kuwa unene tipwatipwa na ulevi ni afya, ni lazima mtu kama Babu angeonekana shujaa kwetu.

  Dawa za Babu zilielezwa na wazee wa Kisonjo kwamba ni za kawaida, na zinatibu magonjwa kadhaa likiwemo kisukari, lakini kwa ujinga wetu watu wakawa wanakunywa kikombe kimoja kwa kudhani imani za kimiujiza zitawasaidia. Wale mababu hawakunywa vikombe vya Babu na bado wanaendelea kuzitumia bila shida kila wakiumwa. Mababu wasiojua kusoma na kuandika wanatushinda akili watu tuliokwenda shule. Dawa zile zimefanyiwa utafiti duniani na zikaonekana kuwa na uwezo wa kufanya kazi fulani, hivyo, ukinywa kikombe kimoja unaweza kupata nafuu lakini hutapona kwa sababu hukunywa kitaalam. Unafuu huu ndio uliowapa wajinga imani kwa Babu anaponya.

  Babu hakuwa na utumishi wa uungu wowote wala utabibu wowote. Huenda ni mgonjwa wa akili na ni kweli amekuwa janga la kitaifa. Aibu na fedheha kwa taifa letu.

  Mobhare Matinyi.
   
 2. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Fedhea kwa serikali ya JK na viongozi wake vimeo karibia wote walikimbilia kwa babu kunywa kikombe.
   
 3. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Ndiyo maana Dr. Magufuli ni mmbabe sana kumbe anaishi kwa kutegemea kikombe cha babu wa Loliondo!!!!!!:embarassed2:
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  KKKT(kunywa kikombe kimoja tu)babu alikuwa sawa kulingana na imani ya kanisa lake,hivi bado watu wanaenda huko?
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Babu nasikia sasa hivi anamiliki kilimo kwanza(shangingi kama zile za mawaziri)mpya...
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Wajinga ndo waliwao

  Mwenye matatizo ya akili zaidi ni yule aliyekwenda kutibiwa na Kikombe kimoja kisicho dozi
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hata serikali yetu ni kichwa cha mwendawazimu haiwezekani kuruhusu watu watumie hiyo dawa pasipokuhakikisha na wakatuhada wanafanya uchunguzi kwakuchukua sample ya watu 200 na majibu yenyewe imekuwa kama kumsubiri Yesu. Na hili suala la babu limegarimu maisha ya waTZ wengi waliopuuza masharti ya hapo awali. Wenzetu kenya baada ya wanchi wao kwenda na hawakupona waliripoti ktk vyombo vya habari nakumkandia babu sana kitendo ambacho kilifanya wakenya kuamini hiyo dawa si sahihi na kuacha kwenda sijui viongozi wetu waliolewa madaraka walifanya nini
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Wagonjwa zaidi ni sie tulioamini na kufoleni kwake. Watu wametumia gharama kubwa kwenda kwa babu, wakiambiwa wafanyiwe ultra sound kwa tshs 10000 wanasema hawana hela! Wabongo bwana!
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kama babu alikuwa mgonjwa wa akili na wale waliokwenda kwake kupata kikombe je?
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Umesahau Serikali ilikataza halafu ika-withdraw? Umati ule ulikuwa unasikia la mtu? Nilimuambia mtu si ungoje mvua zipungue uende kwa raha zako, kidogo anirarue kwenye simu. Utafiti ulifanyika ndugu, matokeo ya maabara na ripoti ilishatoka. Mmea una medicinal characteristics lakini dose establishment haikuwa na scientific evidence (inaitwa statistical significance of dose effectiveness). Tembelea fikra pevu hapo juu
   
 11. Tz-guy

  Tz-guy JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  King'asti, tatizo watu wanalalamika tu bila kufuatilia ukweli, au walitaka serikali iende na FFU ndo wajue kwamba hawakubaliani na ule utaratibu wa babu. Halafu kitu kingine lile suala lilikaa kiimani zaidi hivyo serikali haikutaka kuingilia uhuru wa mtu wa kuabudu. Kiufupii ule mmea hauna matatizo ila utaratibu wa dozi ndio haukuwa mzuri ndio maana serikali ikawatahadharisha wananchi kwamba wasiache dawa za hospitalini.
   
 12. HT

  HT JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wagonjwest! Tuliwaonya watu lakini hawakusikia....wakavuna walichopanda.
   
 13. H

  Haika JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Saa hizi nasikia foleni za huko ni za watu wa nje ya tz. Nadhani dose itakuwa imebadilika.
  Kweli wagonjwa wa akili ni wale waliofuata mkumbo kwenda kutegemea miujiza bila imani husika. Wenye imani yao hawawezi kulalamika.
  Nadhani alikuwa anashangaa sana kuona watu wote wale wakidai wana imani na uponyaji wake
   
 14. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,318
  Likes Received: 610
  Trophy Points: 280
  Mkuu sijui unaongelea serikali ipi! Mkuu wa serikali alikuwa miongoni mwa watanzania wa kwanza kabisa kupata kikombe, akifuatiwa na zaidi ya nusu ya wajumbe wa baraza lake la mawaziri na wote kwa visingizio tofauti.
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kumbukumbu zinaonyesha wengi wa waliojitokeza hadharani kuipinga ile tiba ya babu walikua ni waislam japo walizomewa kila walipojaribu kufanya hivyo hadharani na watu watu dini nyingine wakionekana walikua wakisumbuliwa na wivu sababu babu sio sheikh na wala sio athuman,ally au mohamed...lakini hapa kila mtu anajifanya alikua anaipinga tuache uongo wengi tuliiamini wengine tulikosa tu nafasi ya kwenda loliondo lakini tulikua tunasononeka kwa kuikosa nafasi ile
   
 16. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Kwa maana nyingine wendawazimu walienda kupata kikombe kwa mwenzao???
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Babu wa Loliondo ni muhuni na tapeli, kawatapeli watu wengi sana, eti anatibu magonjwa yote huu si uhuni..

  Sasa hivi anakula bata tu
   
 18. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Lazima mtamkandia maana aliharibu dili za waganga wenu sana! Hata kama ni mgonjwa wa akili basi ugonjwa huo una faida maana aliongeza pato la Taifa, hebu ugua kichaa na wewe utibu watu tukuone!!! Na comment za wengi hapa ni za watoto wa "mamdogo" ambao majini na mapepo yao yalikosa dili sana!!!!
   
 19. Tz-guy

  Tz-guy JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu hao ni viongozi tu na wao wana uhuru wa kuabudu kama watu wengine, ila serikali ilishatoa tamko. Sasa kama mtu ataamua kuamini kitu sababu kiongozi fulani kaamini (hasa katika suala la kuabudu) basi hilo ni tatizo. Mimi sioni tatizo mtu kwenda kwa babu maana ni imani yake, ila napata shida watu wanavyosema serikali ilikaa kimya tu.
   
 20. Tz-guy

  Tz-guy JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu ngoja nikusaidie kidogo katika hili, makundi makuu yaliyopinga hili suala yalikuwa ni matatu:
  1. Waislamu
  2. Serikali, na
  3. Wakristo (Wanaojiita Wapentekoste).
  Pia wapo waganga wa asili waliojitokeza kupinga utaratibu wa dozi (ila dawa waliikubali) japo hawakuwa wengi.
   
Loading...