Babu wa Loliondo,ACACIA na media zetu

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,108
115,842
Toka jana baada ya Magufuli kukutana na CEO wa Barick vyombo karibu vyote vya habari vimejaa 'habari za pongezi' kwa Rais kwa 'kuweza kufanikisha kulipwa' tulichokuwa tunaidai hiyo kampuni.

Taarifa za habari za TV karibu zote na magazeti habari ni hizo hizo.

Licha ya ukweli kuwa jana hiyo hiyo Barrick na ACACIA wote wametoa taarifa za kukataa kulipa chochote sisi vyombo vyetu ni kama hiyo taarifa 'haituhusu' kabisa tuko bize na pongezi.

Inanikumbusha wakati wa Babu wa Loliondo jinsi ambavyo media zoote zilivyokuwa zinaripoti 'miujiza' ya babu huyo huku zikiwa hazitaki kabisa kuripoti taarifa za wagonjwa waliokuwa wanakufa baada ya kutoka huko Loliondo.

Hata taarifa za wataalam wa nje waliofika na kusema 'hakuna tiba' huko Loliondo wagonjwa wasiache dozi za hospitali zilipuuzwa.

Tulikuwa nchi nzima tuko excited na babu wa Loliondo na kikombe chake.

Yeyote aliongea vingine alionekana 'msaliti' na sio 'mzalendo'

Wapo waliotaka Babu wa Loliondo apewe tuzo maalum na kadhalika na kadhalika.

Vyombo vyetu vya habari ndo viligeuza habari ya 'kuuza' na kuwajaza watu ujinga uliopelekea hata watu wengine kupoteza maisha la kusikitisha hii tabia haijawahi kukemewa.

Sasa tuko na kupongezana na kuambiana uwongo mtupu licha ya wahusika kutoa ukweli wao kuwa hakuna walichokubaliana kulipa sisi ndo kwanza na wengine wanataka tuzo kwa tume na Rais aongezewe muda kwa 'haya mafanikio ambayo siyo ya kawaida'.

Sisi hatujifunzi kitu kwa kweli.
 
Hizi media bure kabisa wengine naona wamejikita kuisifia ndege ya huyu mkoloni kana kwamba inafaida yoyote kwa taifa
 
Usisahau pia media hazifanyi kazi ya kuelimisha tuu, ni kufanya biashara pia.breaking news zinazowavutia wateja wao

Kabla ya biashara..wanapaswa kuipa jamii ukweli
sio kwenda na upepo tu hata kama ni uongo
 
Toka jana baada ya Magufuli kukutana na CEO wa Barick vyombo karibu vyote vya habari vimejaa 'habari za pongezi' kwa Rais kwa 'kuweza kufanikisha kulipwa' tulichokuwa tunaidai hiyo kampuni.

Taarifa za habari za TV karibu zote na magazeti habari ni hizo hizo.

Licha ya ukweli kuwa jana hiyo hiyo Barrick na ACACIA wote wametoa taarifa za kukataa kulipa chochote sisi vyombo vyetu ni kama hiyo taarifa 'haituhusu' kabisa tuko bize na pongezi.

Inanikumbusha wakati wa Babu wa Loliondo jinsi ambavyo media zoote zilivyokuwa zinaripoti 'miujiza' ya babu huyo huku zikiwa hazitaki kabisa kuripoti taarifa za wagonjwa waliokuwa wanakufa baada ya kutoka huko Loliondo.

Hata taarifa za wataalam wa nje waliofika na kusema 'hakuna tiba' huko Loliondo wagonjwa wasiache dozi za hospitali zilipuuzwa.

Tulikuwa nchi nzima tuko excited na babu wa Loliondo na kikombe chake.

Yeyote aliongea vingine alionekana 'msaliti' na sio 'mzalendo'

Wapo waliotaka Babu wa Loliondo apewe tuzo maalum na kadhalika na kadhalika.

Vyombo vyetu vya habari ndo viligeuza habari ya 'kuuza' na kuwajaza watu ujinga uliopelekea hata watu wengine kupoteza maisha la kusikitisha hii tabia haijawahi kukemewa.

Sasa tuko na kupongezana na kuambiana uwongo mtupu licha ya wahusika kutoa ukweli wao kuwa hakuna walichokubaliana kulipa sisi ndo kwanza na wengine wanataka tuzo kwa tume na Rais aongezewe muda kwa 'haya mafanikio ambayo siyo ya kawaida'.

Sisi hatujifunzi kitu kwa kweli.
Sisi ndio Watanzania na hizi ndio media zetu.

Paskali
 
Ni kweli, ukweli ni kuwa it's one man shore, kile anachotaka ndicho kinachotekelezwa. Kulikuwa na nini cha kufungia mawiyo kwa mujibu wa sheria?
 
Mwakyembe hana haya
Nipashe kawaogopa

upload_2017-6-15_13-9-29.jpeg
 
Mkuu The Boss kaa tayari kuitwa mtetea majizi pia kuambiwa sio mzalendo. Unajua vyombo vya habari imebidi viwe na unafiki tu kwa kuhofia fedhea kama anayoipata yule mbunge wa upinzani
 
Media tutazilaumu sana kipindi hiki, mimi binafsi nawaonea huruma. Kama watu wamekatazwa kuwahusisha marais wastaafu na unyonyaji wa madini na leo Mawio wamefungiwa kwa kum-quote Tundu Lissu utafanyaje? Rais anataka apongezwe kwa kuchukua hatua kwenye madini na anasikitika kuwa nan katuloga, lakini hataki wahusika wakuu wa mikataba ya madini wasemwe-hiyo ni paradox.

Mkapa lazima alaumiwe kwa sakata la madini. Kikwete lazima alaumiwe kwa sababu ya mikataba ya gesi na mafuta. Kwenye gesi na mafuta kuna mabomu mengi, bado tu hatujapewa fursa ya kuyalipua.
 
Kama hawako huru vya kutosha baso bora wasikubali
kushirikishwa maigizo huku wanajua kabisa haya ni maigizo

Kuliko wao kushiriki kwenye hii 'praise and worship' mode...
 
Back
Top Bottom