Babu Tale: Wanaharakati uchwara siasa zimewashinda sasa wanashindana na Diamond Platnumz

babu tale ndio nani au ni yule jamaa wa comedy akiitwa kitale
Ni kichawi uchwara fulani hivi kilichomdanganya mwenda zake kuwa kina uwezo wa kumkinga asipate madhara.
Kalifanikiwa kupewa ubunge wa viti maalum kwa huu utapeli ila aliyetapeliwa ndio hivyo tena hatunae.
 
Hivyi babu tale??? Alichaguliwa na wananchi au alipewa ubunge?? Hawa ndo aina ya watu tulionao bungeni!! Ni hatari sana
 
Mwanaharakati si mwanasiasa. Mwanaharakati hupiga kote kote......Ukweli uko wazi, akiwa kama mwanamuziki maarufu Diamond na wanasanii wengine wote alipaswa kuwa neutral kama dada Judith Lady Jaydee. Kujitanabaisha kuwa wao ni ccm au cdm kwa waziwazi pasipo haya wamekosea sana. Siku wanamuziki vipenzi wa upinzani wakiwa nominated nao watakumbana na zengwe, na ikitokea chama kingine kikachukua nchi hata kama ni kwa kutotarajia, wasanii mashabiki wa ccm lazima watafanyiwa zengwe.

Music is a universal language, haipaswi mwanamuziki attached kwa tabaka lolote la kisiasa au chama cochote
Siyo kweli
 
Binafsi sioni tatizo Wasafi wakiwa CCM, naona tatizo wanaopinga yeye kupata tuzo kupitia kura za Watanzania wasio wana CCM kuitwa Wanafiki.
Music siku zote hauna Itikadi na inapotokea Mwanamuziki anajiingiza kwenye itikadi za kisiasa ategemee yoyote katika muziki wake haijalishi ni lini na wapi.
Mh. Mbunge ambaye ni meneja wa msanii tajwa kwenye kura za BET hapaswi kuliingiza suala la msanii wake katika siasa moja kwa moja, ingelibaki vile vile ilivyo na si yeye kujustify yanayoendelea mitandaoni na kuwabeza mashabiki kupitia itikadi zao.
 
Wanaharakati ni Wanasiasa ? (Is one necessarily the other) ?

An activist is someone who organizes and acts for the purpose of changing a public policy or law.

A politician is someone who seeks election to a public office on behalf of a general ideology and/or a specific agenda on which they promise to act.
 
babu tale bora ungekaa kimya kusitiri umbumbumbu wako.
Kwanza wewe ni mbunge ndio lakini mbumbumbu!
Ndio maana hata michango yako bungeni hata ongea yako ni ya ki-mbumbumbu.
Hilo Jimbo lako bado tunachunguza tujue kwanini walimchagua mbumbumbu!
 
Inashangaza kuona watu wanaohubiri demokrasia hawataki mtu mwingine awe na uhuru wa kushabikia chama tofauti na chao.

Diamond, wasanii kiujumla, wanahaki zote kama wananchi wengine kuwa wanachama na kushabikia chama wakipendacho.
 
Babu Tale kwanza namtabiria kuwa mbunge wa kipindi kimoja. pili namuona kama mbunbe maamuma kaenda huko kutokana uchaguzi wa hovyo wa 2020
 
Back
Top Bottom