Babu Tale kuweka kambi Morogoro Vijijini kwa ajili ya ubunge! Familia yagawanyika

M
Kuna mtu alileta video hapa JF huyo Tale akihojiwa kwenye kipindi cha bar tender amesema umaarufu na sifa yake kuu imetokana na maswala ya uchawi na kuloga, na akasisitiza kuwa hata yeye anapenda hivyo kwasababu yeye ni mswahili.
Dah! Mnahangaika sana nyinyi ndo wale matajiri wote ni wauza unga
 
Wasalaam,

Meneja wa Diamond Platinumz ambaye amefiwa siku tatu zilizopita ,kuanzia leo ameanza mchakato na kuendelea na mchakato wa kugombea ubunge wa Morogoro vijijini tiketi ya CCM.

Pamoja na mpango huo ndugu zake wa karibu wamekuwa wakiweka shinikizo la kupinga ndugu yao kugombea ubunge hasa kipindi hiki ambacho amefiwa na mke wake na uchaguzi umekaribia, na bahati mbaya ni juzi ametoka kufiwa na mke wake hivyo haitaleta picha nzuri kwenye jamii kwani ubunge usimfanye akasahau utu na yeye ni mfiwa hata msiba hajapoa na hata udongo kwenye kaburi la mkewe haujashikana.

Lakini ushauri wa ndugu na watu wa karibu wa Tale umegonga mwamba kwani waki ijayo Babu Tale anatarajia kwenda kuweka kambi Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya kugombea ubunge wa Morogoro Mjini.

Mi sijaona shida yoyote ile. Ni machungu kumpoteza mwenza wako hata na binadamu yoyote yule ila mtu akishatangulia mbele ya haki ametangulia tu lazima mipango mengine iendelee. Lazima alikuwa na mipango hiyo muda kwa bahati mbaya mke katangulia yeye lazima atimize ndoto yake
 
Kwa hio mama akifariki.. baba asiende kutafuta kazi kwa ajili ya watoto wake waishi maisha mazuri?

Huyo huyo babu tale watoto wake wakikosa ada mtamsema mtandaoni..

Hujui ubunge unalipa sana... unajua watoto wa wabunge wanavyoishi maisha mazuri.. sasa babu tale kuwatafutia hayo maisha watoto wake mnamponda. Mnajifanya hamjui ubunge unapatikana kwa kugombea jimboni na sio kila siku kuna mda wake.. babu tale akichelewa aseme amlilie mkewe itambidi asubiri tena hadi 2025.. huku hio miaka mitano watoto wanasota maisha ya kubahatisha.. hadi diamond ampe posho
Ubunge sio kazi ya kujitafutia kipato. Ni utumishi wa umma au kazi ya wito. Hatutafuti maisha kwa kutumia kazi za wito.
 
Back
Top Bottom