Babu Tale asema anajiandaa kisaikolojia kufungwa jela maana hana millioni 250 za kumlipa Sheikh Hashim Mbonde

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,497

meneja+pic.jpg


Dar es Salaam.
Wakati siku 14 zilizotolewa na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart & Co Ltd, kwa wakurugenzi wa kampuni ya Tip Top Connection Limited kutekeleza amri ya Mahakama zikikaribia kuisha, Hamis Taletale (Babu Tale), amejitetea huku akidai kuwa anajiandaa kisaikolojia kwa kifungo.

Babu Tale ambaye pia ni meneja wa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnum, pamoja na nduguye Iddy Taletale ni wakurugenzi na pia wanahisa wa kampuni hiyo.

Februari 18, 2016, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliiamuru kampuni hiyo kumlipa fidia ya Sh250 milioni Mhadhiri wa Dini ya Kiislam Sheikh Hashim Mbonde, kwa kutumia kibiashara mahubiri yake bila ridhaa wala makubaliano.

Babu Tale amekiri kupokea taarifa hiyo ya Yono, lakini akasema kuwa yeye hajui chochote kuhusu madai hayo, kwani hakuwahi kujihusisha na kampuni hiyo na kwamba hana cha kufanya bali anawasubiri kuona Yono hizo siku walizopewa ili waone hatua zitakazofuata.

“Lakini mimi nasema sijamdhulumu huyo mzee wala sijawahi kufanya naye biashara. Kwa kuwa hiyo ni amri ya Mahakama sawa sina cha kufanya, kama watasema tulipe nitaeleza uwezo wangu maana mimi sina uwezo huo wa kulipa hizo Sh250 milioni,” amesema na kuongeza:

“Kwa hiyo cha kufanya ni kujiandaa tu kisaikolojai hata kama ni kufungwa, kwani hata kina Mandela (Nelson) walifungwa jela hivyo hivyo.”

Amesema kuwa kampuni hiyo ilifunguliwa na ilikuwa ikimilikiwa na kaka yao Abdul Taletale (marehemu kwa sasa) kwa asilimia miamoja na kwamba baada ya kufariki kampuni hiyo haikuendelea na mali zake zote zilipotea kwani zilidhulumiwa.

Amesema kuwa japo anatajwa kama mhusika lakini hakuwahi kuwa mkurugenzi, mwanahisa wala kujihusisha kwa namna yoyote na kampuni hiyo na kwamba hakuona taabu kwani hakujua kama kuna siku yatatokea matatizo kama haya.

Ameongeza kuwa alifahamu kuwepo kwa kesi hiyo baada ya kaka yao kufariki, ambapo wakili wa mdai alimpigia simu akimtaka afike mahakamani, lakini yeye alipuuza kwa kuwa alijua si mhusika.

Kwa mujibu wa hukumu ya kesi ya msingi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, Juni 6, 2013 Sheik Mbonde aliingia makubaliano na kampuni hiyo, kutumia kazi zake za mawaidha, kwa kuzalisha, kurekodi na kuzisambaza na kugawana faida ya mauzo.

Hata hivyo, baada ya kukamilisha kurekodi masomo saba, kampuni hiyo ilimkatia mawasiliano hadi alipobahatika kukutana na ofisa mmoja wa kampuni hiyo, Adam Waziri ambaye alimweleza kuwa wamesitisha mpango huo.

Lakini Agosti 9, 2013, wakati mdai akiendesha mhadhara Bahi Dodoma, alibaini kuwa DVD za masomo yake zilikuwa zikiuzwa sokoni Dodoma na katika mikoa mbalimbali, bila ridhaa yake wala makubalino ndipo akafungua kesi hiyo.


Mwananchi
 
Hahaha ataenda kweli au mali zake zitakamatwa analeta mchezo hahahaha.
Ngoja anyanganywe pass ya kusafiria akose bata za kupiga picha ba mastar huko mbele
 
Ukiifanya dini kwa kumutumikia mungu haitazuru

Lakin ukifanya dini kama biashara itapendeza zaid


shehe mjanja sana anajua fika kabisa din hizi hazina maana yeyeto maana zimeletwa na waarabu ili wafanikishe biashara zao za kuuza tende na kanzu

Naye kaona aitumie dini kwa biashara zake za kuuza cd ili apate mamilion ya shilings


Haitazuru mazee
 
Nadhani kama lengo la sheikh mbonde lilikuwa ni MAFUNDISHO yawafikie watu ili wamjue Mwenyezi Mungu basi hana haja ya kudai fedha zote hizo ambae inaonekana kama alikuwa na lengo la kupiga pesa kuliko kueneza neno la Mwenyezi Mungu
We nawewe una haraka sana mpaka umeniwahi
 
Hili ni fundisho. Ukiona umekua na jina mjini au umeanzisha biashara tafuta mwanasheria uwe unamlipa akulinde. Kila mtu anataka kipande kidogo cha ulichonacho yaani huwezi kimbia kesi. Hakuna mtu mwenye pesa kidogo ambaye hagusi mahakamani angalau mara moja, ukiona hujagusa jua zamu yako inakuja.
 
Mbona maelezo yake yapo wazi kabisa!, hausiki na Kampuni hiyo na si mmoja wa wanahisa/wakurugenzi wa kampuni..sasa wanamuhusishaje? Au majina kufanana?..
 
Nadhani kama lengo la sheikh mbonde lilikuwa ni MAFUNDISHO yawafikie watu ili wamjue Mwenyezi Mungu basi hana haja ya kudai fedha zote hizo ambae inaonekana kama alikuwa na lengo la kupiga pesa kuliko kueneza neno la Mwenyezi Mungu
Usicheze na Shekhe ubwabwaz...!
 
Back
Top Bottom