Babu Seya, Papii Kocha wafungwa maisha - Soma hukumu

oooooooooooooooooops pumzi ndefu ngoja nitafute maji kama Bujibuji alivyotoa advice
 
Niko maeneo ya mahakamani - Ndugu na jamaa zao wanalia kwa uchungu hawaamini kilichotokea mpaka saa hii
Vipi wakili wao Marando ameridhika na hukumu hii,? au ameahidi kukata rufaa, na vipi kisheria anaweza kukata rufaa nyingine?
 
Ni simanzi sana kwa Nguza Sr. na Papii kocha, je baada ya rufaa hii kuna uwezekano kisheria ya nafasi ya hawa wawili kuendelea kutafuta uwezekano wa kujitetea? Wanasheria mtusaidie kuhusu hili.
 
nguza hangeweza kuachiwa labda serikali ije nyingine.....wanaojuwa wameelewa!! hata hao walioachiwa wawili ni at least ..kwa kuwa mahakama ya rufaa ipo somehow free..
 
....kikubwa ambacho hakuna anayekisema pamoja na hao wanaosema kuwa walikuwa mahakamani ni kutupa data kamili za kesi yenyewe.Je, ni ushahidi gani uliwakilishwa mpaka kufikia kwa majudge kutoa hukumu waliyotoa!?maana wote tunajadili bila kuwa na vigezo vyovyote zaidi ya kuwa tuliwapenda babu Seya na Papii kwa vipaji vyao.WEKENI DATA WATU WAJADILI KUTOKANA NA HIZO DATA HASA KWA NYIE MNAOSEMA KUWA MLIKUWA MAHAKAMANI..........
tuache longolongo.......
 
Vipi wakili wao Marando ameridhika na hukumu hii,? au ameahidi kukata rufaa, na vipi kisheria anaweza kukata rufaa nyingine?

Kumbuka katika muhimili huu wa mahakama, mahakama ya rufaa ndiyo mahakama ya juu kuliko zote na uamuzi wake ni wa mwisho. Generally, The only remedy ni kwamba mahakama hii haifungwi na maamuzi yake na inaweza kuyatengua.
 
kumbuka katika muhimili huu wa mahakama, mahakama ya rufaa ndiyo mahakama ya juu kuliko zote na uamuzi wake ni wa mwisho. Generally, the only remedy ni kwamba mahakama hii haifungwi na maamuzi yake na inaweza kuyatengua.
hivyo upo uwezekano wakarejesha ombi la kuachiwa huru upya mahakamani ?
 
nguza hangeweza kuachiwa labda serikali ije nyingine.....wanaojuwa wameelewa!! hata hao walioachiwa wawili ni at least ..kwa kuwa mahakama ya rufaa ipo somehow free..

Philemon Mikael, inaelekea mimi sijaelewa. Nguza hangeweza kuachiwa kwa sababu ushahidi uliotolewa hauachi shaka yoyote au kuna sababu nyingine? Kama tunaamini mahakama ya rufaa ipo 'somehow' (kidogo?) free, je ni vipi imeshindwa kuwaachia hao wawili (nguza na papii) pia?
 
nguza hangeweza kuachiwa labda serikali ije nyingine.....wanaojuwa wameelewa!! hata hao walioachiwa wawili ni at least ..kwa kuwa mahakama ya rufaa ipo somehow free..

weka wazi unamaanisha nini na si kusema tu wanaojua wameelewa.........NANI ANAHUSIKA...!?
 
hivyo upo uwezekano wakarejesha ombi la kuachiwa huru upya mahakamani ?

Mkuu Nguvumali,

Mpaka nisome 'Court of Appeal Rules' nijue zinasemaje kuhusu hili jambo, je, inatoa nafasi kwa aliyeshindwa kuiomba mahakama iyapitie maamuzi yake au la. Pili, ni wakati gani CA inaweza kukaa yenyewe(Suo Motu i.e on its own motion) kupitia uamuzi wake. Kwa kweli kwa sasa kuna nafasi ndogo sana karibu na hakuna kwa hawa waanga wa rufani kufahulu katika hili.
 
Thursday, February 11, 2010 11:50 AM
MAHAKAMA ya Rufaa nchini imeamuru mwanamuziki Nguza Vikingi na mwanae Johnson Nguza warudishwe gerezani kwenda kutumikia kifungo cha maisha baada ya kuonekana kuwa na hatia ya kutenda makosa hayo.
Mbali na wawili hao kurudishwa gerezani mahakama hiyo imewaachia huru watoto wa mwanamuziki huyo ambao wote walikuwa wanatumikia kifungo hicho baada ya mahakama hiyo kuona washitakiwa hao walibambikiziwa kesi.

Walioachiwa huru ni mshitakiwa wa tatu Mbanga Nguza na mshitakiwa wa nne, Fransic Nguza ambao ni watoto wa mwanamuziki huyo wameonekana kutokuwa na hatia na hawakuhusika katika ubakaji huo.

Nguza na Johnson “Papii” wamerudishwa gerezani kwa kupatikana na mashitaka matano ambayo yaliwarudisha rumande kati ya mashitaka 23 yaliyokuwa yanawakabili awali.

Hivyo hukumu hiyo ilioyotolewa mahakmani hap oleo asubuhi ndio mahakama ambayo ina mamlaka ya mwisho dhidi ya rufaa iliyowasilishwa na washitkwia hao na hawataweza kuachiwa huru tena labda msamaha wa rais uweze kuwakomboa wanamuziki hao.
 
Sheria ya kujamiiana ya 1998 inasema makosa yao hayana msamaha (Parole) likiwemo lile la msamaha wa rais.
 
umesikitika nn? kuachiwa au kufungwa maisha?
unaujua undani wa issue yenyewe?
Tuhuma za kulawiti watoto bana......kama kweli mm naona wapewe maisha, na viboko 10 kila siku!
Naona unanyemelewa na mtindio wewe.

Mazingira ya kesi ni utata mtupu kwa kuwa ktk kesi zote wanatafuta ushahidi wa kumtia mtuhumiwa hatiani na ushahidi huo upo katika mafungu mawili
  1. Nia OVU, yaani nia ya kutenda jambo ovu na hii ndiyo inampatia mtiwa hatiani hukumuni bila huruma ya mahakama.
  2. Tendo OVU, ila unaweza kutenda tendo ovu bila ya kuwa na nia ovu ndo maana kuna kesi kama manslaughter ambazo mtu anaweza kuwa acquited. mtu akitiwa hatiani ya kutenda kosa bila ya kuwa na nia ovu anaweza kupata nafuu ya kimahakama
Sasa tuje kwenye utata. Ni kwamba yule mwalimu ambaye alikuwa anawapeleka wale watoto machinjioni ni lazima alikuwa na nia ovu na alijua kinachoendelea. maoni yangu yananipa uhakika kutokana na kiapo chake au maelezo yake ktk ushahidi uliotolewa dhidi yake (nadhani alikiri pia). na hivyo akijua kinachoendelea halafu akawa anaorganize uhalifu kwa kuwapeleka wale watoto si mara moja pekee. huyu mwalimu alipaswa kutiwa hatiani ya ushiriki wa kupanga njama ya kusaidia kosa kutendeka. Pasipo mipango au njama si rahisi kosa kutokea kwa makusudi. Lazima hapa kuna utata maana hata ushahidi wa daktari naambiwa una utata ndani yake. Kama watu wanaohukumu wanamwamini Mungu (Hakimu aliye juu zaidi) basi wanapoamua kuwashindilia hatia watu ambao ushahidi dhidi yao una utata ni dalili ya kwamba nao hukumu inawasubiria. Kama watuhumiwa mahsusi wanaachiwa halafu kisanga kinawaangukia wengine ni ubaguzi wa haki na haifai kwa mahakama ya haki. Mwalimu alipaswa kula mvua sawa sawa na akina nguza. lakini kwa kuwa idara zetu zinaongozwa na utashi, shinikizo na pesa nje ya mfumo, basi haki ni nadra sana kuelekea kwa mhusika

Nadhani kesi hii inaweza kwenda mbele zaidi ikiwa waathirika wakiamua kutafuta haki zaidi.

Asilani sipendi mtu afanye jinai halafu aachwe ila ni budi kujithibitishia kwamba kweli huyu ni mhalifu kwa ushahidi usio na mashaka.
 
Sheria ya kujamiiana ya 1998 inasema makosa yao hayana msamaha (Parole) likiwemo lile la msamaha wa rais.
katika Jamhuri kosa kubwa kuliko yote ni kosa la uhaini, na kama nakumbuka vyema mzee Mwinyi aliwahi kuwasamehe , jamaa fulani hivi waliohusika na tukio la UHAINI la mwaka 1984....kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, nasema mfano huo kwasababu naamini hakuna mkosaji ambae Rais wa Jamuhuri hana uwezo wa kusamehe......kama nakosea nipo tayari kupokea maoni ya kisheria juu ya hili kwaajili ya kujifunza.
 
ok, tupeni hao watoto kwanza, tutakata tena rufani ya baba na papi, we are confident that they will be free before this year end!
 
Hao watoto walioachiwa huru kwa kudai kuwa wamebambikiwa kesi wanaweza kudai malipo ya mateso waliyoyapata ya kufungwa miaka ypte hiyo?
 
Back
Top Bottom