Babu Seya, Papii Kocha wafungwa maisha - Soma hukumu

Tatizo la Appeals za Tanzania ni kuwa hazipokei evidence mpya; mahakama inayoshukulikia rufaa hupitia faili la hukumu ya awali bila kupokea ushahidi mpya. Kwa hiyo wakili wako akiboronga katika kukusanya ushahidi wa kukutetea na kuwahoji kwa kina mashahidi wa mashtaka wakati wa kesi ya awali, kama ilivyotokea kwa huyu mzee, basi unakuwa na nafasi finyu sana ya kuokolewa na rufaa. Wakili wake hakufanya kazi nzuri ya kutosha katika kumtetea wakati wa kesi ya awali.

Jaji aliposema kuwa halikuwa jukumu la upande mashtaka kumpima Nguza kuona kuwa hakuwa na nguvu za kiume, alituma ujumbe wa wazi kuwa kama proof hiyo ingekuwapo, ingeweza kuweka reasonable doubt katika ushahidi wa upande wa mashtaka. Lakini upande wa utetezi haukusukuma hoja hiyo katika utetezi wake wakati wa kesi ya awali.

Pumzika kwa amani huko Keko mzee wa watu Nguza, ni afadhali watoto wako wawili wameachiwa huru; wataendeleza legacy yako.

Mkuu una soft copy ya uamuzi wa Mahakama ya Rufaa utuwekee hapa please?
 
Back
Top Bottom