Babu Seya, Papii Kocha wafungwa maisha - Soma hukumu

JF inanipa raha sana "Zombe" hushahidi haukutosha mahakama imemwachia watu wakapiga kelele angetakiwa kufungwa "Babu seya" ushahidi umetosha kafungwa watu wanapiga kelele angeachiwa!! Sijui lipi ni lipi watu tunaendeshwa kwa hisia au?
kweli kabisa wangeachiwa ingetukanwa serikali kuwa kwanini watoto wamebakwa na ushahidi upo serikali imewaachia.hawana wema binadamu.
 
Tatizo la Appeals za Tanzania ni kuwa hazipokei evidence mpya; mahakama inayoshukulikia rufaa hupitia faili la hukumu ya awali bila kupokea ushahidi mpya. Kwa hiyo wakili wako akiboronga katika kukusanya ushahidi wa kukutetea na kuwahoji kwa kina mashahidi wa mashtaka wakati wa kesi ya awali, kama ilivyotokea kwa huyu mzee, basi unakuwa na nafasi finyu sana ya kuokolewa na rufaa. Wakili wake hakufanya kazi nzuri ya kutosha katika kumtetea wakati wa kesi ya awali.

Jaji aliposema kuwa halikuwa jukumu la upande mashtaka kumpima Nguza kuona kuwa hakuwa na nguvu za kiume, alituma ujumbe wa wazi kuwa kama proof hiyo ingekuwapo, ingeweza kuweka reasonable doubt katika ushahidi wa upande wa mashtaka. Lakini upande wa utetezi haukusukuma hoja hiyo katika utetezi wake wakati wa kesi ya awali.

Pumzika kwa amani huko Keko mzee wa watu Nguza, ni afadhali watoto wako wawili wameachiwa huru; wataendeleza legacy yako.
 
Vipi wewe mbona unazungumza kama vile hapa ni mahakamani?


Mzee, si kama nipo Mahakamani, kinachojadiliwa hapa ni suala la kesi iliyokuwa mahakamani na mahakama ya Mwisho kabisa (ya Rufaa) imeamua hivyo ilivyo amuliwa, ukiendelea kujadilia misingi ya maamuzi hayo ni kwa ajili ya "academics" tu hakuna kinachoweza kugeuza ukweli!. Hivyo ndivyo ilivyo labda kama unataka tuzunguzme kibinadamu "kuwa Babu Seya ameonewa!".. kama hivyo, ndivyo tulivyosema tokea alipokata rufaa dhihdi ya hukumu ya Hakimu Mkazi na baadae ya Mahakama Kuu sasa na ya Rufaa.... mbado mjadala unaendelea? wa nini zaidi ya kusema wale wenye tabia kama ya Seya wajifunze?.
 
Naomba kuwafahamisha kilichotokea leo

with regards and respect.

===================

ONLINE REPORTER,
11th February 2010

Daily News


THE Court of Appeal has sustained both conviction and life imprisonment sentence against Nguza Viking and Papii Nguza for raping minors, but acquitted Nguza Mbangu and Francis Nguza of the charges.

Nguza Viking alias Babu Seya and his three sons, were serving life jail terms for raping and sodomising minors about seven years ago.

The rulling which was read this morning for two hours by Deputy Registrar of the court, Ms Neema Chusi, turned the court into a furneral like situation, whereby the three appellants, together with their relatives cried loudly.

Papii Nguza is the only one that did not cry.

The appeal was heard by Justices Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk and Salum Massati. Advocates Mabere Marando and Hamidu Mbwezeleni, represented the appellants.

MORE DETAILS TO COME
Naona siku hizi hakuna matumizi mazuri ya page ndio maana unaweza kutafuta post usiione. Mode hii na yenyewe ni siasa?
 
jamani hivi kweli umuingilie mtoto wa miaka sita, mbele ama nyuma anawezaje kutembea, ninadoubt kama alivyoshangaa kaka Marando......Lyamuya kila jambo alilofanya pale Kisutu lin mashaka sana.
 
eeeh mwenyezi mungu unisamehe kama mawazo yangu yatakuwa agains't na wengine..na unisamehe sana hasa ninapokuwa mgumu katika kusadiki hili jambo
Hii kesi mpaka inaisha sijasadiki kitu labda ni vile mie nimekuwa mgumu kuamini kama Thomaso katika biblia
Nguva na Papii kama kweli mlitenda matendo haya machafu mnastahiri kifungo mlichohukumiwa jela
Lakini kama hamkutenda haya mliyohukumiwa kwayo hukumu ya mungu ni ya haki kwa watu wote -mungu atawatetea
nahitimisha mjadala wangu -no more coment
thanx
 
eeeh mwenyezi mungu unisamehe kama mawazo yangu yatakuwa agains't na wengine..na unisamehe sana hasa ninapokuwa mgumu katika kusadiki hili jambo
Hii kesi mpaka inaisha sijasadiki kitu labda ni vile mie nimekuwa mgumu kuamini kama Thomaso katika biblia
Nguva na Papii kama kweli mlitenda matendo haya machafu mnastahiri kifungo mlichohukumiwa jela
Lakini kama hamkutenda haya mliyohukumiwa kwayo hukumu ya mungu ni ya haki kwa watu wote -mungu atawatetea
nahitimisha mjadala wangu -no more coment
thanx

copy & paste
 
Sheikh yahya alisema wote wangetoka...

Utabiri wa mtabiri wetu umegonga mwamba.

Huyu Yahya huyu naye aache sheria na katiba za nchi zifanye kazi. Mara utamsikia ooh mwaka huu hakuna uchaguzi, atakayempinga atakufa n.k.
Ananafasi gani katika hii nchi yetu kwani nchi inaongozwa kwa katiba na sheria.
 
Huyu Yahya huyu naye aache sheria na katiba za nchi zifanye kazi. Mara utamsikia ooh mwaka huu hakuna uchaguzi, atakayempinga atakufa n.k.
Ananafasi gani katika hii nchi yetu kwani nchi inaongozwa kwa katiba na sheria.
Si kuna mtu alisema hapa yuko UWT?
Nadhani pia anayo na ofisi yake pale magogoni iko jirani na ofisi ya yule ofisa wa habari wa magogoni pale.
Hiyo ndiyo nafasi yake katika nchi hii.
 
Tanzania amkeni, hawa jamaaa hawajaonewa wanastahili kufungwa.
Arguments za vijiweni naona zimetawala humu, kwa kuamini babu sea kaonewa, bila kutoa ufafanuzi.
mahakama ya rufaa imesha thibitisha wamelawiti so hakuna mjadala hapo.
 
Tanzania amkeni, hawa jamaaa hawajaonewa wanastahili kufungwa.
Arguments za vijiweni naona zimetawala humu, kwa kuamini babu sea kaonewa, bila kutoa ufafanuzi.
mahakama ya rufaa imesha thibitisha wamelawiti so hakuna mjadala hapo.
nahata kina Francis na Nguza Machine mahakama kuu ilithibitisha kua walibaka, na kustahili kifungo cha maisha, wakagongomelea msumari kwenye JENEZA ambalo Addy Lyamuya wa Kisutu alikua amewafungia kina Francis NA NGUZA machine.si kila kauli ya mahakama ni sahihi, hasa mahakama zetu hizi ...aah wacha tu.
hata hukumu ya mahakama ya Rufaa ilipowatoa vijana hao wawili kua hawana hatia bado unaaamini kua hukumu haina utata ?
 
hapa ndipo ulipo udhaifu wetu mkubwa kwenye vyombo vya sheria, haiingii akilini kabisa kwa watu waliohukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa moja, lakini baada ya miaka saba wngine wakaonekana hawakuwa na hatia?, is very shame, hii ni kesi ya kutunga kwa asilimia mia

wengi haituingii akilini, hii yote inadhihirisha kesi za kitanzania zinavyoendeshwa, kiholela, kiurafiki, kwa kujuana, etc... etc... ili mradi hakuna sheria inafuatwa, no wonder 3/4 ya walofungwa hawana hatia. wenye hatia wote hawafungwi sababu wana pesa. poor nguza, I hope watoto wake walioachiwa watalipwa fidia.
mungu yupo watatoka kama hawa wengine walivyotoka.
 
wengi haituingii akilini, hii yote inadhihirisha kesi za kitanzania zinavyoendeshwa, kiholela, kiurafiki, kwa kujuana, etc... etc... ili mradi hakuna sheria inafuatwa, no wonder 3/4 ya walofungwa hawana hatia. wenye hatia wote hawafungwi sababu wana pesa. poor nguza, I hope watoto wake walioachiwa watalipwa fidia.
mungu yupo watatoka kama hawa wengine walivyotoka

Angepigwa mawe na kufa ndo likichwa lako lingeelewa
 
Me nilikuwa nataka kujua je wakipatikana watu wa maana hata 5 then waka wacontact hawa Amnesty international je hawa jamaa hawawezi kuingilia kati ya hili swala au hawaruhusiwi??
 
eeeh mwenyezi mungu unisamehe kama mawazo yangu yatakuwa agains't na wengine..na unisamehe sana hasa ninapokuwa mgumu katika kusadiki hili jambo
Hii kesi mpaka inaisha sijasadiki kitu labda ni vile mie nimekuwa mgumu kuamini kama Thomaso katika biblia
Nguva na Papii kama kweli mlitenda matendo haya machafu mnastahiri kifungo mlichohukumiwa jela
Lakini kama hamkutenda haya mliyohukumiwa kwayo hukumu ya mungu ni ya haki kwa watu wote -mungu atawatetea
nahitimisha mjadala wangu -no more coment
thanx

Ni kweli.. Issue kama hii sio vizuri kutoa hukumu moja kwa moja maana TZ sometimes kuna kutungwa kwa maneno na sisi wananchi tunachukua kama yalivyo.
Navyo hisi mimi kuna possibilities nyingi.

1. Uenda walifanya kweli -(Kama ni kweli itakuwa ni kutokana na imani za kichawi maana mtu mwenye akili timamu hawezi kufanya hivi tena baba na mwana)

2. Uenda ni kweli kuhusu yule kigogo kama tulivyosikia mitaani (Kama ni kweli basi mwenyezi mungu nae atamlipa either hapa hapa au siku ya mwisho)

3. Uenda ni kweli alichukua demu wa muheshimiwa na kubaka alibaka vile vile sasa kwa sababu hiyo basi watu wanaassume kwamba itakuwa ni muheshimu kalipiza.

4. Huenda kauziwa kesi -Alitengenezewa mtego akajikuta kanasa kweli...

Binafsi naona muheshimiwa si mwenye roho mbaya kiasi hichi jamani kisa demu tena sio mke afanye unyama huu. Vile vile naona it is impossible kwa mtu mwenye akili timamu kama nguza na aliyekuwa na chance nzuri ya kupata watoto wakali tu aende kubaka watoto washule.
In short niko kwenye dilemma sitaki kuamini chochote kati ya haya. But what i knw alikuwapo yupo atakuwapo yeye ndio atakae tenda haki isiyonashaka.

Japokuwa ni dhambi kusoma ALBADIR lkn ningekuwa sheikh ningeisoma kukata mzizi wa fitna. Kufungwa maisha si mchezo.. Ni sawa na kufa tu ... all your dreams goes away .....

Regards.
 
Me nilikuwa nataka kujua je wakipatikana watu wa maana hata 5 then waka wacontact hawa Amnesty international je hawa jamaa hawawezi kuingilia kati ya hili swala au hawaruhusiwi??

Tell me you are kidding buddy! Yaani Amnesty International iwatetee wabakaji, tena wa watoto wadogo? Pengine unaamini wameonewa lakini huelezi wameonewa namna gani. Ni nini kinakufanya uamini wameonewa? Kwa kuwa watu wengi wanasema hivyo?
 
Date::2/12/2010 Masikini Babu Seya, wanaye wawili waachiwa
Masikini Babu Seya, wanaye wawili waachiwa
%5Cseyawamivalo.jpg
Mwanamuziki maarufu wa kikongo, Nguza Viking 'Babu Seya' (katikati) na mwanaye Johson Nguza 'Papii Kocha' wakirudishwa mahabusi ya mahakama ya Rufani Dar es Salaam baada ya rufani yao kutupwa jana. YEYE NA PAPII NGUZA WAKWAMA
James Magai na Hussein Kauli

HUKUMU ya Mahakama ya Rufaa, iliyotolewa na jopo la majaji watatu jana iliibua vilio na majonzi baada ya kumtia hatiani mwanamuziki maarufu nchini mwenye asili ya Kongo, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Johnson Nguza hivyo kuendelea kutumikia kifungo cha maisha jela.

Hata hivyo, mahakama hiyo iliwaacha huru wanaye wengine wawili, Nguza Mbangu na Francis Nguza baada ya kubainika kuwa hawana hatia.

Babu Seya na wanaye, Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza walihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2004, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwatia hatiani kwa makosa ya kubaka na kuwalawiti watoto wa kike waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mashujaa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo walikata rufaa Mahakama Kuu ambako Jaji Thomas Mihayo (mstaafu kwa sasa), aliwatia hatiani na kuunga mkono hukumu ya Hakimu Mkazi Mkuu, Addy Lyamuya; kisha wakakata rufaa katika Mahakama ya Rufaa.

Katika hukumu ya Mahakama ya Rufaa, iliyotolewa na jopo la majaji watatu, Salum Massati , Mbarouk Mbarouk, wakiongozwa na Jaji Nathalia Kimaro waliosikiliza rufaa hiyo, iliyosomwa jana na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa (DRCA), Neema Chusi, Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walitiwa hatiani, huku Nguza Mbangu na Francis Nguza wakiachiwa huru.

Wakati akitoka nje ya mahakama kuelekea gerezani, Babu Seya aliendelea kusisitiza kuwa hakufanya kosa hilo na asingeweza kufanya hivyo na watoto wake, huku mwanaye Papii Kocha akisema kuwa wanategemea huruma ya Rais Kikwete na kwamba, wana imani kuwa atawatoa.

Wakili wao Mabere Marando alisema, "Tumeshinda nusu, tumeshindwa nusu. Huo ni uamuzi wa mahakama na kuwa hajawa na mpango wa kuendelea zaidi ya hapo."

Akisoma hukumu hiyo, Chusi alisema mahakama imeridhika na ushahidi ulioko kwenye kumbukumbu za mwenendo wa kesi hiyo kwa kila kosa na kwamba mrufani wa kwanza (Babu Seya) na wa pili (Papii Kocha), walihusika katika kutenda makosa na kwamba, utetezi wao kuwa hawakuwepo katike eneo la tukio ulikataliwa.

Kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama ya Rufaa, Babu Seya alitiwa hatiani kwa makosa matano ya kubaka na Papii Kocha alitiwa hatiani kwa makosa mawili, wakati Mbangu na Francis hawakupatikana na hatia kwa makosa yote.

"Mrufani wa kwanza amepatikana na hatia ya makosa mawili ya ubakaji kosa la 7 na la 12 kinyume cha kifungu cha 130 (2)(e) na 131A vya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) kama vilivyorekebishwa na vifungu vya 5 na 7 vya SOSPA (Sheria ya Makosa ya Kujamiiana),"ilisema hukumu hiyo na kuongeza:

Kwa kosa la 10 na 18 warufani namba moja (Babu Seya) na namba 2 (Papii Kocha) wamepatikana na hatia ya ubakaji kinyume cha kifungu cha 131A cha Kanuni ya Adhabu.

Hata hivyo katika kosa la 1,3,5,14, 20 na 22, warufani wote hawakupatikana na hatia, wakati katika kosa la 7 na 12 mrufani namba 1 mpaka namba 4 hawakupatikana na hatia huku kosa la 10 na 18 yakiwaondoa mrufani wa tatu (Mbangu) na wa nne (Francis).

“Hatimaye, hatia kwa mrufani namba tatu na wa nne inatanguliwa na hukumu pamoja na amri ya fidia inatupiliwa mbali. Wamewekwa huru isipokuwa kwa sababu nyingineyo. Na kwa mrufani wa kwanza na wa pili amri ya fidia bado inasimama tu kwa makosa ambayo yamewatia hatiani na inatupiliwa mbali kwa makosa yaliyobaki ambayo hayakuwatia hatiani,” ilisisitiza hukumu hiyo.

Mara baada ya Chusi kusoma hukumu hiyo majira ya saa 4:22 asubuhi, baadhi ya warufani hao waliangua kilio wakiwa kizimbani hususan Francis ambaye aliangua kilio kwa sauti kuu, huku Papii Kocha machozi yakimtiririka, lakini Babu Seya na Mbangu wakionekana kujawa na huzuni.

Chusi alianza kusoma hukumu hiyo kwa kuelezea kumbukumbu za mwenendo mzima wa kesi hiyo, akielezea ushahidi uliotolewa na mashahidi wa pande zote katika kesi ya msingi, hukumu ya rufaa ya kwanza ya Mahakama Kuu na hoja zilizotolewa na pande zote katika rufaa zote.

Kisha alisema; "Suala lililoko mbele yetu sasa ni kama ushahidi katika kumbukumbu ulithibitisha utendaji wa kosa. Kama ambavyo tayari imeshaonyeshwa PW 9 (Shahidi wa tisa wa upande wa mashtaka alikuwa ni mtoto wa miaka saba na alitoa ushahidi bila kiapo, ushahidi wake ulihitaji kuungwa mkono."

Katika ushahidi kwenye kumbukumbu hakuna mashaka kuwa PW9 alibakwa. Alithibitisha na kulikuwa na ushahidi wa PW20 kuwa PW9 alibakwa na PW9 alisema waomba rufaa ndio walimbaka.

Alisema jambo la msingi lilikuwa ni kuthibitsha kama waomba rufaa ndio walimbaka.

"Tumekwishatoa maoni juu ya mashahidi wa upande wa mashtaka na hatuhitaji kurudia kile ambacho tumekwishakisema. Inatosha kusema kwamba, kwenye kumbukumbu kuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa watoto walikuwa na uwezo wa kuingia katika nyumba ile bila kuonekana," alisema Chusi.

Alisema kwa mujibu wa uchunguzi wa hali ya nyumba iliyodaiwa kufanyika makosa yale kupitia kwa PW13, unaonyesha kuwa kulikuwa na mlango ambao ungeweza kutumiwa na watoto kuingia ndani ya nyumba ile namba 607 bila kuonekana.

Alisema kilichounga mkono ushahidi huo ni mazingira ya chumba cha mrufani wa kwanza (Babu Seya) ambamo ndimo kulimodaiwa kufanyiwa ubakaji, ambapo PW9 alieleza kuwa kuna godoro kitandani na godoro lingine ukutani na kwamba watoto wengine walikuwa wakilazwa kitandani na wengine kwenye godoro sakafuni.

"Tumesema mwanzoni mwa hukumu hii kuwa waathirika wa makosa ya ubakaji walikuwa ni watoto 10 na ushahidi wao katika maelezo yao kuhusu chumba cha mrufani wa kwanza unafanana,"alisema.

Akizungumzia utetezi wa Babu Seya kuwa alikuwa na matatizo ya nguvu za kiume na hivyo asingeweza kutenda kosa kama hilo na kwamba upande wa mashtaka ulikataa kwenda kumpima ili kuthibitishwa na daktari kama ana uwezo au hana uwezo wa kutenda kosa la ubakaji, mahakama iliutupilia mbali.

"Kwa maoni yetu upande wa mashtaka haukuwa na wajibu wa kufanya hivyo,"alisema Chusi katika hukumu hiyo na kuongeza:

"Tunasema hivyo kwa sababu katika kifungu cha 114 (1) cha Sheria ya Ushahidi (LEA) sura ya 6 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 suala la uwezo wa nguvu za kiume za mrufani ilikuwa katika ufahamu wake na suala la kuthibitisha lilikuwa juu yake kuthibitisha kuwa uume wake haukuwa ukifanya kazi".

Mahakama pia iliongeza kuwa ingawa kulikuwa na mazoezi katika nyumba hiyo(wanamuziki wa Bendi ya Akudo) haikuwa sababu ya kumzuia mrufani wa kwanza kutenda makosa kwa kuwa, kwa mujibu wa ushahidi matukio hayo yalikuwa yakifanyika kwa muda mfupi sana wakati wa mapumziko na wakati watoto hao wakitoka shule.

"Zaidi hakuna sababu kwa nini watoto wote hao waseme uongo dhidi yake na alikiri kuwa hakuwa na uhasama na mmoja wapo," iliongeza.

Kuhusu mrufani wa pili Papii Kocha, mahakama katika hukumu hiyo ilisema utetezi wake kuwa hakuwepo hauondoi uwezekano wa kutenda kosa.

"Tunasema hivyo kwa sababu kama ambavyo tumekwishaonyesha makosa yalikuwa yakitendeka kwa muda mfupi kama saa moja tu. Hii ina maana kwamba, hata kama mrufani wa pili alikuwa akifanya shughuli za kutumbuiza nje ya Dar es Salaam, lakini kuna wakati ambao alikuwa Dar es Salaam;

Kwa mujibu wa utetezi wake alikuwa akitoka nje ya Dar es Salaam kwa vipindi na si muda wote. Kwa namna hiyo hatuoni sababu yoyote PW8 ( mmoja wa watoto waathirika) kutengeneza ushahidi dhidi yake. Alikuwa ni mtoto mdogo ambaye hakujua hatari iliyokuwa mbele yake kwa kujihusisha katika, matendo ya ngono katika maisha yake".

Katika hukumu hiyo mahakama ilichambua ushahidi wa kila mtoto na kueleza jinsi ulivyoweza kuungwa mkono na mashahidi wengine, wakiwemo madaktari waliowafanyia vipimo baadhi ya watoto hao na kuthibitisha kuwa walikuwa wameingiliwa.

Ndugu na wakazi wa Dar es Salaam, wamepokea kwa mitazamo tofauti hukumu ya rufaa hiyo.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo, Cheta Chinyama ambaye ni ndugu wa Babu Seya, alisema kuwa Mungu anajua kilichofanyika wao watabaki kumuomba ili aamue.

"Sina mengi ya kusema kwa kuwa Mungu ndiye anayejua yote yaliyofanyika, hivyo tunamuwachia yeye, kilichobaki tutamuomba Mungu ili aamue," alisema Chinyama kwa uchungu huku akilia kwa kwikwi.

Shangazi wa Babu Seya aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwisa, alisema wao walitarajia kwamba ndugu zao wote wangeachiwa kwani walikuwa wakiomba sana kwa ajili yao.

Hata hivyo wanamuachia Mungu na kwamba wataendelea kusali kwa jina la Yesu ili siku moja waweze kuachiwa.

Mbali na masikitiko, baadhi ya wakazi wa jiji hilo wamedai kuwa pamoja na hukumu hiyo inaonyesha kuna siri kubwa imejificha ndani yake.

"Kitendo cha kuwaachia watuhumiwa wawili na kuendelea kuwafunga wengine inaonyesha kuna kitu kimetengenezwa kwa sababu kama walikuwa na hatia wote kwa nini leo wanawaachia wawili,"alihoji Kazimiri Pascal, mkazi wa Dar es Salaam.

Kwa upande wake Emmanuel Kashoke alisema maamuzi ya hukumu hiyo yameonyesha kasoro hasa katika vipimo vilivyodaiwa kuwatia hatiani watuhumiwa.

"Wanasema kwamba vipimo vya madaktari vilionyesha kuwa mlalamikaji alibakwa baada ya kupatikana na ugonjwa wa zinaa, sasa wamethibitisha vipi kama ule ugonjwa umesababishwa na mbakaji wakati hawakuchukua vipimo vya mbakaji, " alihoji Kashoke.

Salvatory Lumenyela, alizitaka nchi za Afrika kuanzisha mahakama ya rufaa ya Afrika kama ilivvyo kwa Ulaya ili kutoa fursa ya kupatikana kwa haki za wananchi.

"Lakini pia kuna haja kwa bara hili kuanzisha utaratibu wa kubadilishana wafungwa kwa sababu kama atakwenda nchini kwao anaweza kukata rufaa na kushinda kesi," alisema Lumenyela.
http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=17905
 
Sheria ya kujamiiana ya 1998 inasema makosa yao hayana msamaha (Parole) likiwemo lile la msamaha wa rais.


Sheria haiwezi kuwa juu ya Katiba ya nchi. Msamaha wa Rais umo ndani ya katiba kama ifiatavyo:

Ibara ya 45(1):

Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:-

(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa masharti, kwa mujibu wa sheria;
(b) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu yeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au asitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum;
(c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu;
(d) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote.

Kwa Katiba nzima bonyeza Hapa.

 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom