Babu Samunge adai kuhujumiwa, atabiri kufurika tena watu Samunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu Samunge adai kuhujumiwa, atabiri kufurika tena watu Samunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kamalaika, Oct 18, 2011.

 1. k

  kamalaika Senior Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 187
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Monday, 17 October 2011 21:32
  Mussa Juma,Samunge

  MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Ambilikile Masapila(76) ambaye, amekuwa akitoa tiba ya kikombe katika kijiji cha Samunge, amesema wateja wamepungua kwenda kwake kwa kuwa amefanyiwa hujuma.

  Msongamano wa magari Samunge sasa umekwisha, kati ya mwezi Januari hadi Juni mwaka huu, magari zaidi ya 500 yalifika Samunge kwa siku na maelfu ya wagonjwa, lakini sasa chini ya magari 15 yanakwenda kwa babu kwa siku. Magari mengi yanatoka nje ya nchi.


  Tofauti na miezi kadhaa, unapofika Samunge sasa idadi ya watu imepungua sana, wafanyabiashara wengi wameondoka, bei za vyakula zimerejea hali ya kawaida na kumuona Mchungaji Masapila hakuna urasimu.

  Akizungumza katika mahojiano maalum jana, huku akiwa bado anaendelea kulindwa na Ofisa Usalama wa Taifa, Mchungaji Masapila alisema kupungua kwa idadi ya Watanzania wanaofika Samunge kumetokana pia na desturi ya watanzania kuoneana wivu na kuchafuana tofauti na nchi jirani.

  Mchungaji Masapila licha ya kukiri kupokea taarifa za baadhi ya watu kutopona baada ya kunywa kikombe cha tiba, alisema kuna kundi la watu lilijipanga kudhoofisha huduma yake.

  "Ni kweli kuna watu walikunywa kikombe hawajapona, lakini hii ni tiba ya kiimani zaidi, wengi walikiri hawakufuata masharti,"alisema Masapila.

  Mchungaji Masapila alisema licha ya kufanyiwa hujuma kuna sababu kadhaa ambazo zinachangia Watanzania wengi kutofurika Samunge kwa sasa.Anasema miongoni mwa sababu hizo ni kuwa watanzania wengi wenye uwezo wakiwamo viongozi wa Serikali wamekunywa kikombe tayari na hivyo wamebaki watu masikini ambao hawawezi kugharamia safari ya kufika Samunge.

  Mchungaji Masapila pia alisema baadhi ya magazeti yalipotosha tiba yake na kusababisha watu wengi kutokwenda Samunge.Awali gharama za usafiri kutoka Arusha mpaka Samunge zilikuwa kati ya Sh150,000 na 100,000 na sasa zimerejea hadi kati ya Sh50,000 na Sh20,000 pia gharama ya mahema Samunge ilikuwa kati ya Sh50,000 mpaka Sh10,000 na sasa imebaki kati ya Sh10,000 na Sh 5,000.

  Uwezo wa tiba yake
  Mchungaji Masapila bado alisisitiza tiba ya kikombe cha dawa inayotokana na mizizi ya mti wa Mugariga inatibu magonjwa sugu kwani Mungu hawezi kumwotesha tiba isiyo sahihi."Mimi naamini hii ni tiba kwani kuna ambao wamepona na wengine hawajapona na hii inatokana tu na kufuata masharti au imani yao,"alisema Masapila.


  Kikombe bado ni kimoja hakuna kurudia
  Mchungaji Masapila alisema watu ambao hawajapona, wamekuwa wakimpigia simu kutaka kurejea kupata kikombe kingine, lakini amewaeleza kuwa wanapaswa kunywa kikombe kimoja tu na ambao hawajapona wanafanyiwa maombi.

  "Kikombe nimeelezwa ni kimoja tu, sasa siwezi kusema vinginevyo labda nipate maelekezo mengine kutoka kwa Mungu, ila ambao wananipigia simu naomba majina yao nay a wagonjwa ili niwaombee,"alisema Masapila.


  Licha ya watu wachache kufika Samunge kwa sasa, mchungaji Masapila bado anaendelea na mpango wa ujenzi wa kituo kipya cha tiba ambacho alieleza kuoteshwa ahamie.

  Masapila alisema tayari amenunua vifaa vya kupeleka maji katika eneo lipya vyenye thamani ya Sh7 milioni.


  Atabiri kufurika tena watu Samunge
  Mchungaji Masapila alisema bado anaoneshwa kuna watu watafurika tena Samunge kama ilivyokuwa awali.
  "Hata mwanzo nilikuwa nawaeleza watu hapa kuwa wataona magari na mamia ya watu Samunge hawakuamini na wakaona pia wataona tena,"alisema Masapila.Hata hivyo, hakufafanua ni lini watu hao watafurika Samunge na watakwenda kutibiwa magonjwa gani.

  Anunua magari ya kusaidia tiba akamilisha ujenzi wa nyumba yake.Katika kuhakikisha tiba ambayo inatoa inaendelea kuwa endelevu, Mchungaji Masapila amenunua gari aina ya Isuzu na Toyota Landcrusser kwa ajili ya kufuata dawa porini."Ni kweli nimenunua magari mawili ili yatoe huduma kwa kuwa siku hizi dawa zinapatikana mbali,"alisema Masapila.

  Mchungaji Masapila ameishukuru Serikali kwa kuendelea kumuunga mkono na kumpa ulinzi jambo ambalo linaendelea kumpa moyo."Naishukuru sana serikali wakati wote wamenipa ushirikiano mkubwa na bado wanaendelea,"alisema Masapila.


  Source: Gazeti la Mwananchi
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,902
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  akaunti yake inasoma kati ya 600m au 500m..what would you want more???kama ameoteshwa na Mungu mawazo ya anahujumiwa yanatoka wapi??nina shaka na upako wake kama kweli kasema maneno haya...
   
 3. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hana jipya,naye magamba muhujumu watanzania,kama watu wamekosa imani naye analazimisha waende,anataka kujitoa kwenye magazeti ili arudi kwenye ramani,jamaa mjanja huyu utasikia nimeoteshwa tena unaweza kurudia kikombe,aliyowadaka ndyo hao hao,aendelee kuwadanganya wageni,watanzania tupo kwenye mikakati ya kuwaondoa magamba,
   
 4. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  babu katoka uzeeni kweli maisha usikate tamaa
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee ni muuaji.
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  utukufu na uweza vina Yeye aketiye juu ya Kiti cha Enzi na Mwana Kondoo

  Jina la Bwana Libarikiwe!
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  He made millions if not billions, he generated businesses for many others, anastahili sifa ya ufanya biashara lakini si ya tiba. Waliokwenda wengi wamekufa na hakuna hata mmoja aliyepona. Ukweli ubaki kuwa ukweli.
   
 8. G

  Gambus New Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mashaka yake yanaonyesha jinsi tiba yake ilivyo na utata!kama mungu yupo upande wake anatapatapa nini?hii inaonyesha jinsi alivyo muongo!
   
 9. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Babu alikuwa Mjasiriamali ...
  Tangu mwanzao mimi nilishastuka..tiba gani ya mwenyezi Mungu ..ina masharti kibaoooo..
  mfano ..alikuwa anasema watu wasivuruge foleni..lakini wakija mawaziri..ruksa..
  kashapiga mpunga..yeye atulie tu!!!..bahati haiji mara mbili!!!
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Alimtoa mwanawe kafara huyu......
   
 11. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hehehe babu kamiss jero jero hana lolote
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Duh! Kumbe bado watu wanaendaga tu????
   
 13. Ziroseventytwo

  Ziroseventytwo JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 3,544
  Likes Received: 1,538
  Trophy Points: 280
  Tatizo la wabongo, ukitaka kumwibia mtangulizie neno "MUNGU" mfan6 mzuri ni huyu babu wa samunge. Na watu walioibiwa na "Deci" kwa kutumia mgongo wa kanisa!.wajinga ndo waliwao! Poleni
   
 14. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wanamuonea wivu? ebo nilidhani wagonjwa wanamuitaji babu kumbe babu ndo awahitaji wagonjwa. Asante babu kwa kufunguka. Indeed time do tell.
   
Loading...