"Babu" mwingine anapatikana Geita mlimani, karibuni!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Babu" mwingine anapatikana Geita mlimani, karibuni!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ms Judith, Mar 15, 2012.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Aliyekaribishwa Ikulu ampa JK sharti la kupanda mlima [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 14 March 2012 19:13 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Salum Maige,Geita
  SAKATA la muhubiri na muumini wa Kanisa la Kibaptist lililopo Wilayani Geita la kufunga bila kula kwa muda usiojulikana akifanya maombi kwa ajili ya Rais Jakaya Kikwete na Tanzania limechukua sura mpya baada ya muhubiri huyo kutoa siku 20 kwa Kikwete awe amefika kwenye mlima alioweka kambi kabla ya kushuka.

  Muhubiri huyo alitishia kuwa iwapo hatafika mambo yatakayolikumba nchi, asilaumiwe.

  Muhubiri huyo Mussa Lunyeka (35) mkazi wa Kijiji cha Chabulongo, Kata ya Bung’hwangoko, Kasamwa, amekuwa akiendesha maombi yake mlimani kijijini hapo kwa madai kwamba Mwenyezi Mungu amemwambia afanye hivyo.

  Kwa mjibu wa Lunyeka ambaye yuko kwenye kilima hicho tangu Feburuary 7, mwaka huu alisema kupitia maombi hayo, amemtaka Rais Kikwete afike kwenye kilima hicho kwa mazungumzo zaidi kuhusu mstakabali wa nchi. Alisema maelekezo hayo alipewa na Mungu.

  “Leo ni siku ya 29 niko hapa mlimani nimefunga kwa ajili ya kumwombea Rais wangu pamoja na nchi, kuna mambo ambayo nimeelezwa na Mungu na ninapaswa kumweleza Rais kuhusu mwelekeo wa nchi yetu.

  "Nikiwa hapa nimeoteshwa tena ndoto nyingine ikinitaka nishuke kweye kilima hiki Machi 30, mwaka huu na iwapo Rais kikwete hatafika hapa kwa siku 22 zilizobaki, naomba nisilaumiwe maana yatakayotokea hapa chini kwa mjibu wa ndoto yangu ni mambo mazito hivyo kabla hayajatokea namwomba Rais afike na kusikiliza niliyoelekezwa na Mungu.

  “Maandiko yanasema kwamba katika kitabu cha Zaburi 33:3, "Niiteni nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua, unaweza kujifikiria kuwa Mungu amekusudia neema kwa Tanzania, yawezekana kuna watu hawapendi kuiona hiyo neema kwa Rais na hata kwa Watanzania,. Mungu ameniambia nipande kwenye mlima huu na kufunga kwa kufanya maombi, na kuna mambo ambayo Mungu anapaswa kuzungumza na Rais kupitia kwangu kwa hiyo anapaswa kuja hapa nilipo ili nimweleze mambo hayo muhimu sana,’’ alisema Lunyeka.

  Mwaka jana muhubiri huyo alisafiri kwa baiskeli kutoka kijijini Chabulongo hadi Ikulu, Dar es Salaam kumpongeza Rais kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa mwaka 2010.

  Alisema mujibu wa maelekezo ya Mwenyezi Mungu, hapaswi kukatisha maombi na kuondoka kwenye mlima huo bila kuonana na Rais kabla ya Machi 30, mwaka huu. Akiwa kwenye mlima huo anakunywa uji na maji.

  Huku akisoma baadhi ya vifungu kwenye Bibilia, Lunyeka alisisitiza: "Nanaamini Rais wangu Kikwete ni msikivu na mnyenyekevu na kwamba baada ya kupata taarifa hizi kupitia vyombo vya habari, atafanya utaratibu wa kuja kuniona kwenye mlima huu ili asikilize anayotaka Mungu kunena naye kupitia kwangu kwa maslahi yake na Watanzania.

  "Tangu nianze maombi kwenye mlima huu, nimekuwa nikisikia maneno ya kejeli kutoka kwa baadhi ya watu kuwa nimechanganyikiwa.

  "Nataka nikueleza ndugu mwandishi, maandiko yanasema katika kitabu cha mithali 1:7 yanasema: "Kumucha bwana ni chanzo cha maarifa bali wapumbavu huidharau hekima na adabu,"alisema.

  Alisema kwa maandiko hayo yanatosha kuwaeleza Watanzania kwamba mimi sijachanganyikiwa bali natekeleza maelekezo ya Mungu.

  “Unajua ndugu yangu, Biblia inasema kuna wakati wa kulia na wa kucheka, wakati wa kusema na wa kunyamaza, kila kitu na wakati wake, wanaosema nimechanganyikiwa ni haki yao kusema hivyo, lakini mimi najua kwamba wakati utafika na wataamini kuwa huu ni wakati kwa Rais na Watanzania kulia au kucheka,” alisisitiza.

  Mwandishi wa habari hizi alipomtaka aeleze alichoambiwa na Mungu ili amueleze Rais Kikwete, alikataa kuweka hadharani kwa maelezo kuwa maelekezo hayo ni kwa ajili ya Rais pekee na siyo mtu mwingine.

  “Mungu hajaniambia kukueleza wewe, haya ni kwa ajili ya Rais peke yake, yeye akifika hapa atayapata kwa sababu atakayeyanena siyo mimi bali ni Mungu mwenyewe kupitia kwangu, kwa hiyo unaponiambia nikwambie nashindwa nikwambie nini, kama unakumbuka mwaka 2008 nilioteshwa kwenda Ikulu kwa kutumia baiskeli kumpongeza Rais iwapo angeteuliwa kwa mara ya pili kuongoza nchi yetu, nami nilifanya hivyo na sikumwagiza mtu mwingine badala yangu,’’ alisema Mhubiri huyo.

  Uchunguzi wa mwandishi wa habari hizi ulibaini kuwa mamia ya watu wamekuwa wakimiminika kumwona mhubiri huyo mlimani alikopiga kambi na kushirikiana naye katika maombi, ingawa baadhi yao wamekuwa wakimkejeli,kwamba anatafuta umaarufu, jambo ambalo amekuwa akilipinga kwa nguvu zote.

  Kwa mujibu wa uchunguzi huo, kwa siku amekuwa akipokea watu kati ya 100 na 150 wanaokwenda kumwona mlimani hapo wakati wa maombi na wengine wakishiriki naye kuimba nyimbo za sifa na kuomba.

  source: Aliyekaribishwa Ikulu ampa JK sharti la kupanda mlima[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Mromboo

  Mromboo JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 728
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Haya JK kama ulivyofuatwa Ikulu na Baiskeli wewe nenda Kilimani. Uamuzi ni wako eidha kwa Bajaji, Helkopta, V8 au Boeing.
   
 3. SIM

  SIM JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 1,642
  Likes Received: 792
  Trophy Points: 280
  Ngoja kwanza tupige ramli tuone upepo ukoje huko ndipo tumruhusu rais wetu aende
   
 4. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  It is very unlikely kwamba Rais atakwenda Mlimani kusimuliwa Torati. Mimi namkaribisha huyu Nabii Mussa afike Msasani anieleze maagizo yake aliyoyapata kutoka kwa Baba waw wa Mbinguni. Mimi sitakwenda Mlimani. I do not go to any rendezvous.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  vi hawa mabau hawawezi kukaa mabondeni?? :A S 13::A S 13:
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Yeye ndio amfuate Kikwete magogoni ampe huo ujumbe aliopewa na "Mungu"
   
 7. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tapeli tu huyu; watu kama hawa wanaolaghai watanzania tena wenye kipato cha chini inafaa kuwafunga jela mana ni wezi kama wezi wengine tu
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  MDHARAU MWIBA MGUU HUOTA TENDE!...Tusiishie kudhani kuwa kila kitu ni mizaha!
   
 9. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Ya kaisari mpe Kaisari na ya MUNGU mwachie MUNGU. Tutawatambua kwa matendo yao.
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Anakula bei gani jero au buku kwa kichwa?
   
Loading...