Babu awekewa umeme wa jua LOLIONDO

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Babu awekewa umeme wa jua



Na Said Njuki, Arusha

MCHUNGAJI Ambilikile Masapila ‘Babu’ wa Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha amewekewa umeme wa juu nyumbani kwake na kusema kuwa
umeokoa zaidi ya sh 600,000 alizokuwa akitumika kwa mwezi kwa shughuli mbalimbali na maandalizi ya huduma yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Babu alisema jenereta peke yake ilikuwa ikitumia zaidi ya sh 450,000 kwa mwezi ikiwa ni sawa na sh 15,000 kwa siku, mbali na matumizi ya tochi zilizokuwa zikitumika usiku kucha kuandaa dawa kila siku.

Kampuni ya Ensol (T) Limited ya jijini Dar es Salaam ilifunga mtandao wa
umeme huo wa nguvu ya jua wenye thamani ya sh milioni 4 ikiwa ni sehemu ya
kutambua mchango wa mchungaji huyo kwa taifa, na kuweka taa hadi barabarani kwa ajili ya usalama wa wagonjwa.

Kampuni hiyo pia kampuni hiyo ilimtunukia Mchungaji huyo tuzo maalumu ya kutambua mchango wake kwa jamii katika kuhudumia wagonjwa wa magonjwa sugu kama sukari, saratani, pumu, shinikizo, la damu na UKIMWI.

Akizngumza na gazeti hili jana Msaidizi wake, Bw. Jackson Dudui alisema
kitendo cha kampuni hiyo kuwafungia umeme huo umepunguza gharama za
uendeshaji wa huduma hiyo pamoja na kurahisisha tiba hiyo ambapo kwa sasa
wanaweza kuifanya wakati wowote.

“Tulikuwa tukitumia lita tano za mafuta kwa ajili ya jenereta kila siku sawa na sh 15,000, mbali na betri za tochi tunazotumia wakati wa kuandaa dawa na uchemshaji wake usiku kucha. Kwa kweli tumefarijika hasa baada ya kupunguza gharama za uendeshaji, kwa kweli cha kuwalipa hatuna bali tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awalipe malipo mazuri,” alisema Bw. Dudui.

Akizungumzia maendeleo ya huduma hiyo, Bw. Dudui alisema tiba inaendelea
vizuri na kwa sasa wamekuwa wakitoa huduma kwa idadi kubwa zaidi ambayo ni
kati ya wagonjwa 3,000 hadi 6,000 kwa siku na hiyo inatokana na kuboreka kwa miundombinu.

Alisema dawa zimekuwa zikichambuliwa kwa wakati kutokana na kuwepo kwa
mwanga usiku kucha, zimekuwa zikichemshwa kwa usalama zaidi pia pia kuwepo
kwa mazingira ya usalama katika maeneo yanayowazunguka, ni baadhi tu ya
vichocheo vya kutoa huduma hiyo kwa ufanisi zaidi.

Naye Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni hiyo, Bw. Godwin Msigwa alisema lengo ni kuhakikisha Mchungaji Masapila anapata mwanga bora, salama na wa uhakika ambapo pia anaweza kuchaji simu yake huku akiwa na uhakika wa kufanya kazi zake kwa ubora zaidi.

“Ensol inatambua juhudi za Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata
huduma bora katika nyanja mbalimbali na kwa kuwa serikali inatambua mchango wa mchungaji huyo kwa jamii nasi tumeonelea tuunge mkono juhudi hizo kwa kufunga umeme wa jua nyumbani kwake ili tu kumrahisishia shughuli zake kwa ujumla,” alisema Bw. Msigwa.

Ensol (T) Limited ni kampuni ya uuzaji na ufungaji wa vifaa na mitambo ya
umeme wa jua nchini na imekuwa ikijishughulisha kwa kufunga mitambo hiyo
katika taasisi na sehemu mbalimbali nchini hususan zile hazina nishati ya
umeme wa kawaida.
 
habari njema.serikali itambue mchango wa babu kwa kuboresha huduma za wananchi wa loliondo.wanapata faida kubwa kama wilaya wamefanya nini?
 
wote hawa wezi tu, wamepata kikombe ndio wanajifanya wakarimu, kumbe pesa ya kusaidia watanzania hipo, sasa kwani hospitali (zahanati) vijijini hazina umeme wa jua
 
Back
Top Bottom