Babu aliyetaka CCM ife kabla yake na kushangiliwa kwenye TV agongwa na gari na kufariki...

Hoja iko wapi hapo? Kwamba CCM ni wachawi? Mods mnatoa uhuru uliopitiliza kwa kuruhusu imani hasi kama hizi kupenya kwenye hii site. Hili jukwaa limefanyiwa marekebisho lakini hata sioni faida yake. Sasa hii ilete hisia kwamba watu wote waliokufa wiki iliyopita, mwezi uliopita au mwaka uliopita wamerogwa na CCM?

Hili ni jukwaa la kijamii, yote yanayohusu jamii yatazungumzwa mkuu, wewe ndio unataka kupenyeza hizo imani maana kwa post moja tu, umeongea mengi sana.

Du!!,mbona yule mtaalam wao alishafariki since May au tayari mrithi wake keshapatikana?

Sina hakika endapo nimekuelewa; hata hivyo nina uhakika kwa 100% kwamba wewe hujanielewa!! NINA HOFU; NAOGOPA!!

Hili jamvi hivi sasa limekumbwa na gonjwa baya sana ambalo linatutafuna wana-jamvi!!! Nina hofu maradufu kwavile sikutarajia kwamba hata mkuu MKJ nawe ama unanyemelewa au tayari limeshakukumba gonjwa hilo!! Prove me wrong! u know what? Hivi sasa imefikia mtu akizungumza chochote +ve abt CCM au CDM basi mtu huyo anaitetea CCM au hiyo CDM!!!! Come on men!!

Sizani kama thread yako inahitaji mtu awe na shahada ya GREATER THINKING ndipo afahamu kwamba inalenga kuonesha kifo hicho kina dalili za kuwa na mkono mtu!!! So, kama hoja ambazo zinapamba thread hiyo ni kwamba huyo aliikosoa vibaya CCM na serikali yake sasa ni nani basi anaweza kuwa first suspect (as per ur thread) endapo itaonekana kuna mkono wa mtu?! Sasa mtu akiwa na mashaka endapo kweli CCM/serikali wanaweza kupoteza muda kwa mtu kama huyo ambae sio influencial kivile huko ndo kuitetea CCM??!!

Tell me bro; sio kwamba kale kagonjwa nilikokataja hapo juu kanaanza kukunyemelea au ndo ushaathirika nako?! I wouldn't bother if could be someone else; but u?! no plz, stop it!

Na wewe kwa nini upate hofu na kuogopa? Kwani wewe unaufahamu ukweli kuliko sisi kuhusu kifo cha huyo marehemu? Tuambie bwana, labda wewe unaufahamu wa ziada, maana waswahili tunasema "asifuye mvua imemnyea". Watu tujifunze kutumia masikio kusikia, macho kuona, na kisha ubongo kujumlisha dots. Ukianza kukanusha taarifa iliyotolewa nyuma yake kuna mambo mawili 1. huenda wewe una data sahihi zaidi zinazopingana na taarifa iliyotolewa, ni vyema ukazitoa ili tuzipime na sisi tubadili imani. 2. ama wewe ni mhusika direct or indirect wa tukio hilo na hivyo usingependa ukweli ufahamike. Na utaendelea kutoa maelezo tatanishi, au hisia za uongo ili kuhafifisha ukweli usipokelewe. Mimi hujanishawishi kitu.

Sasa nani ataishi milele kwenye hii dunia? Na wewe mleta mada ukifa leo jioni, kesho watu watapost hapa kwamba umafia wa CCM umehusika kwasababu (jana) yaani leo ulileta mada inayohusisha kifo cha huyo mzee na CCM. Watu wengi watashangalia lakini baadhi watalia, ingawa CCM itadumu milele. Kwa maslahi ya chama, kipi ni nafuu zaidi? Kifo cha huyo mzee au kufedheheshwa kwa CCM?
hapo kwenye red inaashiria akili imegandishwa kama wale samaki wa japani wenye sumu! CCM lazima ife...sooner or later!

Umezungumza kwa uhakika mkubwa kwlei (absolute certainty) unajua aligonjwaje, wapi, na nani, na vipi? Vipi kuhusu huduma aliyopewa na majeraha aliyosuffer? au kwa mfano familia waliambiwa nini na madaktari kuhusu hali ya mgonjwa?

Inaelekea una taarifa kamili, tupatie basi nasi tujue.

Faiza,hebu tujuze vizuri maana baada ya yule mzee kutoa ile kauli ulikuja juu sana na ukasema atakufa kabla ya CCm ukitolea hata mfano wa Nyerere.Vipi haujashiriki kwenye huo mpango mkakati kweli?

kwa hiyo na nyerere alivyosema atamuona raisi wa awamu ya nne na badala yake kafa kabla ya kumuona kulikuwa na mpango mkakati siyo!

Yule Mzee alitoa Hisia Zake!! Hata wanaokufa wakati wowote ungewafuatilia utakuta muda mfupi au wakati wowote uliopita wameongea na watu na kutoa yaliyo moyoni!! Ila tungependa kujua gari lililohusika katika Ajali Numba zake je ni dereva wa daladala? Je Mzee aligongwa saa Ngapi? Just to Know the connection of the accident we can connect dots!! Ila kwa pale Ubungo Uvukaji wa Pedestrians ni wa Hatari Kuliko Maelezo!! Ila naona wahusika wamefumba Macho Hadi watoto wao wagongwe!!
Just to know the ownership of the vehicle involved!! Unaweza Kukuta ni dereva Mzembe amemchukua Mtu Muhimu katika kipindi Hiki!!

Naona. Watakuwa waliona uchuro wakaona ngoja atangulie yeye mbele za haki!
Kwani sisiemu bado ipo ! kilichopo ni mkusanyiko wa magenge yenye imani tofauti na ile tuliyoambiwa Feb. 1977 , uwepo wa magenge haya ni uthibitisho tosha kuwa chama kilishajifia kabla ya mzee kufikwa na mauti .

Hii ndiyo laana yetu watanzania, kufikiri juu ya uchawi kabla ya kitu kingine. Adui wa maendeleo ya mwafrika ni mwafrika mwenyewe. Inashangaza miaka 50 baada ya uhuru, imani za kishirikina bado zinapewa kipaumbele kiasi hiki. Haitashangaza kuona hii thread itaongoza kwa idadi ya wachangiaji leo na kuziacha mada chanya pembeni. Huu ni utumwa na wazungu wanatucheka sana kwa ujinga wetu.

1.Ushirikina ulikuwepo toka Mungu alipo mtupa shetani duniani,na
hautakwisha hadi pale Yesu atakapo rudi,sijui "uhuru wako wa miaka 50" au miaka 100 unahusiana
nini na uchawi,....by the way,ulitegemea uishe miaka mingapi baada ya uhuru?

2.Inaonekana unaabudu sana wazungu,yaani kwako wewe kila kitu wazungu
ndo role model wako,....kwanini usiseme waarabu,wachina,nk?
Kwako kila mzungu anaakili sana eh?
Huo ndo utumwa wa kifikra,set yourself free

Na wewe kwa nini upate hofu na kuogopa? Kwani wewe unaufahamu ukweli kuliko sisi kuhusu kifo cha huyo marehemu? Tuambie bwana, labda wewe unaufahamu wa ziada, maana waswahili tunasema "asifuye mvua imemnyea". Watu tujifunze kutumia masikio kusikia, macho kuona, na kisha ubongo kujumlisha dots. Ukianza kukanusha taarifa iliyotolewa nyuma yake kuna mambo mawili 1. huenda wewe una data sahihi zaidi zinazopingana na taarifa iliyotolewa, ni vyema ukazitoa ili tuzipime na sisi tubadili imani. 2. ama wewe ni mhusika direct or indirect wa tukio hilo na hivyo usingependa ukweli ufahamike. Na utaendelea kutoa maelezo tatanishi, au hisia za uongo ili kuhafifisha ukweli usipokelewe. Mimi hujanishawishi kitu.

I like your signature,...."Envy is a waste of time. You already have all you need

Sasa nani ataishi milele kwenye hii dunia? Na wewe mleta mada ukifa leo jioni, kesho watu watapost hapa kwamba umafia wa CCM umehusika kwasababu (jana) yaani leo ulileta mada inayohusisha kifo cha huyo mzee na CCM. Watu wengi watashangalia lakini baadhi watalia, ingawa CCM itadumu milele. Kwa maslahi ya chama, kipi ni nafuu zaidi? Kifo cha huyo mzee au kufedheheshwa kwa CCM?

Na wewe ukifa leo utajuaje kama CCM itaishi milele?

Hoja iko wapi hapo? Kwamba CCM ni wachawi? Mods mnatoa uhuru uliopitiliza kwa kuruhusu imani hasi kama hizi kupenya kwenye hii site. Hili jukwaa limefanyiwa marekebisho lakini hata sioni faida yake. Sasa hii ilete hisia kwamba watu wote waliokufa wiki iliyopita, mwezi uliopita au mwaka uliopita wamerogwa na CCM?

hayo ni maono yako, kwenye taarifa yake MMM hajausisha chama ama mtu yeyote, so think scholary and nt schoolary.

Back
Top Bottom