BABATI: Mzazi wa mwanamke aliyepigwa risasi 4 na askari wa FFU atoa ya moyoni

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Baba mzazi wa Regina, Daniel Labai akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Oktoba 29,2017 amesema wanatarajia kumzika kesho Jumatatu Oktoba 30,2017 katika Kijiji cha Mamire wilayani Babati.

Labai amesema hawana chochote cha kusema juu ya tukio hilo zaidi ya kumuachia Mungu.
Amesema wanaiachia Serikali kushughulikia suala hilo kwa kuwa mtoto wao ameshauawa.

"Tunatarajia kumzika Regina kesho Jumatatu na baada ya mazishi na kumaliza msiba ndipo tutajua nini kinachoendelea kwenye suala hilo," amesema Labai.

Amesema suala la kesi wanaiachia Jamhuri kwa kuwa ndiyo itakayoisimamia itakapoanza mahakamani na wao watabaki kuwa wasikilizaji.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Longinus Tibishubwamu amesema polisi wanaendelea kumshikilia askari huyo.

Amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani mtuhumiwa
 
dam nzito sana
baba ana uchungu sana na mwanawe na anaamini hakuwa na hatia kwa kuwa alikuwa anadai haki ya mtoto aliyezaa na muuaju( baba mtoto).
hapa tunataraji jamhuru kutenda haki.
 
dam nzito sana
baba ana uchungu sana na mwanawe na anaamini hakuwa na hatia kwa kuwa alikuwa anadai haki ya mtoto aliyezaa na muuaju( baba mtoto).
hapa tunataraji jamhuru kutenda haki.
.....
.....Mkuu tunasafari ndefu sana
 
Naona moyo wa huyu mzee jinsi unavyo tiririka machozi Mungu akupe faraja katika kipindi hiki kigumu
 
Back
Top Bottom