Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Mkurugenzi wa Mashitaka ya jinai nchini l (DPP)amemfutia Mashtaka ya uhujumu uchumi yaliyokuwa yakimkabili Mahakamani mhadhiri wa Chuo kikuu cha SAUT tawi la Arusha, Subilaga Masebo na wenzake wanne.
Akiwasilisha maombi ya kuondoa shtaka hilo, mwendesha mashtaka wa serikali Lusiana Shaban ameiambia mahakama ya wilaya Babati Mkoani Manyara ,upande wa jamhuri haina Tena Nia ya kuendelea na shtaka hilo lililofunguliwa dhidi ya washtakiwa hao.
"Mheshimiwa hakimu ,kesi hii ilikuja Kwa ajili ya kusikilizwa lakini upande wa jamhuri unawasilisha Mbele Yako maombi ya kuliondoa shauri hilo mahakamani"alisema Shaban.
Alisema tunaomba kufanya hivyo kupitia kifungu Cha 91(1) Cha Sheria ya makosa ya jinai, sura ya 20 ya mwaka 2019.Tunaliondoa shauri hili Kwa hiyari bila kushurutishwa na yeyote.
Katika shauri hilo wengine waliokuwa wameshtakiwa ni Hilari Mmbando,Hemed Nyokaa, Ramadhani Hasani na Ally Juma wote wakati wa wilaya ya Babati.
Mhadhili huyo alikuwa akitetewa na wakili Kapimpiti Mgalula wa jijini Arusha baada ya kufunguliwa kesi hiyo ya jinai namba 39/2021 katika mahakama ya wilaya Mkoani Manyara, April 29,mwaka huu yeye na wenzake wakikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 40 .50 yaliyokuwa kwenye gari yake.
Akisoma uamuzi wa kuondolewa Kwa shauri hilo, Hakimu wa wilaya ya Babati Victor Kimaro alisema mahakama yake haina pingamizi na uamuzi wa serikali wa kuondoa shauri hilo mahakamani.
Alisema washtakiwa hao Kwa Sasa wapo huru kuendelea na shughuli zao kama kawaida ,Hata hivyo aliongeza kuwa upande wa mashtaka unaweza kufungua upya shauri hilo wakati wowote itakapotaka.
Akizungumza nje ya mahakama wakili Mgalula alimshukuru DPP Kwa kuwafutia mashtaka watuhumiwa wote kwani aliamini kwamba Mhadhili huyo hakuwahi kuhusika na biashara ya mirungi ukizingatia kwamba yeye ni mhadhili wa Chuo kikuu,taaluma inayoheshimika kwenye Jamii.
Naye Sublaga Masebo ambaye alikuwa mshtakiwa namba moja katika shauri hilo ,alisema katika maisha yake hakuwahi kufanya biashara ya mirungi ila kilichomponza ni kuwapatia lifti kwenye gari yake watu wasiofahamika na baada ya kusimamishwa na askari polisi Watuhumiwa walifanikiw kutoroka na yeye kukamatwa ,hivyo anashukuru mahakama kwa kumwachia huru.
Ends...