Babati: Jela miaka 30 kwa kukutwa na bangi gramu 566.9

Mie binafsi nadhani, watunga sheria wangeliangalia hili swala la bangi kwa mapana.

Iwe hivi, kosa la kukutwa na kiasi kidogo cha bangi mfano kete kadhaa au misokoto, adhabu yake iwe ni faini tu, kama mtu akishindwa kuilipa hiyo faini ndio apelekwe jela.

Idadi ya vijana vijana wanaovuta bangi ni kubwa kushinda hata ya wale wanaokunywa pombe(mtazamo wangu) nadhani mtaani, kati ya vijana 5, watatu ama wanne ni wavuta bangi(hiki ni chanzo cha mapato)

Iwepo tu sheria, ukikutwa na msokoto mmoja faini yake ni 20000, ikiwa misokoto 2 basi ni 2*20000, vivyo hivyo pia kwenye kete.

Watakao kamatwa kama wauzaji, wao wapelekwe mahakamani moja kwa moja na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Hiyo walau itasaidia kuingiza mapato serikalini na pia kupunguza speed ya uuzaji.

Hao mabeberu waliotwambia bange ni mbaya, kila siku wanazidi kuhalalisha huko makwao, jana tu, NEWYORK wametoka kuhalalisha bange kwa matumizi ya dawa, na itachukua miezi 18 pia wahalalishe kwa wavutaji.
 
duuh. mbona kuna watu wanakutwa na shamba zima sijawahi kuona wamepigwa miaka mingi hivi
tofautisha kati ya kukutwa na bangi na mimea ya bangi,ili iwe bangi ni lazima iwe processed tayari kuvutwa,ukimkuta mtu kalima bangi utamshitaki kwa kifungu kingine,kwa sababu ushahidi utakaoletwa ale ni miti,sio bangi
 
Nchi za Afrika sijui tumelogwa. Hivi unamfunga mwenzako kama mtumwa. Hizi ni sheria za kikoloni. Tumekua tunatumia haya majani kama dawa miaka mingi kabla ya ukoloni. Kweli watu weusi tumekosa maarifa. Tunaoneana kama wakoloni wslivyotufundisha.
 
Watu wajiepushe tu na bangi na madawa ya kulevya Sheria za Sasa ni Kali kwelikweli, ila Cha kyshangaza ninakoishi watu wanavuta bangi hadharani bila woga wowote plus mirungi vijana hawajihurumii kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom