Baba Yangu Amebaka Housegirl-Mama Anataka Kuondoka!

Hii ngumu sana ila mtuhumiwa ni muhimu kuface case yake aimalize. Kama mtoto aking'ang'ania police huna la kufanya ila kuna njia mnaweza kutumia kama kumlipa fine, ila najiuliza fine inaweza kufuta machungu ya kubakwa??? Afungwe tu, pole sana kwa masahibu
 
Hili tatizo lako ni kiboko. Anyways kwa upande wangu mimi nafikiria yafuatayo;
1. Kama kuna ushahidi wa msichana kubakwa kutoka kwa daktari+police+mahakamani, basi sheria ichukue mkondo wake.

2. Kama sheria kuchukua mkondo wake inakuwa ni tatizo(kihisia kuwa ni baba), basi jiandaeni kuishi na bomu litakalolipuka any time.
 
polene sana ..ila tafuteni mtu mzima aongee na baba na mama kila mtu kwa wakati wake.......msikae nalo wenyewe kwan mnaweza kuwapoteza wote..pamoja na yote huyo bado ni baba yenu ...amri za Mungu zipo kumi kavunja moja.........so tok to him asije akafa kwa presha hamjuia yalimsibu yapi..hakuna mtu anependa fedheha hata kama ni kicheche(am sorry kwa lugha) ila ana haki pia ya kusikilizwa hawa wasichana bwana wana mambo may be kuna mtu anataka awafanye nyie mtaji.....
 
Wadau wa JF.
Hiki ni kisa cha ukweli kilichotokea wiki iliyopita. Ninakiandika kwa huzuni sana na aibu kubwa. Nilikuwa safarini na niliporudi nimekuta kesi hii inafukuta ikiwa imetokea kama siku 2 kabla ya mimi kuwasili.
Baba yangu ana umri wa miaka 70 plus. Mama yangu yupo Mid 60s. Ilitokea kwamba wana housegirl wa umri wa miaka 18 hivi toka maeneo ambayo hutoa wasichana wengi wa jinsi hii.
Bila kupamba jambo hili, baba yangu amembaka huyu msichana wakati mama hayupo. Msichana alitaka kwenda kushitaki polisi ila aliombwa sana na ndugu zangu asifanye hivyo.
Jambo hili limeleta vurugu kubwa sana nyumbani. Hakuna anayetaka kungea na mzee na mama amesema anafunga mizigo yake arudi kwao (at that age?). Watoto tumebaki tunashangaa hatujui la kufanya maana wale ni wazazi wetu na tunaona aibu hata ku-share na spouses wetu (tunaogopa kumbe nyiye ndivyo mlivyo). Pia watu wa dini unaanzaje kuwaelezea? Tunajiuliza kama huyo binti amepata ujauzito je? Kama akiamua kushitaki polisi je?
Yani sijawahi kupata fedheha kama hii. Hata sisi kwa sisi hatutaki kulizungumzia jambo hili.
Tumsaidieje mama?
Tuokoeje ndoa yao? Mzee hataki kukaa nyumbani safari za hapa na pale haziishi!
Tumsaidieje yule binti wa watu na trauma hiyo?
Naombeni msaada, bila matusi tafadhali. Mbakaji akiwa mbali rahisi kusema - afungwe, ila baba yako unasemaje?


yaani hawa ndo madingi mi naowataka...sio umestafu unakuwa una kazi ya kusimulia hadithi wajukuu kibarazani..haya ndo mambo sasa yaani mama akizubaaa tu unajipindua anakukuta uko nyavuni unatweta tu..nani kasema ng'ombe inaseeka maini?eeeh hisi ni ng'ombe sa ngelengele au alusha? Aminia baba yaani katika hili tupo ukurasa mmoja...
 
Dah mbombo ngafu hapa mpaka nimeishiwa maneno
DA hivi wewe unatoka nyanda za juu? I always admire your contributions, keep it up. Hili suala si jipya, kumbuka maandiko katika Biblia takatifu. Huyo mama apate ushauri nasihi kwani hatakuwa na pa kwenda na asijidanganye, hapo ni kwake na aibu ni ya wote asimkimbie wala kumwachia huo mzigo mumewe na anaweza kuwa chanzo. Nakumbuka kuna wakati bibi yangu alipokuwa anaombwa na babu, alikuwa anakataa katakata, kisa? ni 'mchezo wa vijana, tuwaachie'.
 
Aisee!! pole sana sana. Mimi nadhani tusimhukumu kwanza baba kwani hatujui yaliyojiri mpaka amefikia kufanya tukio hilo. Wengine huwa ni tamaa tu, wengine ushirikina lakini wengine ni kushawishiwa. Ingawa binti amesema wazi kwamba amebakwa na anakusudia kwenda polisi, huenda ipo sababu iliyopelekea akafanya hivyo hasa kama hana tabia tabia hizo.

Nashauri, kwanza ninyi kama wenyewe obvious mnamfahamu baba yenu kama ana tabia ya kupenda dogodogo, kama hana lazima mjiulize kumetokea nini?

Aidha, kwa kuwa wewe ni una familia na ndg zako wengine najua mama atawaelewa, jaribu kumuuliza hivi mama kwani baba ulishawahi kumhisi kuwa na tabia hii hapo mwanzo, akisema ndiyo basi mjue baba yenu ana roho ya tofauti ambayo anahitaji kusaidiwa kisaikolojia, akisema hapana, mjue ni shetani tu anataka kuleta mvurugano katika familia yenu na kusababisha mama kuondoka na hata nyie kumchukia baba yenu! mnachopaswa kufanya, ni kumuomba Mungu kwanza, kisha kama ana kaka yake au ndg wa karibu sana ambaye amempita umri aje aongee naye kwa busara maana huenda na yeye anajisikia vibaya ila hajui atajitetea namna gani.

Msihi mama asiondoke kwani anaweza kusababisha madhara makubwa kwa baba mara atakapoondioka, anaweza jiua akiona aibu yake inaenda kutangazwa kwao mama aat that age? please mama asiondoke na amsamehe kwanza kisha hata yeye mama anaweza kuongea naye akamueleza na huenda kuoma msamaha. Poleni jamani
 
Duh! ngoma nzito, Ila hakuna linaloshindikana kama mtawashirikisha watu waziam wenye hekima kulimaliza hilo.
Pole kwa hilo, ndiyo dunia ya utandawazi
 
Nilitamani kumchapa. kweli anastahili adhabu ila ipi sasa? tumeamua kutoongea naye na kaamua kwenda kunywa pombe zake. Akipata ukimwi umri huo ARVs atazimudu?
We Chupaku,under any circumnstances usije ukarogwa kujaribu kumwinulia mzazi wako mkono,never never never,and I mean never,nshawaona mimi waliowabonda wazazi wao na walikoishia najua mie,usithubu,futa kabisa hiyo njozi!
 
Hapo kwenye ipi kushitakiwa anastahili....fikiria kibabu cha jirani kikikubakia mtoto utafanya nini???Mpeni huyo binti na familia yake haki ya kupata haki!Kama hatoshtaki iwe kwa mapenzi yake na sio shinikizotoka kwenu!
Lizzy kesi za kubaka unatakiwa uripoti hapo hapo wakati mbegu bado ziko ndani na michubuko ni fresh,sasa mpaka Chupaku kapata muda wa kuingia kwenye kompyuta na kusema binti keshaondoka ila wana contact zake,kuna kesi tena hapo?
 
Jamani mi binafsi naona binti wa miaka 18 hawezi kubakwa...alipenda mwenyewe then anataka kumbambikia kesi mzeewa watu,,,,ili wambembeleze walau kw mil kadhaa ili asiende mahakamani.....MIAKA 18 ANGEWEZA KUMSUKUMA HUYO MZEE AKAANGUKIA HUKO.....MANAKE MI DK SLAA NAMUONA MZEE IL ANA MIAKA 63 AFU UYO WA MIAKA 70 JE...?BINTI ALIKUWA NA HAMU HUYOOO
 
Huyu Mzee ana PEPO WA NGONO AU kitaalam SEXUAL MANIAC.

Kwanza ni kum-consell mama na mtoto wapone majeraha, kisha kudeal na MZEE WA MAPEPO.

Huyu mzee anastahili kwenda JELA kutumikia kifungo cha miaka 30, HUKO atakutana na wenye mapepo wenzake WANTAFUNE na yeye aone raha ya kutafuna kwa nguvu. Kisha pepo wake watamtoka au watashika adabu.

wabongo tumekuwa na tabia mbaya sana ya kulea maovu, tunalea na kukingia kifua maovu mengi kuanzia ndani ya familia zetu hadi kwenye ngazi za serikali, ufisadi, umalaya, ufataki,ulevi, n.k. Hii ni aibu kubwa, huyu anatakiwa kuhukumiwa kwa kosa lake hata km ni baba.

Mimi kuna watu ambao siwezi kuwasamehe:

1. MBAKAJI
2. JAMBAZI
3. ANAYETAFUNA WAKE ZA WATU

HAWA ni watu wa kuondoshwa kabisa ktk jamii. kungekuwa nauwezekano wa kuwapeleka sayari yao ingekuwa poa sana. hawafai, msiwaonee huruma.:bange:
Mkuu kwenye red hapo,na anayetembea na waume wa watu unamhukumu vipi huyo? Au mzee ndo ile 'akipiga kelele chiriku anaimba ,akiimba bundi ni uchuro'?
 

Duh! Pole sana......

Ila inavyoonekana huyu mzee ni mchafu sana hata wajukuu zake, wanawe na wakwe zake anaweza kuwabaka!!!

Hebu fikiria sasa kama huyo baba yako angekua amembaka binti yako wa kumzaa ungemsamehe!!!????? Je ungeendelea kuuficha ukweli????

Natafakari nitarudi nikipata ushauri mzuri
 
Chupaku
Hii thread nimeiona ila nilishindwa kucomment kwa sababu ni ngumu but ninapenda kushiriki nawe mawili matatu
1. Jua kuwa Baba anajutia sana kitendo alichokifanya (Unless ni tabia yake) hizo safari anazozifanya ni kutafuta mbinu ya siku zipite
2. Huu ni wakati wa Mama kuonyesha ukomavu wakek kwa mumewe......... she should wear that 'stiff face' mbele yenu kwa kuonyesha kuwa she is besides your father (Hata kama huko chumbani wamewekeana mipaka ya mito) watoto msijua (At the age of 60 is she willing to give it up?)
3. Ongeeni taratibu na msichana wa kazi, checkini kama hajapata ujauzito au magonjwa ya kuambukiza (au hajaambukiza) kisha zungumzeni naye out of court, privately and be willing to compensate her with whatever amount/price she name.....................to save the face of the family
4. Then waacheni wazazi wenu wasort out their own messes......msiside na upande wowote.

Pole sana
 
Nahisi Chupaku roho yako ipo kwatu hivi sasa ukisoma jinsi baba yako anavyo chambwa.
 
Mh, pole sana!
Inasikitisha, baba miaka 70??? Kweli dunia imeisha, huyo babako hafai hata kupewa mjukuu. Kaa nae umwulize kwa nini kambaka huyo binti.
 
cha msingi mjipange mmpe ushaur mama ndo jambo limetokea na hyo binti inabidi mnae kwa muda mpk mjue kama n mjamzto au lah mkijua mrudishen kwao ili kulinda ndoa ya mama na mdingi anaona noma
 
Housegirl kaondoka ila tunazo contacts zake bado. Hivi babu wa hivyo unaweza hata kumuacha na mjukuu kweli? AArrrgggghhh

Kwanza poleni sana kwa hilo
Ni wewe tu umeamua kuvunja ukimya na kuanika hapa hadharani. Wahanga wa mambo kama haya wako wengi ingawa huishia kwa ndugu kumalizana kimyakimya. Hebu agalieni sasa adhabu ni kwa huyu binti! Yeye kaondoka! Kaenda wapi? Kijijini! Anaenda kuzeekea kijijini kwao na kwa taswira alokkuwa nayo hatotaka kufanya kazi tena kwa mtu. Je kama familia mlimpa chochote cha kuanzia maisha ama kama kawaida yeye ndiye aliyeonekana mkosaji!

Kwanza ni lazima baba yenu ajue msimamo! Kukaa kimya ni kuogopa na kuendelea kuongeza ufa kwenye ndoa ya wazazi wenu. Ajue amewazalilisha! Yaani uogope kumwambia mzazi wako kuwa hivi sio vizuri? Angekuwa kamlala mkeo ungenyamaza? Mwelezeni hata akiamua kunywa pombe! Mwelezeni! Tena mumwambie umuhimu wa kumwomba radhi mama yenu kwa tabia zake chafu. Msiposema hata wake zenu hawataamini. Likitokea tu watafananisha Like father like son! Jamani hivi mkubwa akikosea haambiwi?
Kuna mzee mmoja haa Moshi namjua! Kamaliza wake za watoto wake woote kahamia kwa wajukuu! Watoto walizoea ndiyo mzee! Hivi ndiyo mzee! Wake zenu mtawaacha hapa nyumbani! Ndiyo mzee! Kuja kustuka wake zao ni wake za baba yao! Wakaishia kufukuza wake zao. Babu sasa kahamia kwa wajukuu!
Mtoto wa kwanza angesema wote wasingeathirika hivi. Mbaya zaidi mama wa hawa vijana alikuwa anaona naye hakuweza kusema! Akadhoofu mpaka mauti yakamkuta.
Sasa mnatakiwa muamue kumsema baba yenu ama kumpoteza mama yenu! Na amini huyu mama akiodoka tu, baba yenu mtamkuta ohio akitafuta binti wa kumpooza na believe mtampoteza mara!
Chukueni hatua haraka.
 
Kwanza kabisa naweza kusema wewe mtoa mada hii ebu niangalie jina lako kwanza... Ooh Chupaku, HUNA ADABU hata kidogo tena naweza kusema umemkosea adabu Mzee wako (I mean Baba yako Mzazi), napata wasi wasi kama huyo uliye muelezea hapa ni baba yako kweli au ni baba wa kambo au wa Kufikia.

Haiwezekani jambo kama ili la kifamilia mshindwe kulizungumzia uko uko nyinyi kwa nyinyi, mpaka ulilete hapa hadharani, kwani unafikiria watu hawakujui wewe Chupaku ni nani? Nikiangalia IP tu hapa najuwa unaandika kutokea wapi na unatumia mtandao gani.

Hivi uko kwenu ukufunzwa adabu na heshima? Ukuambiwa kuwa mambo yanayo husu familia huwa yanatatuliwa kifamimilia!? Hakuna wazee kwenye ukoo wenu, au mzee aliye baki hai ni Baba na Mama Chupaku tu!?

Siku mkeo akikunyima unyumba pia utaleta humu JF ili kupata ushauri? Grow up my friend, this is not funny.

Alafu unadai eti nanukuu "...aibu hata ku-share na spouses wetu (tunaogopa kumbe nyiye ndivyo mlivyo)...."

Sasa unataka kosa la mtu mmoja kuhumiwa ukoo mzima, unacho kiogopa kuongea na wake zenu nini na unacho kifanya hapa ni nini.

Yaani hapa unataka kudhihirisha kuwa wewe unamini watu walioko JF kuliko spouses wenu, familia yako wewe na ndugu zako na hata wazee wa Ukoo wanu.

Maybe you better think twice next time my friend before you just post mambo ya kifamilia.
Mbona kawaida sana mkuu? humu tunashauriana mambo mengi tu na hata kwa ujumla wake ndio yanayoleta maana ya MMU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom